Naomba kufahamishwa bajeti ya Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Tanzania

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
6,602
9,343
Waungwana habari zenu.

Hapo mwishoni mwa mwaka 2021 na mwanzo wa 2022 nchi yetu imepita kwenye sekeseke la mvurugano wa mihimili mikuu miwili ya nchi yetu ambapo Bunge kwa kupitia Spika limeonekana kumshambulia Rais ambaye ni Executive kutokana na yanayodaiwa kwamba hatupaswi kukopa pesa ingali Kuna tozo na Kodi.

Kiufupi ni story ambayo ime-hit sana haihitaji kurudia na kujadili kwamba Nani na Nani walikuwa sahihi.

Jambo kuu ni kwamba mwisho wa siku tumeshuhudia speaker akijiuzulu na kusababisha haja au takwa la kikatiba la kufanya uchaguzi mwingine ili kumpata speaker.

Hivyo mchakato huu unanivuta nifikirie gharama tunazobebeshwa watanzania kutokana na watu wazima hawa kutunishiana misuli kiasi speaker kutojali gharama ambazo anazikataa na ambazo mtanzania ndio anazibeba kulingana na tozo na Kodi anazotaka zifanye miradi ingali anajitoa kusababisha gharama unnecessarily.

Je wandugu, uchaguzi huu mchakato wake hufanyika siku ngapi na wahusika ni kina Nani na wanalipwa kiasi gani?

Najaribu kuangalia gharama ya kuita wabunge wote wakae na kupewa seating allowance ambayo haikuwa planned kwenye budget plus gharama nyingine naona ni zaidi ya bilioni kadhaa tunapigwa kisa ujeuri wa mtu.

Natamani kujua gharama halisi tuweze kufanya assessment ya siasa hizi za majitaka zinavyotugharimu walipakodi.
 
spika ni MTU mdogo sana kwenye uhalisia kuliko kinadharia.

amechomolewa lkn hajavuja dam hata panya...

ingekuwa amechomolewa rais kibabe ungeshuhudia mtiti.
 
Hii mitandao bwana shida sana! Mtu anaposti tu maujinga yanayomjia kichwani! Siku mtaomba gharama za ushungi anazovaa Samia maana anabadilisha kila siku? Hivi ni Serikali gani duniani inatoa gharama ya kila kitu inachofanya kwa wananchi? Hata hizo bajeti bungeni zinajadiliwa kwa mafungu mafungu
 
Hii mitandao bwana shida sana! Mtu anaposti tu maujinga yanayomjia kichwani! Siku mtaomba gharama za ushungi anazovaa Samia maana anabadilisha kila siku? Hivi ni Serikali gani duniani inatoa gharama ya kila kitu inachofanya kwa wananchi? Hata hizo bajeti bungeni zinajadiliwa kwa mafungu mafungu
Kuuliza Si Ujinga.
 
Kuuliza Si Ujinga.
Heri umenisaidia kuhoji maana hata waliohoji kuhusu kipi Bora kuhusu tozo au mikopo walitokea watu wa namna hii na kubeza ilimradi amekopa vi-MB vyake bila kuhususha ubongo.
 
Back
Top Bottom