Naomba kuuliza jaman wana sheria" hivi ni kosa kwa mmiliki wa carwash kuwauzia maji wananchi wenye uhitaji?

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
2,072
1,697
Habar za usiku huu wana nzengo, mimi ni mmiliki wa carwash somewhere

Kwa bahati mbaya au nzuri pale nilipoweka carwash yangu kuna shughuli kadha wa kadha za kijamii,

Kwa kipindi ambacho nimeanzisha hapakuwa na shughuli yeyote ila sasa kutokana na kuendelea kwa lile eneo ndio ikapelekea uwepo wa shughuli za kijamii wakiwemo na mama lishe

Sasa kutokana na uhitaji wao wa maji, wakaniomba kwamba niwe nawauzia ili waweze kuendeshea biashara zao

Mimi nilikataa kwa kuamini kwamba wataniongezea mzigo wa bili sababu vipesa vyao vidogodogo nitakuwa navitumia na si kuviweka kwa ajili ya kulipia bill

Baadae nikagundua kwamba kitenda cha kuwakatalia kuwauzia ni kuwakwamisha kwenye biashara zao hivyo nikaamua kufanya hiyo huduma nikiamin kama nawasaidia

Sasa bas baada ya kama liwiki limoja akaja jamaa akajitambulisha kama ni mtumishi wa mamlaka ya maji hivyo akaniambia nisiwauzie maji wale wa akina mama kwani ni kosa kisheria hivyo wanaweza wakanikamata

Na wale wa mama wameshazoea na hawana sehem nyingine ya kupata huduma zaid ya pale kwangu

Sasa naomba kuwauliza wana sheria

Jeh! Sheria inasemaje kuhusiana na hili swala la kuuza maji?

Kama sheria inakataza nifanye nini ili niweze kuwasaidia hawa watu wenye uhitaji?

Maana hawana sehem nyingine yeyote ambayo wanaweza kupata hiyo huduma kwa eneo lile

AAksanteni
 
Inaweza isiwe kosa kisheria lakini taratibu za dawasa haziruhusu pia yawezekana huyo ni mtumishi mwenye njaa kwaiyo anauhitaji wa maungo
 
Nenda kawaone Watakupa utaratibu, na Pia utapewa bei elekezi ya kuuza.

Maana kuna bei elekezi kutoka EWURA ambayo maji yanatakiwa kuuzwa na si vinginevyo. Ni kama ilivyo kwenye mafuta ya Petrol, Diesel na mengineyo.

Inawezekana unauza bila kufuata utaratibu wao na Sio Bei elekezi unayowauzia.
 
Nenda kawaone Watakupa utaratibu, na Pia utapewa bei elekezi ya kuuza.

Maana kuna bei elekezi kutoka EWURA ambayo maji yanatakiwa kuuzwa na si vinginevyo. Ni kama ilivyo kwenye mafuta ya Petrol, Diesel na mengineyo.

Inawezekana unauza bila kufuata utaratibu wao na Sio Bei elekezi unayowauzia.
Okay hapo nimekupata mkuu
 
Back
Top Bottom