Umpate anayechelewa kama wewe sasa, itakua bomba. Me leo nlikula saa 5 kasoro, na sinaga mda maalumMimi ndo nimetoka kupata bf si muda mrefu kutoka sasa!
Basi churaless but una suraMe nikajua ukikosa pesa, kumbe chura.! Mbona we're churaless na maisha bado ni muswano.!
Baada ya kupitia hili bandiko imenibidi niangalie avatar yako ,nianze kufikirika,ni picha yako au ya kudownload?!! Mimi nishajizoelea kuamka Na kusonga mbele kumtafuta mshiko,sasa unanibadili fikra,sijui nianze kumkurupua bibie asubui aniandalie kifungua kinywa? Ila viumbe kama nyie vinazidi kupotea,Hi guys,
Habari zenu, natumaini mpo salama japo najua hali si shwari, kwani hofu ya corona imetawala kila pande ya dunia, tuendelee kuomba Mungu atulinde wakati huo huo tukifuata maelekezo yote yatolewayo na wizara ya afya..!!
Naomba nitoe hili jambo, katika mfumo wa swali naamini kuna wajuvi wa kutosha humu na watanisaidia barabara katika hili,
Kuna siku asubuhi tulikuwa tupo pahala na baadhi ya wamama watu wazima kama wawili na mkaka mmoja, kila mmoja kaingia mule ndani kwa ajili ya shughuli zake, akaingia mkaka mwingine, alivyomkuta mwenzie pale ndani, akamuambia 'bora hata nimekuona, twende tukapate breakfast, njaa inaniuma mno', na kweli yule mwenzie akamsapoti vyema kabisa kuwa na yeye njaa inamuuma hasa,
Wale wamama wakawashangaa, mmoja akamuambia 'wewe si tumekuozesha tu mwaka Jana? Umeshaanza kutoka nyumbani bila kuandaliwa chai mapema hivyo.!?'
Akacheka, 'hamna bwana nimemuacha amelala sitakagi kumsumbua'.! Mwenzie akachangia kuwa wanatoka wote na mkewe alfajiri na mapema, huo muda wa kuandaa chai asubuhi utatoka wapi.?
Wale wamama wakawasema sema pale, si busara mwanaume mwenye mke kutoka nyumbani bila kupata chochote asubuhi bwaana, wakaongea ongea pale, wale wakaka wakaenda zao.! Kiukweli hata sikuchangia chochote, niliona kabisa hayanihusu, wale wamama wakanigeukia eti 'binti hivyo ndivyo tunavyowafunza mkaishi na waume zenu? Nikajifanya pale 'ujue mama kila familia ina taratibu zake na pia wana makubaliano yao, hivyo kila familia inafanya kile inachoona wao wapo sahihi'.!
Sikutaka kutia comment yoyote katika lile sababu sikujiona kama nipo kwenye position ya ku-judge ama niko na 'eksipiriensi' ya kutosha katika masuala hayo yawahusuyo wanandoa, japo kiukweli sijawahi ona mtu aondoke nyumbani kwa Mama Carleen hata awe mgeni wa kuwahi basi la alfajiri eti atoke bila kutia kinywani chochote kitu, na ndivyo nilivyokuzwa nikaaminishwa hiyo ndiyo busara.!
Je, kiukhalisia kwa kuzingatia mfumo mzima wa maisha yetu ya kudamka hata kabla ya jogoo kuwika hiki kitu kipo applicable? Na kama ni ndiyo, Je, kwa ambao hawafanyi hili, hivi ndiyo inamaanisha kuwa kuna mahali tunafeli sisi kama wanawake?? Japo wanaume wetu baadhi wanaonesha kuridhika na hili, hivii ni kweli wanaume wetu mmeridhika au ndiyo zile za, wacha tu tulisongeshe gurudumu la maisha..??
Bado najiuliza kwanini wanaume wote mnaojiweza tayari mmekwishawahiwa?Mimi katika kitu nisichojali ni hicho, kama niko na ratiba yangu ya kuamka saa kumi nikamsumbue mwenzangu aniandalie chai siwezi kwa kweli. Kama ni muhimu sana huwa naandaa mwenyewe.
Mwanamke ni zaidi ya hayo mambo ya vyakula na kula.
Sent using Jamii Forums mobile app
Haha.![emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mm nimekopy tu hiyo sentesi yako ya mwisho ,maisha yenyewe yako speed Sana haya, kuna vitu vingine sio lazima kufanyika ili kupunguza ugumu Wa maisha,
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha..!Hahahahah inaonekana wewe binti si wakienyeji hufahamu makachakacha serious!!,hivi ni aina ya vyakula visivyo eleweka mapishi yake mfano mtu anapika tambi na maharage Apo tayari ni makachakacha,yai linakangwa dry hata kitunguu halina Apo ni makachakacha
CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
Haha,Baada ya kupitia hili bandiko imenibidi niangalie avatar yako ,nianze kufikirika,ni picha yako au ya kudownload?!! Mimi nishajizoelea kuamka Na kusonga mbele kumtafuta mshiko,sasa unanibadili fikra,sijui nianze kumkurupua bibie asubui aniandalie kifungua kinywa? Ila viumbe kama nyie vinazidi kupotea,
Sent using Jamii Forums mobile app
@carleen watu tunatofautiana sana katika maisha.Ndo maisha ya kisasa wenyewe mnaita
Japo kwa upande mwingine shida aweza kuwa nayo huyo mwanaume(mume wa mtu)
Experience kwa upande wako ipoje Noelia??
Kwakweli nisiwe mnafiki mpaka 'nifurahishwe' ndo nakuwa mtoto mzuri
Mnawaza mengi mpaka mnapitiliza nyie watu
Wooow'..!!Kama mke lazima asubuhi niandae kifungua kinywa kwa mume kabla hajaenda kazini.
Kutokana na mazingira yetu ya foleni kutompa nafasi ya kupata kifungua kinywa kwa utulivu , najiongeza kwa kununua flask ndogo na container ambayo naweza muwekea akale ofisini.
It's a good gesture na kumuonyesha kuwa unamjali afya yake.
Sent using Jamii Forums mobile app