Naomba kuelimishwa kidogo juu ya hili

Naomba kuelimishwa kidogo juu ya hili

uwiii,libarikiwe tumbo lako. Shikilia hapo hapo,naamini ni malezi toka ungali mdogo na hujayubishwa na hawa sijui "motivation speakers"
Amen.
Toka mdg nakumbuka ofisi ya baba haikua mbali so chai alikua anakunywa home asbh....mchana either anarudi kula I'f not bi mkubwa anapack kwenye kikapu tunapeleka ofisini kwa baba.
So hata kwangu najionea sawa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wote mmelala saa 5, mshapiga viroba vyenu...wote mnaamka saa 10, game ya alfaji, mnaamka 11.30, mnatoka saa 12.30....kila mmoja anatoka na bilauri lake la kahawa....kuziandaa ni jinsi mepenavyo...leo yeye kesho mimi...but sio ratiba ni mahaba tuu....on weekend breakfast, lunch and dinner,,,,familia nzima in one table....thats it....
Waoooh'.. Sentensi za mwisho nikiwa mkubwa nataka kama nyie ila huko juu kwenye viroba kiukweli hapana.!!
 
sana unajua inawezekana kabisa....mtu akapoteza pochi lakini kama alifungua kinywa nyumbani anaweza akashinda tu fresh bila kunywa chochote
Honestly speaking Prince ila kama ulivyoona wanaume wengi ndiyo wameridhia kutoandaliwa.!
 
Kusema kweli itategemea. Kama karidhika ni sawa. Mfano wote mnadamka kuwahi daladala mwanaume mwingine anakwambia atakunywa ofisini. Mwingine hata ukijihimu, anakwambia hawezi kunywa chai mapema sana. So it depends
thank you dia..!
Umejibu vyema sana.!
 
Hi guys,
Habari zenu, natumaini mpo salama japo najua hali si shwari, kwani hofu ya corona imetawala kila pande ya dunia, tuendelee kuomba Mungu atulinde wakati huo huo tukifuata maelekezo yote yatolewayo na wizara ya afya..!!

Naomba nitoe hili jambo, katika mfumo wa swali naamini kuna wajuvi wa kutosha humu na watanisaidia barabara katika hili,

Kuna siku asubuhi tulikuwa tupo pahala na baadhi ya wamama watu wazima kama wawili na mkaka mmoja, kila mmoja kaingia mule ndani kwa ajili ya shughuli zake, akaingia mkaka mwingine, alivyomkuta mwenzie pale ndani, akamuambia 'bora hata nimekuona, twende tukapate breakfast, njaa inaniuma mno', na kweli yule mwenzie akamsapoti vyema kabisa kuwa na yeye njaa inamuuma hasa,

Wale wamama wakawashangaa, mmoja akamuambia 'wewe si tumekuozesha tu mwaka Jana? Umeshaanza kutoka nyumbani bila kuandaliwa chai mapema hivyo.!?'
Akacheka, 'hamna bwana nimemuacha amelala sitakagi kumsumbua'.! Mwenzie akachangia kuwa wanatoka wote na mkewe alfajiri na mapema, huo muda wa kuandaa chai asubuhi utatoka wapi.?

Wale wamama wakawasema sema pale, si busara mwanaume mwenye mke kutoka nyumbani bila kupata chochote asubuhi bwaana, wakaongea ongea pale, wale wakaka wakaenda zao.! Kiukweli hata sikuchangia chochote, niliona kabisa hayanihusu, wale wamama wakanigeukia eti 'binti hivyo ndivyo tunavyowafunza mkaishi na waume zenu? Nikajifanya pale 'ujue mama kila familia ina taratibu zake na pia wana makubaliano yao, hivyo kila familia inafanya kile inachoona wao wapo sahihi'.!

Sikutaka kutia comment yoyote katika lile sababu sikujiona kama nipo kwenye position ya ku-judge ama niko na 'eksipiriensi' ya kutosha katika masuala hayo yawahusuyo wanandoa, japo kiukweli sijawahi ona mtu aondoke nyumbani kwa Mama Carleen hata awe mgeni wa kuwahi basi la alfajiri eti atoke bila kutia kinywani chochote kitu, na ndivyo nilivyokuzwa nikaaminishwa hiyo ndiyo busara.!

Je, kiukhalisia kwa kuzingatia mfumo mzima wa maisha yetu ya kudamka hata kabla ya jogoo kuwika hiki kitu kipo applicable? Na kama ni ndiyo, Je, kwa ambao hawafanyi hili, hivi ndiyo inamaanisha kuwa kuna mahali tunafeli sisi kama wanawake?? Japo wanaume wetu baadhi wanaonesha kuridhika na hili, hivii ni kweli wanaume wetu mmeridhika au ndiyo zile za, wacha tu tulisongeshe gurudumu la maisha..??
Kama unataka udumu milele kwenye ndoa yako hakikisha unamuandaria chai mumeo hata kama ni saa 11 alfajiri
 
Huu Uzi umenisaidia kujua wanawake ambao wameolewa humu JF
 
Nilivyoona

Hii "Kufika home saa tatu usiku, kuamka saa 10 asubuhi, kutoka saa 11 asubuhi" ndio imetumika sana kama sababi ilopelekea pia kutumika sana kwa sentensi hii "mfumo wa maisha kubadilika".

Lakini pia nadhani hiyo ni kwa Wakaazi zaidi wa Dar Es Salaam. Kulingana na msongamano wa usafiri.

Swali langu naongezea; Je kwa wale waishio mikoa ambayo inaruhusu kutoka nyumbani saa moja asubuhi na kurudi nyumbani angalau saa moja kasoro jioni, mnajibuje swali la mtoa mada?

Au ndio basi kwa vile inatokea Dar Es Salaam basi ni Tanzania nzima?

Sent using Jamii Forums mobile app
Words..!!
Wakikujibu unitag tafadhali sana..!
 
Back
Top Bottom