Walimu 1832 wa Madarasa ya Awali Wapata Mafunzo Kuhusu Utekelezaji wa Mtaala Mpya wa Elimu Nchini

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
WALIMU 1832 wa madarasa ya awali ambao wameshiriki mafunzo ya Mtaala wametakiwa kuwa watekelezaji wazuri wa Sera iliyoboreshwa yenye kujumuisha mtaala mpya wa elimu nchini.

Agizo hilo limetolewa leo Novemba 19, 2023 na Naibu Katibu Mkuu Or-TAMISEMI Dk.Charles Msonde wakati akifunga mafunzo ya walimu kazini.

Amesena walimu wanapaswa kuwa watekelezaji wazuri ili serikali ifikie malengo ya utoaji elimu iliyo bora.

Pia, amesema kuwa serikali kwa makusudi imeamua kuhakikisha inamaliza kero zote za walimu nchini kwa kutatua changamoto mbalimbali ili wafanye kazi yao kwa weledi.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk Aneth Komba amesema kufuatia kukamilika kwa kazi ya uboreshaji wa mitaala ya elimu kuanzia Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari, anaamini walimu waliopata mafunzo hayo watakwenda kuwapa ujuzi walimu wengine na kuweza kuwa bora katika ufundishaji wao.

Mafunzo hayo yamefanyika kuanzia Novemba 13 hadi 19 katika mkoa wa Iringa ambapo yanatarajiwa kufanyika katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam kwa kuwahusisha walimu wa elimu ya awali nchini.
-
 
Back
Top Bottom