Nawashukuru sana wana Jamiiforums, mipango ilianzia hapa na hoja na mawazo niliyapatia hapa hakika tunaishi kwa upendo sana!

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
376
979
Kwanza kabisa naomba nitoe shukrani na samahani nyingi kwa kuchelewa kutoa shukrani kwa msaada mlionipatia hapa na nimerudi hapa pia hakika hapa ni shule na nisehemu ya kujifunza na kuelimika zaidi ya hapo ni mahala ambapo hutakiwi kuishi kiubinafsi mtu anapoleta hija au maoni tusiishie kumcheka wala kumdhihaki tumepeni anachokuwa anakusudia kama ni ushauri tutoe bila ya kumung,unga mambo.

Mwaka 2020 hadi 2021 nilipitia mengi na nilipata wakati mgumu katika utafutaji, nachoshukuru nilibahatika kuchakalika huku na huko mpaka nikawa na kiasi cha Tsh million 12,000,000 fedha halali za kitanzania.

KABLA YA YOTE NILIFANYA HILI KWANZA.
Baada ya kuwa nimepata kiasi hiki cha pesa nilimalizia kuezeka nyumba ambayo niliojenga nyumbani ya vyumba 3 ambayo ilinighalimu zaidi ya million 3.5

20220206_154701.jpg

Mambo mengine niliyomalizia ni mageti, madirisha nikawa nimeishia hapo.

Baada ya hatua hiyo kuona nimeitua nikawa nipo free sas kufanya mambo yangu kwa uhuru.

Ndipo niliamua kwenda kuangalia Biashara.

Tuendelee.
Na katika miaka hiyo miwili sikukaa kizembe kutafuta tu hela hapana nilifanya mambo kadhaa ya kimaendeleo.

Mwaka 2020 nili oa na nikanunua kiwanja kwa ajili ya makazi yangu.

2021 nilikuwa na plan sasa kabla ya kujenga au kufanya kitukingine niwe na biashara ili mambo yawe rahisi. Lakini plan zikagonga mwamba nikajikuta hata pesa niliyonayo haitoshi.

Mfano mzuri ni nilichojifunza ni kuwa na nidhamu na pesa na usibweteke vishawishi ni vingi hasa sisi vijana wa karne hii ya 21.

Niende moja kwa moja kwenye shukrani zangu.

Tarehe 13 Oct 2021 nikaja na wazo tena likisema "Ninahitaji kuanzisha biashara ya vipodozi au vifaa vya pikipiki ila sina uzoefu navyo"

Nov 01, 2021 nilileta hapa wazo ambalo ni " Nina kiasi cha shilingi million 7,500,000 itamaliza ujenzi wa vyumba 3" baada ya kuleta joja hiyo nilipata kupitia comment zenu baada ya kupitia taratibu kuna kitu niliendelea kujifunza ingawa siwezi kuwajibu wote ila mlinipa mawazo mazuri mno nawashukuru sana sana.

Baada ya hapo nikaja tena kwenu kuuliza ilikuwa tarehe 01, Nov 2021 napo nolikuja na hoja hii " Kwa mtaji wa Tsh. Million 7" ambapo niliuliza kwamba "Nina mtaji wa Tsh million 7 naweza kupata msaada wa kitaaramu wa biashara?"

Napo hamkuniacha mlinipa mawazo mazuri sana tena wengine wakanifuata hadi inbox tukajadiliana sana tu.

Nilipata mawazo mengi sana na niwashukuru sana maana hamkujichoka.

Katika yote hayo nilifanya mengine kwa kufuatilia mwenyewe huku nikiweka TAHADHARI mbele zaidi.

Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo,
2021 mwishoni kabisa mwezi wa 10 hivi tarehe za katikati hadi mwishoni wa mwezi huo wa 11. Niliondoka na kwenda Katoro na kufanya litakalowezekana kufanyika kulingana na nafasi itakavyo ruhusu.

Baada ya kufika sikukaa zaidi nilifanya haraka haraka kile kilichonileta ili niwahi kazini maana nikikuwa rikizo fupi ya siku kama 14 hivi baada ya hapo inatakiwa nirudi kazini.

