Sekondari zisizo za amali zaingia mkenge kufundisha mtaala mpya

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Ndugu wadau,

Wote tunajua kwamba mtaala mpya umeanza mwaka huu 2024 kama ilivyoelezwa mara nyingi na wakuu wa wizara ya Elimu na hadi Waziri mwenyewe.

Kadiri ya maelezo ni kwamba shule za sekondari zitakazoanza na mtaala mpya hasa kwa form one ni zile chache tu zenye mkondo wa amali.

Shule hizi chache ambazo orodha yake tumeiona wote ndizo pekee zitakazoanza na mtaala huo mwaka huu.

Jambo la ajabu ni kwamba zipo sekondari ambazo hazimo katika orodha ya shule za amali lakini eti nazo zimeanza mtaala mpya.

Binafsi sikuamini lakini katika kuulizia wenzangu nimegundua ni kweli kwamba zipo shule zimeshafanya kosa la kuanza kufundishia mtaala mpya wakati siyo shule za amali.

Ndugu wadau, hili ni jambo very serious. Hii maana yake shule hiyo walimu wote na uongozi wote umeingia mkenge kwa kufundisha masomo yasiyotakiwa kufundishwa.

Kwa mfano, shule hiyo inatakiwa ifundishe somo la Civics kwa formo one lakini kumbe kimakosa wanafundisha somo la Historia ya Tanzania la mtaala mpya.

Kwa sababu hii ni hatari na shule hizi zinaweza kuchelewa sana kugundua ni bora tujadili humu na ikibidi tuziorodheshe na kwa kupitia Jamii Forum shule hizo zijirekebishe mapema au wizara ilijue hili iziiingile mapema kabal ya hasara kubwa kutokea.

Kuna tetesi kwamba watenaji wa Halmashauri ya Kibaha wamekosea na wamezipotosha baadhi ya sekondari kufuata mtaala mpya
kwa form one kimakosa.

Hii maana yake shule hizo za Kibaha sasa hazifundishi somo la Civics amacho ni kosa kubwa na kwa kweli ni scandal.
 
Possibly mtoa mada ndio ambaye hujaelewa.

Shule zote zinaanza kutumia mtaala mpya. Ufundishaji umebadilika as well as contents zimebadilika.

Mabadiliko yanahusisha shule zote sio za amali tuuu hata za kawaida.

Mtoa mada jielimishe kwanza
iiiiiiiiiiii!
 
Ungerahisisha sana kwa kuelezea Maana ya Amali/kama ina kirefu chake pia..
Inavyofanya kazi n.k..

Hilo tuu, kuhusu kujichanganya hilo sio shida kwa Tz.
Kitu unachotakiwa ujue wa Tz walicho serious nacho ni Majungu na Unafiki..

NB. Vidada vingi vya Jf ni vijizi na vishirikina.
Amali ni vocational.

Wizara imerudiarudia kueleza hii issue hadi imechoka.
 
Possibly mtoa mada ndio ambaye hujaelewa.

Shule zote zinaanza kutumia mtaala mpya. Ufundishaji umebadilika as well as contents zimebadilika.

Mabadiliko yanahusisha shule zote sio za amali tuuu hata za kawaida.

Mtoa mada jielimishe kwanza
Sio kweli.
 
d03b29c1-a485-4eb3-b8c5-057055f69b5b.jpg

Hiyo “Amali” ndo Vocational education?
 
Back
Top Bottom