NAOMBA USHAURI: Hizi mbao zilizoko sokoni hapa Dar ni zipi zafaa kwa kupaulia nyumba ya kuishi? naziona kama nyepesi sana

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,011
Habari za hapa kwa wataalam.

Ninampango wa kuezeka nyumba ya kuishi wiki ijayo. Mimi sina uzoefu sana ktk mambo ya building industry hasa roofing. nimepita hapa na pale kupelelez mbao zinazouzwa maeneo mbali mbali hapa Dar nimekutana na aina mbali mbali.

1. pine (misonobali)
2. Cyprus
3. padoo
4. mikaratusi (nimesahau lugha yake ya kisayansi)
5. mihonda (kama sijasahu jina kwa usahihi)

jamani katika makundi yote haya zipi zinafaa kwa uezekaji na kwa nini?

lakink pia swali la nyongeza, nimepewa ushauri ni nununue za size ya 2×2 na 2x4. je hizi zinatosha kwa kuezeka?

wataalam na wazoefu naomba msaada wenu na ushauri zaidi.

wasalaam.
 
Kuwa makini ktk vipimo kwani tape measure za hao wauzaji wanazichakachua sana ili kumuibia mteja so ingependeza uwe na tape measure yako mwenyewe ili huyo muuzaji akimaliza kupima na ww ujiridhishe kama unalipa kwa kipimo halisi nakupa tahadhari you.
 
habari za hapa kwa wataalam.

Ninampango wa kuezeka nyumba ya kuishi wiki ijayo. Mimi sina uzoefu sana ktk mambo ya building industry hasa roofing. nimepita hapa na pale kupelelez mbao zinazouzwa maeneo mbali mbali hapa Dar nimekutana na aina mbali mbali...
Ukipata mbao ambazo zimezoeleka kwa jina la mlingoti utakuwa umefanya jambo la maana mno. Zenyewe haziwekwi dawa. Upate zilizokomaa na utazifuta kwa rangi yake kuwa nyekunyekundu hivi.

Hapo hautawahi kulia juu ya wadudu. Bati zitaisha, utaezeka tena bati huku mbao zako zikiwa vilevile. Mafundi wengi hawawezi kukuombea juu ya hilo ingawa wanazijua ubora wake kwani wanataka mbao laini.
 
Ukipata mbao ambazo zimezoeleka kwa jina la mlingoti utakuwa umefanya jambo la maana mno. Zenyewe haziwekwi dawa. Upate zilizokomaa na utazifuta kwa rangi yake kuwa nyekunyekundu hivi. Hapo hautawahi kulia juu ya wadudu. Bati zitaisha, utaezeka tena bati huku mbao zako zikiwa vilevile. Mafundi wengi hawawezi kukuombea juu ya hilo ingawa wanazijua ubora wake kwani wanataka mbao laini.
ahaa asante kwa maelekezo. na Bei yako sio kali sana?
 
Fundi huyo Hapo mtaalam kinguku hutojuta.

FB_IMG_16208058895091533.jpg


FB_IMG_16208059463129333.jpg


FB_IMG_16208058972530603.jpg


FB_IMG_16208058931952456.jpg
 
ahaa asante kwa maelekezo. na Bei yako sio kali sana?
Bei inaendana tu. Iwapo kuna kuwa na tofauti basi ni kidogo mno. Kama Chanika kwa hapa Dar kuna sehemu unaweza kupata moja kwa elfu kumi. Sasa huo ubao mmoja unapotaka zile za kenchi wanachana katikati na hivyo unapata mbili.

Ni Sawa na kusema ubao mmoja umenunua elfu tano. Vilevile kwa zile za rati, ule ubao mmoja unazalisha mbao mbili na kuwa tatu ambapo ni sawa na kusema umenunua kwa 3350 hivi.

Kuna fundi amebobea sana katika fani ya uezekaji na tena kwa kutumia aina hiyo ya mbao kwa bei nafuu (ndiye aliyeniezekea). Ili ujiridhishe, nashauri uulizie kwa wanaozijua mbao hizo wakueleze.
 
Bei inaendana tu. Iwapo kuna kuwa na tofauti basi ni kidogo mno. Kama Chanika kwa hapa Dar kuna sehemu unaweza kupata moja kwa elfu kumi. Sasa huo ubao mmoja unapotaka zile za kenchi wanachana katikati na hivyo unapata mbili...
inaonekana wewe tayari ni mzoefu nielekeze Fundi anapatikana wapi ni mfate maan aniko hapa hapa Dar Segerea.
 
inaonekana wewe tayari ni mzoefu nielekeze Fundi anapatikana wapi ni mfate maan aniko hapa hapa Dar Segerea.
Fundi anapatikana Chanika. Nitajitahidi Nikutumie namba yake baadae leo hii . Sijajua namna ya kumtumia mtu ujumbe inbox hapa jamii forum. Hakika utazifurahia hizo mbao pamoja na huduma ya huyo fundi.

Ukiona namna alivyoezeka nyumba kwa ubora na kwa mvuto hata huwezi kuamini unafuu wa bei. Mimi alinihudumia kwa laki tisa wakati mafundi wote niliozungumza nao bei zao zilikuwa zinazidi milioni moja na laki tatu. Furaha niliyonayo napenda pia mtu mwingine aipate.
 
Fundi anapatikana Chanika. Nitajitahidi Nikutumie namba yake baadae leo hii . Sijajua namna ya kumtumia mtu ujumbe inbox hapa jamii forum. Hakika utazifurahia hizo mbao pamoja na huduma ya huyo fundi. Ukiona namna alivyoezeka nyumba kwa ubora na kwa mvuto hata huwezi kuamini unafuu wa bei. Mimi alinihudumia kwa laki tisa wakati mafundi wote niliozungumza nao bei zao zilikuwa zinazidi milioni moja na laki tatu. Furaha niliyonayo napenda pia mtu mwingine aipate.
kwa kuwa ni fundi na ni mfanya biashara pia weka namba yake hapa ili na wahitaji wengine wanufaike
 
i hope so!
sasa ndugu hizo mbao kuzipasua vipande vipande si gharama nyingine tena inabidi nilipoe ufundi? au muuzaji mwenyewe ananifanyia hivyo? nipe uzoefu wako
Wauzaji wa hizo mbao wanakuchania hapo hapo kwa mashine. Bei ya kuchana siyo kubwa. Umwone huyo fundi. Akupeleke hapo zinapouzwa ili uulize gharama hasa baada ya fundi kukukadiria mbao zinazohitajika katika boma lako. Ukishafanya tathmini ufanye maamuzi.
 
Back
Top Bottom