Cha kwanza nilicho fanya, kwenye wazo la VIPODOZI nilimtafuta muuzaji ambae anauza jumla na rejareja pia ni mtu wangu wa karibu sana. Aliniambia ni kweli biashara hii inalipa tena sana tu, isipokuwa mimi kama naanza nikubali kusumbuliwa na TMDA, TBS na TFDA yaani hao huwa hawaishi kutuzungukia kwenye haya maduka yetu na wako na njaa mno usipokuwa makini unaweza kufungua biashara yako ikaisha sababu ya wao kama nimependa hiyo biashara akasema karibu sana.

Mambo yalikuwa mengi na mimi nilimuelewa sana, kikubwa alichonieleza aliniweka wazi katika biashara ya VIPODOZI Mpaka nikaona ni kweli.

Ila ingekuws ni mimi nitakaa kufanya ile biashara ningeweza kupambana na changamoto hizo ila kwa sababu nilitaka lisimamiwe na mke nikaona bado nitakuja kulaumu tu bila kujua nikaona niruke step niende kwenye step ya wazo la wadau la vifaa vya pikipiki.

WAZO LA BIASHARA YA SPEA ZA PIKIPIKI.
Kwenye hii biashara yenyewe sikupata changa moto yeyote zaidi ilihitajika mtaji tu na sehemu ya kuweka biashara maana yenyewe haina mambo ya kuwa na ufuatiliaji kama Vipodozi.
Baada ya kuhamisha wazo na kuja na wazo la vifaa vya pikipiki, kilichobaki ni Flemu ya kuweka biashara na mazingira yawe yenye mzunguko mkubwa kidogo.

Kwa pale Katoro nilienda sehemu moja inaitwa CCM panajulikana sana pale kwa mzunguko wa biashara maana nilihitaji nipate sehemu iliyochangamka kwanza kwa biashara yangu ya spea za pikipiki pale pangefaa maana bodaboda ni wengi sana. Nilitafuta chumba cha biashara kuanzia saa 2 hadi jioni hailikuwa bado ngumu kupata chumba/Flame, kesho yake tena nikaamkiapo bado hali ikawa ngumu mpaka nikatumia DALALI lakini napo nilichemka vyumba vya biashara vikawa dili bhana pale CCM.

Baada ya kuchoka nimekata tamaa kesho yake siku ya 3 napata chumba ila kina masharti, ni kwamba kile chumba kina milikiwa na mpangishwaji ambaye alikuwa akiuza baadae akasimama, akadai aniuzie chumba cha biashara kwa million 2.5 kwa miezi 6 baada ya hapo mkataba utakuwa umeisha naanza kulipia kama kawaida kwa mwenye nyumba.

Nikabembeleza lakini wapi kakomaa na bei yake tena muda huo napiga hesabu muda nao unanitupa mkono, nioichokuja kukifanya huku nitakikosa sasa kama mwendo ndio huu. Jamaa aligoma mpaka tunaachana msimamo ni uleule wa mwanzo alioanza nao, baada ya kuina hilo la CCM limegoma nikahama nikaenda NJIA PANDA ambapo napo kuna centre kubwa tu napo ila watu siyo wengi sana kama CCM napo nikapata mtu anataka kuachia chumba kuongea nae ananiambia yaleyale ya jamaa yulieshindana CCM yeye alikuwa anadai million 2.6 semehu yenyewe haina hata bodaboda nikapiga chini wazo hilo la spea za pikipiki.

Maana niliona pesa niliyonakiwa nayo ni Million 6.5 nikitoa Million 2.5 au million 2.6 nipate chumba nitabakiwa na mtaji wa kiasi gani hapo?

Bado sijalipia TRA, bado ukarabati, bado kununua mzigo bado hapo sijapata chumba cha kuwa na kaa au atakayekuwa anauza ambae ni mke wangu bado, kiukweli nilipiga mahesabu mpaka kichwa kikawa kidogo nikajikuta nasema sasa hapoa nirudi tu nikajipange kivingine tu imeshindikana hili la biashara sasa nisilazimishe.

