DOKEZO Baadhi ya Wadau wa Sheria wanapora Haki za wenye uhitaji kwa kuwa wana uelewa mdogo wa Sheria

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Katika pitapitia yangu ya mambo tofauti mtandaoni, nikakutana na post ya JF iliyokuwa na kichwa cha habari “Umewahi kuata Changamoto ya Mazingira ya Rushwa wakati wa Kujifungua?

Nikapata wazo na kukumbuka kitu ambacho naona na ninajua kimekuwa changamoto kwa miaka mingi hasa kwa Wananchi wa kawaida ambao hawana uhusiano au elimu ya mambo ya Sheria.

Kutokana na Wananchi wengi kutofahamu elimu ya huduma za Kisheria na Mahakama kuna Mawakili wengi hutumia fursa hii kuhujumu Wananchi ama kwa kupokea rushwa upande wa pili ili kukwamisha kesi au kuchukua hela wakijua hawawezi kuwasaidia.

Kuna wakati hata Mahakimu nao wanapokea kesi ili kuhujumu hukumu na kupoteza haki ya Mwananchi, wanachofanya kuna wakati ni kuchelewesha hukumu ili mshtakiwa aweze kupoteza ushahidi.

Naomba vyombo mbalimbali ikiwemo Jamii Forums, taasisi za kutetea Haki za Raia zishiriki kwenye kutoa elimu kwa raia hasa wanaoenda kukutana na mazingira ya kesi au sheria kwa faida ya kuwapa angalau mwanga kidogo wa masuala yanayowahusu.
 
Back
Top Bottom