Naomba nijibiwe swali langu. Mtaala mpya wa elimu somo la dini

Naomba nijibiwe maswali yangu kuhusu huu mtaala mpya wa elimu.

Jedwali na.4: Somo, umahiri mkuu na umahiri mahususi kwa darasa la iii hadi la vi.

Kipengele na:
8. Elimu ya Dini Itatolewa na viongozi wa dini inayohusika kwa kuzingatia mwongozo utakaotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

. Hili somo la dini litahusisha mafunzo ya dini gani kwa wanafunzi ?

. Utaratibu gani utatumika kwa wanafunzi wasio na dini kuto kushiriki mafunzo hayo kwa kuzingatia uhuru wao kama ulivyo elezwa na katiba ya jamhuri ya muungano ?

. Uandikishaji wa kipengele hiki ulizangatia matakwa ya katiba ya jamhuri ya muungano ?
Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1992 Na.4 ib… 19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
Asiye na dini hatafanya chochote

Somo na dini haliongezi credit kwa hiyo ufanye au usifanye ni sawa tu.

Dini ni ya mtu na Mungu wake sio mitihani yetu
 
Sio hilo tu unafiki wa hawa viongoz mbumbumbu na wenye roho mbaya ni kuendelea kufanya kiswahili kitumike shule za msingi wakat watoto wao wanasona english medium,haya maviongozi yana roho mbaya sana
Tatizo la kiswahili siyo la msingi sana maana secondary tunatumia kingereza ila wanafunzi bado awaelewi masomo ....tatizo ni mfumo wa ufundishaji masomo katika shule za serikali....maana hata ilo somo la kiswahili wanafunzi wana feli ....somo la kingereza lipo toka primary ila wanafunzi wanamaliza miaka 7 bila ya kujua kingereza na secondary wanasoma masomo kwa kingereza na somo la English lipo wanasoma miaka 4 ila wanamaliza awajui kingereza ....tatizo ni ufundishaji siyo lugha.
 
Msingi wa Lugha lazima uanze utotoni sio utu uzima mkuu,hivyo basi lazima English ianzie shule za awali kama Lugha ya kufundishia na Kiswahili kiwe somo ,tuache siasa English ni Lugha ya dunia na maarifa.
 
Hayo unayosema hayawezi kuwa na tija kwa sababu mitaani tunatumia kiswahili ....mwanafunzi kushindwa hesabu primary ni ufundishaji siyo lugha ...lengo la kwenda shule siyo kujua lugha ya kingereza tu ...shule za serikali hata zikitumia English kuanzia primary haziwezi kufanya vizuri ...huo ndiyo ukweli
 
Naomba kuuliza, je hii italazimu shule za kiislam kufundisha biblia na wanafunzi wakristo kutovaa mavazi ya kiislam , kadhalika shule za kikristo kufundisha Quran na wanafunzi wa kiislam kuvaa mavazi Yao husika?
 
Simple logic!

Wanafunzi wa dini kubwa zinazofuatwa hapa kwetu watafundishwa na walimu watakaopendekezwa,wale wasiokuwa na dini huo muda wenzao wanakula pindi wataachwa kufanya yatakayowafaa.

Ama kwa dini zisizokuwa na wafuasi wengi?nadhani nao watakuwa na option hiyo hiyo kama idadi yao itatosha kuitwa darasa nao watafundishwa na mwalimu teuliwa lah hawatoshi nao watafanya mengine.
Mara nyingi Wanafunzi wasiokuwa na dini au wasiopenda kwenda kwenye vipindi vya dini hupata usumbufu sana wakati wa vipindi vya dini. Wanakuwa harassed au kulazimishwa kuhudhuria dini.
 
Haya yatakuwa matumizi mabaya ya pesa za walipakodi
Mzee masheikh wanatafutiwa kazi Angalau na wao wafundishe mashuleni sio misikitini..