Katika harakati za kuendelea kutafakari na bado nimekata tamaa, wazo liliniijia kwa haraka haraka nikaona litakuwa sawa nikimshirisha Mama angu anipe mawili matatu. Wazo lenyewe lilikuwa hapohapo Katoro maeneo ya kilimanjaro kwa chini kidogo ndipo nilinunua kiwanja changu nilienda kulitembelea eneo langu nilipofika kwanza nilipotea watu wamejenga mpaka eneo langu limekuwa katikati wakati pindi na nunu hakukuwa na mtu aliye jenga hata mmoja ila baada ya kurudi nikakuta mpaka majirani wamejenga wanakaribu miezi 6+

Baada ya kufika eneo langu nilivutiwa sana na kuanza ujenzi maana nikiangalia kule kweye plan zenyewe zimegonga mwamba bora nijenge tu ili nisije kutumia pesa niliyonayo kwa mambo ambayo sikuyatarajia na shida huwa hazigongi hodi zinakujaga tu kama zinajua hela ipo.

Baada ya hapo nilifanya maamuzi mengine kule kwenye wazo la biashara nika-cancel nikawa na mawazo mengine ambayo niliyatoa kwa mdau mmoja wa hunu Jamiiforums.
IMG_20211109_090116.jpg

IMG_20211109_164514.jpg

Nilianza ujenzi wa nyumba ya vyumba 3 sebure choo cha public, jiko la ndani na semehu ya kulia chakula nayo ilikuwemo lwenye lamani hiyo.

Msingi ulijengwa siku 3 tu na baada ya kunaliza walianza na ujenzi wa shimo la choo walichimba na kulijengelea baada ya hapo nikapata wazo lingine tena mimi shida yangu ilikuwa biashara na pale nimekuta wakazi ni wengi sana na wanahangaika kununua mahitaji ya nyumbani, na sehemu wanakoenda kuhemea ni mbali sana wazo nilaniijia palepale kwanini nisijenge hapa chumba kimoja ambacho nitakigawa kwa pazia pakulala na biashara, wazo likawa zuri Mama akalibariki kwa mikono yote miwili.

IMG_20211112_104522.jpg

IMG_20211112_155333.jpg

Kile chumba kilijengwa kwa siku 3 na siku ya 4 kilipigwa lipu, na bati moja kwa moja yaani mafundi walikuwa wanapiga lipu wengine wako juu wanaweka kenchi kwa ajili ya bati, kufika saa 11 nyumba nikawa nimekabidhiwa mpaka geti kila kitu

Screenshot_20220206-140447_Photos.jpg

Screenshot_20220206-140516_Photos.jpg
Kilicho fuata baada ya siku tatu mke alikuja siku ya nne nikaweka mbao za kuwekea bidhaa na kutenganisha moja kwa moja kile chumba kwa ajili ya kulala na biashara.

SIKU YA TANO
Tukaenda kuhemea vitu vya dukani vyote kila kitu tukaweka dukani siku ya sita nikaondoka kwenda kazini likizo yangu ikawa imefika mwisho.

Kikubwa nilichokuwa nataka kuwashukuru ni ushirikiano wenu hapa na muendelee kufanya hivyo kwangu hata na kwa wengine ambao wanapata fulsa ila wengine huogopa kuleta mawazo yao kwenye Jamii kama hii.

Kuna watu humu wanamitaji ila hawana mawazo watazifanyia nini mpaka anakuja kunaliza ndio anashtuka hana tena pesa.

Mimi nimeshukuru mtandao huu wa Jamiiforums maana sasa niko kwangu pamoja ni chumba kimoja ila msingi wa nyumba kubwa upo nikipata nguvu nitausimamisha na vilevile silipii kodi ya chumba cha biashara.

Biashara imekuwa nzuri maana eneo nililopo niko peke yangu pia kwa siku kama biashara siyo nzuri mke wangu huuza elf 40+ siku ikiwa nzuri huuza hadi elf 50, elf 60 hadi elf 80+ swala la matumizi ya nyumbani nimepumzika na hilo situmi tena pesa ya matumizi yeye mwenyewe anapambana wale mimi huku nakomaa kufanya mengine pale nyumbani.

Na mpaka sasa nimeongeza msingi wa chumba kimoja self na jiko la nje kwa ajili ya kujihifadhi humo ili ni viute nguvu kwenye msingi mkubwa maana ule hauhitaji papala ni pesa hasa inatakiwa ili nyumba isimame.

