Naomba Nijitambulishe Kwenu - Big Lady

Naomba Nijitambulishe Kwenu - Big Lady

Hapana hayo maneno yako hayo. Mara "Makubwa", mara "Mwaya". Yamekaa kitaarab taarab hivi. Si unajua tena mwananyamala na taarab ni kama chanda na pete? Unapenda Taarab weye?

Wala. Mimi napenda Gospel Music na Bongo Flavour.
 
Karibu sana! unatumia line gani ya simu nikutafute? tiGo ama vodafasta? Nipo engaged na sipatikani hahahahahaahhahh

Karibu jamvini!

Jamani? Kwa nini unaniambia hivyo?

Natumia Zain.
 
Aisee karibu sana vp kwenye tuktuk unaenea?

Jamani kaka mie sipandi hizo Bajaji Bwana.

Halafu mimi kipicha chako cha mifupa ya kunyata kinanitisha. Si kitoe tu jamani?
 
Big Lady kabla hujajiunga ulivutiwa na nani haswaaaaa?

Mambo mengi tu. Nataka niapate mawazo ya biashara pia na wapi pa kupata mtaji maana mambo si ni kuuliza wanaojua.

Pia napenda habari za Siasa na hata za Mahusiano.
 
Karibu big lady
mie ndo Mod au kiranja hapa, so matatizo yote tuwasiliane kwa PM...afu kwa ushauri nasaa pia ni PM tu usiwe na wasi. Karibu sana dada.


Asante sana Mod. Nimekupata.
 
Big Lady

Mimi ninapost kibao halafu ni premium member, matatizo madogo madogo naongea na MOD tunamaliza. Nitakupunguzia walau posts uwe seniour member


Hiyo Premium Member ndiyo nini. Kweli lakini unapost nyingi sana wewe.

Hee, utakuwa unaandika sana.
 
karibu sana mama, tupo pamoja katika hii jukwaaa letu la kubadilishana mawazo
hope to learn a lot from you. kaka yoko mtui

Asante jamani. Lakini Mtui wewe si mchaga? Mimi wala si mchaga. Sasa kaka yangu kivipi jamani?
 
Big_Lady umekaribishwa vizuri sana sijuhi kwa sababu ya hiyo picha yako au uchangamfu wako, any way karibu sana
 
Waungwana wote hamjambo?

Nimekuwa nikisoma JF na nimevutiwa saaa na michango yenye kuelemisha.

Mimi ni mdada wa umri wa kati niliyeishia sekondari na kujiendeleza.

Naomba ukaribisho wenu.

Asanteni.


Invisible
user_offline.gif

Invisible is around but busy!
Robot
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png

green.png

green_right.png
Join Date: Sat Feb 2006
Location: Here...!
Posts: 5,468
Thanks: 147
Thanked 407 Times in 122 Posts
Rep Power: 100000
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif



Karibu JamiiForums.com (A Welcome Note)
Tunafurahi umetutembelea. Ni faraja kuwa mwanachama wa bodi yetu. Heshimu uliowakuta kwenye bodi hii. Tunawaheshimu wanachama wetu na kuwapa thamani sawa.

Tunatoa UHURU WA KUONGEA. Kama mada inakukuna au kukugusa kwa kiwango ambacho unaona lazima utoe majibu jisajili na kutoa ufafanuzi yakinifu.

Ieleweke kuwa, Yaandikwayo hapa ni mawazo ya wateja wetu na si msimamo wa JamiiForums.com ama vinginevyo. Lugha za matusi hazitavumiliwa!

Tutashukuru pale ukiona jambo baya ukatufahamisha tulifanyie marekebisho haraka kabla hujakashifu au kutoa lawama. Sisi ni binadamu na tuna mapungufu yetu.

JamiiForums Administration

Invisible
user_offline.gif

Invisible is around but busy!
Robot
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png

green.png

green_right.png
Join Date: Sat Feb 2006
Location: Here...!
Posts: 5,468
Thanks: 147
Thanked 407 Times in 122 Posts
Rep Power: 100000
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif



icon1.gif

Mkuu wangu Big Lady

Ukweli ni kuwa siku za nyuma tulijaribu sana kuwafahamisha members kuwa JF haiendeshwi kwa fedha za watu flani bali kwa kujitolea.

Tukatanabaisha wazi kuwa wanachama na wote wenye mapenzi mema inabidi watambue kuwa tuna mzigo mkubwa wa kubeba kwa niaba yao.

Nyakati hizo tulikuwa na wanachama waliojisajili karibia 2,000 hivi na tukasema endapo kila mwanachama (aliyejisajili) angechangia Tshs 10,000/= basi ilimaanisha kuwa tungepata Tshs 20,000/= ambayo kwa wakati huo ingetosheleza kuiendesha JF kwa karibia mwaka mzima bila wasiwasi.

Maisha yakabadilika, Server tuliyokuwa nayo ilikuwa ndogo sana kumbe kulinganisha na uhitaji wa watanzania, balaa lilionekana wazi Mwezi Februari pale Mhe. Lowassa alipokuwa akijieleza Bungeni... Server ikachemsha kubeba mzigo mkubwa.

Kwa wakati huo tukaona ni vema tukaangalia namna ya kuweza kuwashirikisha wanachama juu ya ugumu tunaokumbana nao... Tukalazimika kununua server kubwa zaidi mbili na zenye back up za kila baada ya masaa 6 kwa nyakati tofauti. Tukiwa na uwezo wa kufanya hosting hata BURE kwa website za watanzania.

Hilo likasaidia japo kwa gharama ambazo zilitoka mfukoni mwa mwanachama mmoja! Ndiyo, kulipia server hizo kila mwezi ni karibia $900 na ameendelea kufanya hivyo kwa imani kuwa kuna siku mambo yataenda sawa.