Si unajua pesa ndogo madrasa sasa hivi watakula pesa ya kutosha kila mwezi Naamini watafurahi sana..Maalimu
 
Mambo ya ajabu sana, itahitaji utashi mkubwa wa kisiasa na uongozi jasiri sana kukomesha kasumba hii.
KOSA KUBWA KUINGIZA DINI MASHULENI ...SWALI KWANINI DINI ZISIFUNDISHWE SEHEMU HUSIKA....TUTATENGENEZA TAIFA LA WAPUMBAVU AMBAO KILA MTU ANAYE JIHITA MTUME NI MTUME KWAO ..PIA TUTATENGENEZA TAIFA LA WANAFIKI ..... NASHAURI HARAKA SANA SERIKALI IPIGE MARUFUKU MAMBO YA DINI KWENYE SHULE ZOTE ZA SERIKALI NA BINAFSI ZINAZO TOA ELIMU YA DUNIA ....IPIGE MARUFUKU VITU VYOVYOTE VYA KIDINI MASHULENI KUVALIWA KAMA HIJABU AU MISALABA...WAKO WAPUMBAVU WATANIPINGA KWA UPOFU WALIO NAO WA KUSHINDWA KUONA MBELE.
 
Asiye na dini hatafanya chochote

Somo na dini haliongezi credit kwa hiyo ufanye au usifanye ni sawa tu.

Dini ni ya mtu na Mungu wake sio mitihani yetu
Shule nyingi walimu, viranja na wanafunzi wafia dini huwa wanawalazimisha wanafunzi kuingia katika vipindi vya dini.
 
Hii ni hatari,labda kama serikali itafanya kuwatambua walimu iliowaajiri yenyewe ambao ni waumini wa hizo dini. Lkn kusema hizi taasisi za dini ndio ziwaajiri na serikali ilipe,hapo siyo sawa.
Wajanja, walianza kuitaka serikali kuanzisha combination zenye somo la Isamic na Arabic language. Serikali ilipoanzisha kwenye mashule yake ikaacha liwe jukumu la wakuu wa shule zilizoanIsha kupanga walimu kama ilivyoada.
Walivyoona hiyo habari ya serikali kuwatambua walimu wa kiislam ili wafundishe waliiogomea hadi kupelekea waziri akaombe maoni ya mufti. Mufti kashirikiana na mwenzake wa Zanzibar na wale wanaoendesha MMU wakaja na hayo mapendekezo, ya mtaala, vitabu, taasisi ya elimu ya kiislam na kuagiza serikali iwalipe hao walimu wataopendekezwa na taasisi hiyo. Ndo tunasubiri tuone uprofesa wa Mkenda.
 
KOSA KUBWA KUINGIZA DINI MASHULENI ...SWALI KWANINI DINI ZISIFUNDISHWE SEHEMU HUSIKA....TUTATENGENEZA TAIFA LA WAPUMBAVU AMBAO KILA MTU ANAYE JIHITA MTUME NI MTUME KWAO ..PIA TUTATENGENEZA TAIFA LA WANAFIKI ..... NASHAURI HARAKA SANA SERIKALI IPIGE MARUFUKU MAMBO YA DINI KWENYE SHULE ZOTE ZA SERIKALI NA BINAFSI ZINAZO TOA ELIMU YA DUNIA ....IPIGE MARUFUKU VITU VYOVYOTE VYA KIDINI MASHULENI KUVALIWA KAMA HIJABU AU MISALABA...WAKO WAPUMBAVU WATANIPINGA KWA UPOFU WALIO NAO WA KUSHINDWA KUONA MBELE.

Wapuuzi wanaturudisha nyuma na upuuzi wa dini,sehemu za umma kuleta dini ni upuuzi mtupu.
 
Wapuuzi wanaturudisha nyuma na upuuzi wa dini,sehemu za umma kuleta dini ni upuuzi mtupu.
Kuna mambo ya chini chini walifanya jitihada kuingiza hayo mambo kwenye majeshi ila walikataliwa ila jitihada za kuingiza majeshini hijabu zipo mbioni ...walitaka kuanzia JKT wakadai watoto wa kike jkt wajisitili kwa kuvaa hijabu kwenye polisi nako wameingia ka kuwalazimisha vazi la suruali badala ya sketi
 
Back
Top Bottom