Yangu yalikuwa ni hayo tu nawashuru kwa wale mliosoma hadi mwisho wa makala hii naimani mmejifunza mengi na mtaendelea kujifunza zaidi na zaidi ahsanteni sana wana Jamiiforums wote.
 
Kwanza kabisa naomba nitoe shukrani na samahani nyingi kwa kuchelewa kutoa shukrani kwa msaada mlionipatia hapa na nimerudi hapa pia hakika hapa ni shule na nisehemu ya kujifunza na kuelimika zaidi ya hapo ni mahala ambapo hutakiwi kuishi kiubinafsi mtu anapoleta hija au maoni tusiishie kumcheka wala kumdhihaki tumepeni anachokuwa anakusudia kama ni ushauri tutoe bila ya kumung,unga mambo.

Mwaka 2020 hadi 2021 nilipitia mengi na nilipata wakati mgumu katika utafutaji, nachoshukuru nilibahatika kuchakalika huku na huko mpaka nikawa na kiasi cha Tsh million 12,000,000 fedha halali za kitanzania.

Na katika miaka hiyo miwili sikukaa kizembe kutafuta tu hela hapana nilifanya mambo kadhaa ya kimaendeleo.

Mwaka 2020 nili oa na nikanunua kiwanja kwa ajili ya makazi yangu.

2021 nilikuwa na plan sasa kabla ya kujenga au kufanya kitukingine niwe na biashara ili mambo yawe rahisi. Lakini plan zikagonga mwamba nikajikuta hata pesa niliyonayo haitoshi.

Mfano mzuri ni nilichojifunza ni kuwa na nidhamu na pesa na usibweteke vishawishi ni vingi hasa sisi vijana wa karne hii ya 21.

Niende moja kwa moja kwenye shukrani zangu.

Tarehe 13 Oct 2021 nikaja na wazo tena likisema "Ninahitaji kuanzisha biashara ya vipodozi au vifaa vya pikipiki ila sina uzoefu navyo"

Nov 01, 2021 nilileta hapa wazo ambalo ni " Nina kiasi cha shilingi million 7,500,000 itamaliza ujenzi wa vyumba 3" baada ya kuleta joja hiyo nilipata kupitia comment zenu baada ya kupitia taratibu kuna kitu niliendelea kujifunza ingawa siwezi kuwajibu wote ila mlinipa mawazo mazuri mno nawashukuru sana sana.

Baada ya hapo nikaja tena kwenu kuuliza ilikuwa tarehe 01, Nov 2021 napo nolikuja na hoja hii " Kwa mtaji wa Tsh. Million 7" ambapo niliuliza kwamba "Nina mtaji wa Tsh million 7 naweza kupata msaada wa kitaaramu wa biashara?"

Napo hamkuniacha mlinipa mawazo mazuri sana tena wengine wakanifuata hadi inbox tukajadiliana sana tu.

Nilipata mawazo mengi sana na niwashukuru sana maana hamkujichoka.

Katika yote hayo nilifanya mengine kwa kufuatilia mwenyewe huku nikiweka TAHADHARI mbele zaidi.

Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo,
2021 mwishoni kabisa mwezi wa 10 hivi tarehe za katikati hadi mwishoni wa mwezi huo wa 11. Niliondoka na kwenda Katoro na kufanya litakalowezekana kufanyika kulingana na nafasi itakavyo ruhusu.

Baada ya kufika sikukaa zaidi nilifanya haraka haraka kile kilichonileta ili niwahi kazini maana nikikuwa rikizo fupi ya siku kama 14 hivi baada ya hapo inatakiwa nirudi kazini.

Cha kwanza nilicho fanya, kwenye wazo la VIPODOZI nilimtafuta muuzaji ambae anauza jumla na rejareja pia ni mtu wangu wa karibu sana. Aliniambia ni kweli biashara hii inalipa tena sana tu, isipokuwa mimi kama naanza nikubali kusumbuliwa na TMDA, TBS na TFDA yaani hao huwa hawaishi kutuzungukia kwenye haya maduka yetu na wako na njaa mno usipokuwa makini unaweza kufungua biashara yako ikaisha sababu ya wao kama nimependa hiyo biashara akasema karibu sana.

Mambo yalikuwa mengi na mimi nilimuelewa sana, kikubwa alichonieleza aliniweka wazi katika biashara ya VIPODOZI Mpaka nikaona ni kweli.