JF inahitaji SANA michango ya watanzania na wote wenye mapenzi mema.

Kuna wanachama ambao humu mnawaona wana usernames ambazo ni bolded, hawa ni Premium Members. Hawa walau wamechangia kwa kiwango cha kuanzia $5 na wawili walau $300 tangu JF inaanzishwa mwaka 2006 (ikijulikana kama JamboForums).

Tangu JF inaanza (2006) mpaka sasa, tumekwishapokea jumla ya US$ 1,450/= toka kwa wanachama waliojisajili na wasiojisajili.

Wengi wa waliohitaji kuchangia walikuwa wanatuma barua pepe nasi tunawapa maelekezo juu ya namna ya kutufikishia michango hiyo.

Ukweli ni kwamba kwa wasio wanachama wa JF wakiwa wanasoma hapa wanaona matangazo mengi ya Google kuliko wanachama waliojisajili.

Dhamira yetu si kuweka matangazo haya ya Google kwani hayaingizi kwa kiwango kikubwa hivyo, watu hawabonyezi matangazo hayo na hivyo income yake inategemea pale mtu atakapokosea akabonyeza tangazo ndipo tupate vijisenti kidogo kwa clicks hizo. Gharama za uendeshaji bado zinatoka mfukoni mwa mtu mmoja mpaka sasa na baadhi ya Premium Members ambao wameendelea kuona umuhimu wa kufanya hivyo.

Mpaka sasa JF ina wanachama waliojisajili karibia 8,000. Endapo waliojili hawa wangechangia walau Tshs 10,000/= kwa mwaka basi inamaanisha JF ingetengeneza Tshs 80,000,000/= kwa mwaka na hivyo tusingeweka matangazo KABISA na tungejitahidi kupata moderators ambao watakuwa wanalipwa kwa kazi yao na wangeifanya kwa umakini mkubwa zaidi.

Ukiangalia katika historia ya Forums nyingi, huwa zinashindwa kuhimili traffic inapokuwa kubwa kutokana na servers kuhitaji umakini zaidi na Forum owners hujikuta wanaona ni mzigo usio na faida hivyo forums hizo kufa.

Tumshukuru Maxence kwa kuendelea kulipia gharama hizi kila mwezi kwa kujitolea mpaka sasa huku akilipia na Chat Server (IRC Server).

Wapo wanachama kama Ogah, Nyambala, SteveD, FairPlayer, Mchukia Fisadi na Phillemon Mikael ambao huchangia walau kila wanapopata wasaa... Hawa nao wamesaidia kwa kiwango kikubwa katika jitihada za kuhakikisha JF inakuwa hewani. Bila kuwasahau wadau waliochangia walau $200 hivi initially kama Mtanzania, Field Marshal ES na Halisi.

Ninachoamini binafsi ni kitu kimoja, Tshs 5,000/= kwa mwaka inawezekana kabisa kwa watanzania tulio na uwezo wa kuingia mtandaoni. Na uzuri, benki zetu Tanzania zinaruhusu mtu ku-deposit Tshs 5,000/= kama kiwango cha chini.

Endapo kuna mwanachama anaguswa (kutoka moyoni) na angependa kuiwezesha JF kuendelea kusimama imara na kufanya vema zaidi bila mizengwe ya kifedha, basi anaweza kukubali kuchangia Tshs 5,000/= walau kwa mwaka.

Benki zetu (hapa naongelea NBC na CRDB kwa haraka) hazikulazimishi unayetuma hela kuandika jina lako la kweli bali lile ambalo ungependa mpokeaji alitambue.

Kwa walio Tanzania wanaweza kuichangia JF kwa kutuma katika akaunti za NBC au CRDB.

Akaunti ambazo tangu awali tulipendekeza zitumiwe ni za Maxence Melo (as the JF Founder) na tukawaomba wanaotuma waandike Nicks za kuweza kutanabaisha kuwa wao ndio walotuma.

Michango inaweza kutumwa kwa njia kuu nne:

Kwa walio nje wanaweza kutumia PayPal au Credit Cards au Debit Cards kwa kufuata link hii ( https://www.jamiiforums.com/payments.php) iliyo kwenye sahihi yangu (linapoonyesha dole gumba) na pindi mchangiaji anapoweka chochote tunakuwa notified nasi tunafanya kuwasiliana na mhusika ili aweze kupandishwa kwenda katika group la Premium Members.

Njia ya pili ni kutumia Western Union au Money Gram na kutuma kwenda kwa Maxence Melo wa Dar es Salaam.

Njia ya tatu ni kutumia Bank accounts za Maxence kama ifuatavyo:

NBC:

Acc #: 033201064359
Jina: Maxence Melo Mubyazi

CRDB:

Account Name: Maxence Melo Mubyazi
Bank: CRDB Pugu Road Branch
Swift Code: CORUTZTZ
Acc No: 01J2092391800

Njia ya nne ni kwa kutumia email ya macdemelo@gmail.com
kwenye hii link: https://www.payoneer.com/webapps/Load/LoadToPage.aspx

Ikumbukwe, SI LAZIMA kuandika jina lako la kweli na SI LAZIMA kwenda mwenyewe bank kutuma pesa hizo (kwani unaweza kumpa unayemwamini na kumpa account details na jina lako ambalo ungependa aandike).

Tunaweza kuandika mengi lakini ukweli unabakia pale kuwa JF inahitaji michango yenu kwa sana tu.

Kwa wenye maswali zaidi wanaweza kuwasiliana na Maxence kupitia namba yake ya simu +255713444649.
 
Back
Top Bottom