Masomo yaongezeka mtaala mpya msingi

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
207
453

Na Halima MlachaAugust 17, 2023

Darasa-la-saba-780x470.jpg

TAASISI ya Elimu Tanzania imetoa mtaala wa elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba 2023.
Muundo wa mtaala huo umebadilika na sasa elimu hiyo itakuwa ni ya miaka sita badala ya saba kama ulivyokuwa Mtaala wa Elimu ya Msingi wa mwaka 2016.
Mtaala huo umezingatia nadharia za ukuaji na ujifunzaji na falsafa ya elimu ya kujitegemea inayosisitiza elimu inayomwezesha Mtanzania ajitegemee na amudu maisha yake ya kila siku.
Muundo wa mtaala unaonesha elimu ya msingi itatolewa kwa miaka sita katika hatua mbili ambazo ni darasa la kwanza na la pili ili kujenga umahiri katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Katika hatua ya pili inaonesha mtaala huo utaanzia darasa la tatu hadi la sita na italenga kuimarisha stadi za KKK na stadi nyingine za maisha.
Mwanafunzi wa shule ya msingi anatakiwa aanze darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka sita na kumaliza darasa la sita akiwa na umri wa miaka 11.
Kwa mujibu wa mtaala huo mwaka wa masomo utakuwa na siku 194 sawa na wiki 39 na umegawanyika katika mihula miwili inayolingana.
Katika kila muhula wiki mbili zitatumika kwa ajili ya upimaji endelevu na tamati.
Vipindi na muda wa ufundishaji na ujifunzaji katika elimu ya msingi utakuwa dakika 30 kwa kila kipindi kwa darasa la kwanza na la pili na dakika 40 kila kipindi kwa darasa la tatu hadi la sita.
Katika eneo la Dira, Malengo na Umahiri wa Jumla, mtaala umelenga kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi na mitazamo chanya, anayethamini usawa, haki na elimu bila ukomo katika kuleta maendeleo endelevu ya kitaifa na kimataifa.
Kwa mujibu wa mtaala huo, maeneo ya kujifunza na umahiri mkuu kwa darasa la kwanza na la pili yamezingatia ujenzi wa lugha, mawasiliano na stadi za hisabati, utamaduni, sanaa, michezo na afya na mazingira.
Kwa darasa la tatu hadi la sita maeneo ya kujifunza na masomo yamezingatia kumjengea mwanafunzi umahiri wa lugha na mawasiliano, hisabati, sayansi ya jamii, sayansi na teknolojia na sanaa na michezo.
Katika eneo la lugha wanafunzi hao watajifunza masomo ya lugha za Kiswahili, Kiingereza, Kichina, Kiarabu na Kifaransa.
Mtaala umeelekeza kuwa katika eneo la sayansi ya jamii watakuwa na masomo ya historia ya Tanzania na maadili, Jiografia na mazingira, hisabati, sayansi, sanaa na michezo.
Aidha, lugha ya kufundishia kwa mujibu wa mtaala huo Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 inaelekeza matumizi ya lugha ya Kiswahili, Kiingereza, Lugha ya Alama Tanzania (LAT) na lugha nyingine za kigeni katika elimu na mafunzo.
Sera inatamka kuwa lugha ya Kiswahili itatumika kama lugha ya kufundishia katika shule zinazotumia Kiswahili na Kiingereza kitatumika katika shule zinazotumia Kiingereza kama lugha ya kujifunzia na kufundishia.
Aidha, masomo ya lugha za Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kichina na Kiarabu yatafundishwa kwa lugha inayohusika.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Elimu katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Lyabwene Mtahabwa mtaala huo umeandaliwa kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023.
Dk Mtahabwa pia alieleza kuwa mtaala umezingatia maoni ya wadau yaliyokusanywa na kuchakatwa kati ya mwaka 2021 na mwaka jana na matokeo ya uchambuzi wa maandiko kuhusu uzoefu kutoka nchi nyingine.
 
Kwa Bongo tatizo la ajira linaanziaga apa kwenye mitaala ovyo.Kwa upande wangu ningependa sana masomo yanayoongeza ujuzi yapewe kipaumbele kuliko masomo mengine.

Masomo kama stadi za kazi na sayansi kilimo (sijui saivi kama yapo) yangefundishwa seriously with passion sizani kungekuwepo na hili tatizo la ajira kama ilivyo sasa sababu kwanza wasomi ni wengi lakini hata ukisema unawapa mitaji kwa baadhi ya kozi walizosoma ni ngumu kujiajiri kwa mitaji duchu imagine mtu kasomea hotel management utampa mtaji gani akafungue hotel eti jamanii.

Lakini ikiwa msomi huyohuyo anafani nyingine kama fundi ujenzi,miundombinu ya maji ,ususi ,ufundi makinikia na fani nyinginezo alizofunzwa pindi anasoma either primary au secondary inakuwa rahisi kwa yeye hata kujiajiri ukiachana na kozi specific alivosomea katika ngazi za chuo na ufundi.

ILA ANYWAY NGOJA TUENDELEE KUIJENGA TANGANYIKA YETU KWA WANASIASA WAPENDA TAKWIMU KULIKO UHALISIA.
 
Back
Top Bottom