Ila ingekuws ni mimi nitakaa kufanya ile biashara ningeweza kupambana na changamoto hizo ila kwa sababu nilitaka lisimamiwe na mke nikaona bado nitakuja kulaumu tu bila kujua nikaona niruke step niende kwenye step ya wazo la wadau la vifaa vya pikipiki.

WAZO LA BIASHARA YA PIKIPIKI
Kwenye hii biashara yenyewe sikupata changa moto yeyote zaidi ilihitajika mtaji tu na sehemu ya kuweka biashara maana yenyewe haina mambo ya kuwa na ufuatiliaji kama Vipodozi.
Baada ya kuhamisha wazo na kuja na wazo la vifaa vya pikipiki, kilichobaki ni Flemu ya kuweka biashara na mazingira yawe yenye mzunguko mkubwa kidogo.

Kwa pale Katoro nilienda sehemu moja inaitwa CCM panajulikana sana pale kwa mzunguko wa biashara maana nilihitaji nipate sehemu iliyochangamka kwanza kwa biashara yangu ya spea za pikipiki pale pangefaa maana bodaboda ni wengi sana. Nilitafuta chumba cha biashara kuanzia saa 2 hadi jioni hailikuwa bado ngumu kupata chumba/Flame, kesho yake tena nikaamkiapo bado hali ikawa ngumu mpaka nikatumia DALALI lakini napo nilichemka vyumba vya biashara vikawa dili bhana pale CCM.

Baada ya kuchoka nimekata tamaa kesho yake siku ya 3 napata chumba ila kina masharti, ni kwamba kile chumba kina milikiwa na mpangishwaji ambaye alikuwa akiuza baadae akasimama, akadai aniuzie chumba cha biashara kwa million 2.5 kwa miezi 6 baada ya hapo mkataba utakuwa umeisha naanza kulipia kama kawaida kwa mwenye nyumba.

Nikabembeleza lakini wapi kakomaa na bei yake tena muda huo napiga hesabu muda nao unanitupa mkono, nioichokuja kukifanya huku nitakikosa sasa kama mwendo ndio huu. Jamaa aligoma mpaka tunaachana msimamo ni uleule wa mwanzo alioanza nao, baada ya kuina hilo la CCM limegoma nikahama nikaenda NJIA PANDA ambapo napo kuna centre kubwa tu napo ila watu siyo wengi sana kama CCM napo nikapata mtu anataka kuachia chumba kuongea nae ananiambia yaleyale ya jamaa yulieshindana CCM yeye alikuwa anadai million 2.6 semehu yenyewe haina hata bodaboda nikapiga chini wazo hilo la spea za pikipiki.

Maana niliona pesa niliyonakiwa nayo ni Million 6.5 nikitoa Million 2.5 au million 2.6 nipate chumba nitabakiwa na mtaji wa kiasi gani hapo?

Bado sijalipia TRA, bado ukarabati, bado kununua mzigo bado hapo sijapata chumba cha kuwa na kaa au atakayekuwa anauza ambae ni mke wangu bado, kiukweli nilipiga mahesabu mpaka kichwa kikawa kidogo nikajikuta nasema sasa hapoa nirudi tu nikajipange kivingine tu imeshindikana hili la biashara sasa nisilazimishe.

Katika harakati za kuendelea kutafakari na bado nimekata tamaa, wazo liliniijia kwa haraka haraka nikaona litakuwa sawa nikimshirisha Mama angu anipe mawili matatu. Wazo lenyewe lilikuwa hapohapo Katoro maeneo ya kilimanjaro kwa chini kidogo ndipo nilinunua kiwanja changu nilienda kulitembelea eneo langu nilipofika kwanza nilipotea watu wamejenga mpaka eneo langu limekuwa katikati wakati pindi na nunu hakukuwa na mtu aliye jenga hata mmoja ila baada ya kurudi nikakuta mpaka majirani wamejenga wanakaribu miezi 6+

Baada ya kufika eneo langu nilivutiwa sana na kuanza ujenzi maana nikiangalia kule kweye plan zenyewe zimegonga mwamba bora nijenge tu ili nisije kutumia pesa niliyonayo kwa mambo ambayo sikuyatarajia na shida huwa hazigongi hodi zinakujaga tu kama zinajua hela ipo.

