Naomba msaada juu ya tararibu za kufuata na hatua zakufunga ndoa na raia wa kigeni

el_magnefico

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
488
570
Habari wanajamii, kuna rafiki yangu (raia wa Tanzania anataka kufunga ndoa na mpenzi wake ni raia wa Marekani anayeishi nchini kwa kufuata taratibu zote . Hivyo nahitaji kufahamu ni taratibu zipi afuate ili aweze kufunga naye ndoa ya kiserikali.
 
Aende Kwa Mkuu wa wilaya aka bomani...akiwa na vibali vya huyo mwenza wake
Nafahamu hilo la katibu tawala wilaya kama mfungisha ndoa ila nataka kujua upande wa mwanamke je ni vibali gani anatakiwa awe navyo kabla ya kufunga ukiachana na vibali vya kuishi nchini(ambavyo anavyo).
 
Nafahamu hilo la katibu tawala wilaya kama mfungisha ndoa ila nataka kujua upande wa mwanamke je ni vibali gani anatakiwa awe navyo kabla ya kufunga ukiachana na vibali vya kuishi nchini(ambavyo anavyo).
Kitambulisho kinacho mjuulisha mhalisia na kwenda kwa wahusika wanao fungisha ndoa. Hakuna tofauti na kuoa mzaliwa wa Tanzania akisha funga ndoa wawe na cheti cha ndoa cha serikali ili kama atataka kufanya safari kwenda marekani iwe ni ushahidi wao kuwa wao ni mke na mume.
 
Huitaji kibali chochote kufunga ndoa na raia mgeni

Cha umuhimu awe na kibali halali cha kuishi Tz.... haijalishi iwe visiting visa au working permit or whatever
Mahali pa kufungia ndoa ni maamuzi yenu, iwe kidini au kiserikali
 
Back
Top Bottom