Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,503
2,980
SPIKA wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakati wa Mkutano wa Bajeti unaoendelea na kwamba Bunge halitachukua hoja zitakazochangiwa na Mbunge kuhusu ripoti ya CAG kwa sababu Mkutano wa sasa wa Bunge ni wa Bajeti na si kujadili ripoti hiyo.

Kwa hiyo tuendelee kuibiwa tu?
Kura za uchaguzi waibe na Kodi zetu waibe?
 
Kwani yeye hajui kilichompata Ndugai kiasi kwamba ajitoe ufahamu kuhusu mamlaka ya muhimili uliojichimbia!? Hizo kazi za Bunge sijui za kuisimamia, kuishauri na ikibidi hata kuiwajisha serikali ni sawa tu na maneno yaliyopo kwenye khanga tu, si kwa hapa Tanzania na tena kwa katiba tuliyonayo hivi sasa!
 
Spika amepotoka CAG anakagua fedha za umma.

Bunge ni kikao cha wananchi na wananchi ndio waajiri wakuu wa watendaji wa Serikali.

Hivyo wanayo haki za msingi kupatiwa majibu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.

Hakuna Sheria iliyo juu ya haki hii ya msingi ya wananchi kufahamishwa kuhusiana na utendaji wa Serikali.
 
PCCB ipo muda wote, kwani lazima ingojee ripoti ya CAG? Hizi ni siasa tu, kama kuna ufisadi kweli PCCB wanafanya kazi gani??
 
Spika amepotoka CAG anakagua fedha za umma.

Bunge ni kikao cha wananchi na wananchi ndio waajiri wakuu wa watendaji wa Serikali.

Hivyo wanayo haki za msingi kupatiwa majibu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.

Hakuna Sheria iliyo juu ya haki hii ya msingi ya wananchi kufahamishwa kuhusiana na utendaji wa Serikali.
Kama unaona ni vibaya sasa nenda huko upinzani...tuachie CCM yetu. Pesa hipo nyingi nchi hii
 
Huyo mwanamke hana akili na ni wa hovyo sana na hakuchaguliwa kuwa naibu spika kipindi cha dikteta Magufuli kwa sababu ya weledi bali kuna mambo mengine yanayohusiana na jinsia yake ndiyo yaliyo mbeba.

Kwenye katiba mpya tunataka spika awe ni mtu ambaye hajawahi kabisa kujihusisha na siasa za vyama kama huyu mwanamke. Bunge la sasa ni kama klabu ya pombe tu halina maana kabisa.
 
SPIKA wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakati wa Mkutano wa Bajeti unaoendelea na kwamba Bunge halitachukua hoja zitakazochangiwa na Mbunge kuhusu ripoti ya CAG kwa sababu Mkutano wa sasa wa Bunge ni wa Bajeti na si kujadili ripoti hiyo.

Kazi ya wizi iendelee
 
Pesa nyingi kiasi hicho zilizofisadiwa wahusika wake ni wengi sana na wengine hawagusiki! Ukilazimisha unakwenda na maji!! Keshaona kwa mbali kuwa ni maji marefu au kawekwa kikao na kuambiwa Tulia TULIA kama lilivyo jina lako. Huko mwezi wa tisa wakubwa watakuwa wamesawazisha mambo na mhemuko wa wananchi kuhusu ufisadi huu utakuwa umepungua sana!! Wewe ukiona Mwigullu Nchemba alipata ujasiri wa kumhusisha Rais ujue kuna kitu kizito hapo!!!
 
Back
Top Bottom