Baada ya hapo nilifanya maamuzi mengine kule kwenye wazo la biashara nika-cancel nikawa na mawazo mengine ambayo niliyatoa kwa mdau mmoja wa hunu Jamiiforums.
View attachment 2110076
View attachment 2110077
Nilianza ujenzi wa nyumba ya vyumba 3 sebure choo cha public, jiko la ndani na semehu ya kulia chakula nayo ilikuwemo lwenye lamani hiyo.

Msingi ulijengwa siku 3 tu na baada ya kunaliza walianza na ujenzi wa shimo la choo walichimba na kulijengelea baada ya hapo nikapata wazo lingine tena mimi shida yangu ilikuwa biashara na pale nimekuta wakazi ni wengi sana na wanahangaika kununua mahitaji ya nyumbani, na sehemu wanakoenda kuhemea ni mbali sana wazo nilaniijia palepale kwanini nisijenge hapa chumba kimoja ambacho nitakigawa kwa pazia pakulala na biashara, wazo likawa zuri Mama akalibariki kwa mikono yote miwili.

View attachment 2110078
View attachment 2110079
Kile chumba kilijengwa kwa siku 3 na siku ya 4 kilipigwa lipu, na bati moja kwa moja yaani mafundi walikuwa wanapiga lipu wengine wako juu wanaweka kenchi kwa ajili ya bati, kufika saa 11 nyumba nikawa nimekabidhiwa mpaka geti kila kitu

View attachment 2110089

View attachment 2110090Kilicho fuata baada ya siku tatu mke alikuja siku ya nne nikaweka mbao za kuwekea bidhaa na kutenganisha moja kwa moja kile chumba kwa ajili ya kulala na biashara.

SIKU YA TANO
Tukaenda kuhemea vitu vya dukani vyote kila kitu tukaweka dukani siku ya sita nikaondoka kwenda kazini likizo yangu ikawa imefika mwisho.

Kikubwa nilichokuwa nataka kuwashukuru ni ushirikiano wenu hapa na muendelee kufanya hivyo kwangu hata na kwa wengine ambao wanapata fulsa ila wengine huogopa kuleta mawazo yao kwenye Jamii kama hii.

Kuna watu humu wanamitaji ila hawana mawazo watazifanyia nini mpaka anakuja kunaliza ndio anashtuka hana tena pesa.

Mimi nimeshukuru mtandao huu wa Jamiiforums maana sasa niko kwangu pamoja ni chumba kimoja ila msingi wa nyumba kubwa upo nikipata nguvu nitausimamisha na vilevile silipii kodi ya chumba cha biashara.

Biashara imekuwa nzuri maana eneo nililopo niko peke yangu pia kwa siku kama biashara siyo nzuri mke wangu huuza elf 40+ siku ikiwa nzuri huuza hadi elf 50, elf 60 hadi elf 80+ swala la matumizi ya nyumbani nimepumzika na hilo situmi tena pesa ya matumizi yeye mwenyewe anapambana wale mimi huku nakomaa kufanya mengine pale nyumbani.

Na mpaka sasa nimeongeza msingi wa chumba kimoja self na jiko la nje kwa ajili ya kujihifadhi humo ili ni viute nguvu kwenye msingi mkubwa maana ule hauhitaji papala ni pesa hasa inatakiwa ili nyumba isimame.

Yangu yalikuwa ni hayo tu nawashuru kwa wale mliosoma hadi mwisho wa makala hii naimani mmejifunza mengi na mtaendelea kujifunza zaidi na zaidi ahsanteni sana wana Jamiiforums wote.

Umeandika kwa kutulia na kwa hekima kubwa, asante sana Mura!

Ushauri; mwambie wife awe na kauli nzuri....mafanikio yako mbele yako! Karibu sana Katoro.
 
Ahsante sana Jebel hilo ndio kelele ya kila siku nikifunga nae mahesabu.

Uko Katoro sehemu gani?
 
MAda yako ingekuwa inahusu "Kula tunda kimasihara" ungepata LIKE NA COMMENTS zakutosha Ila Kwavile umepost ishu za maendeleo kama hivi kuna wengine watakuja kuponda....

hongera Sana na MUNGU azidi kukubariki
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom