Idrissa Juma: Elimu ya kupokea Matokeo kwa viongozi wa vyama vya siasa baada ya Uchaguzi iwekwe kwenye Sheria

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 14, Kikao cha 2, leo Januari 31, 2024.


"Mchango wangu unajielekeza katika Muswada wa Tume ya Uchaguzi, ninatamani katika kutekeleza majukumu ya Tume ya Uchaguzi ambayo yapo na yameelezwa mengi katika ibara ya 11, ningetamani liongozwe suala la elimu ya kupokea matokeo kwa viongozi wa vyama vya siasa, kushindwa kwa baadhi ya viongozi katika chaguzi ndiyo kinaleta 'kitahalani' katika Taifa kumbe labda kwa sababu hawana elimu,"- Mbunge Abdulhafar Idrissa Juma.

"Moja ya majukumu ya Tume ni kuwafunza wanasiasa kupokea matokeo, wakishindwa wajue huyu ameshindwa, mimi chama changu cha Mapinduzi (CCM) ni wazoefu wa kupokea matokeo ya kushinda na kushindwa pale tunaposhindwa tunahimili tunasubiri miaka mitano mingine, nina wasiwasi na vyama vya upinzani kama wanapewa elimu ya kupokea matokeo ya uchaguzi, sasa nataka nione Tume ya Uchaguzi ina wajibu wa kisheria wa kuwafundisha ukishindwa kubali, tulia, unga mkono juhudi tujenge taifa letu," Mbunge Abdulhafar Idrissa Juma
 
Back
Top Bottom