Naomba kuelimishwa kidogo juu ya hili

Naomba kuelimishwa kidogo juu ya hili

How I like the way unajua ku-present ideas zako Mr. Titicomb.! you nailed it mkuu..!!
Umeongea kweli tupu, mbio za maisha zimefanya familia nyingi mno wazazi kuwa mbali na watoto wao,
Kila kitu kimebadilika kuanzia malezi ya nyumbani, kwenye jamii mpaka shuleni.!!
Kuna namna ni lazima wazazi wakubali kuendana na hii kasi wakati huo huo wakikazana kuhakikisha watoto wao wakipata makezi bora na lishe bora.!
Umenigusa mpaka nimetoka nje ya mada sema ahsante sana ilikuwa kwa nia njema ya kujenga.!!
Thanks.
I'm humbled mkuu.
 
Changamoto ni Mazoea aliyoyaona binti wakati anakua, kama mama ake alikua anatengeneza chai asubuhi basi ataendelea nayo, vivyo hivyo kwa mwanaume.

kwa upande wangu whatever ni jibu sahihi, sitamlaumu.
Hapa sasa sawa..!
Nimekuelewa vizuri kabisa na wanaume wengi wamesapoti kutoka bila bila majumbani mwao.!!
 
Kwa kizazi hiki naona heshima haipo tena kwenu wanawake ambao mnajiita wake za watu. Kitchen paty zenyu nadhani hamfundishani lolote bali uchuro tu.

Binti ukishakubali kuolewa naomba uelewe kuwa; Siku unavikwa ile pete na kukubali kubadili jina lako ukaitwa Mrs yaani weye ni mali yake. Yeye ndo kichwa kwa kila kitu, Wewe hujui lolote tena bali ngojea uongozi wake tu.

Sasa mtu muhimu hivyo kwako, anaondoka kwenda kusakanya kwa ajili yako, halafu unasema; Nimelala kachemshe chai huko jikoni!!! Kweli au naota?? Nikiisha ondoka weye utakuja chemsha yako au utapika chai yako weye??
Ndio maana wanaume wakionja tu mchepuko huzamia huko huko.

Nina experience na michepuko. Kamwe, mchepuko hawezi kukuambia "Pole kazini" akiwa ameketi kwenye sofa. Atasimama na mkono kanyoosha kukupokea gazeti lako la Mwana spoti.

Huko nyumbani, akikuambia pole unatamani laiti hata angelinyamaza. Hiyo sauti utadhani ni dume limeingia kwako siku hiyo.

Wamama, jifunzeni kunyenyekea. Wanaume tunatamani kubembelezwa. Tumekwazwa kazini, tumepigwa vikumbo njiani, tumechoka halafu hata sauti ya kubembelezwa hatupati?

Mleta hoja; Kama hujaolewa; Ukiolewa usikubali mumeo atoke home bila kunywa chai yenye kitafunwa hata kiporo cha wali kidogo. Hatakaa ale kwa mama ntilie. Utaiponya ndoa yako.

Jitahidi kuamka mapema zaidi kama ni kurudi kulala iwe baadaye akishatoka. Kama mnatoka wote kwenda kutafuta; Wewe amka mapema zaidi huku ukimwandalia vyema. Hatakaa akurupushwe na viruka njia vya ofisini kwake. Atakutafuta mchana mkale wote.
 
Being African lady si sababu ya kubadilisha mtu tabia, ni mabinti wengi sana wa kizazi cha sasa hawajui kufanya kazi za nyumbani, na case ni ile ile malezi na lifestyle!
hakika yatupasa kua makini. Malezi ya hovyo hovyo hupelekea kua na jamii yenye watu wa hovyo hovyo. Mungu atufanyie wepesi.
 
Kwa kizazi hiki naona heshima haipo tena kwenu wanawake ambao mnajiita wake za watu. Kitchen paty zenyu nadhani hamfundishani lolote bali uchuro tu.
Binti ukishakubali kuolewa naomba uelewe kuwa; Siku unavikwa ile pete na kukubali kubadili jina lako ukaitwa Mrs yaani weye ni mali yake. Yeye ndo kichwa kwa kila kitu, Wewe hujui lolote tena bali ngojea uongozi wake tu.
Sasa mtu muhimu hivyo kwako, anaondoka kwenda kusakanya kwa ajili yako, halafu unasema; Nimelala kachemshe chai huko jikoni!!! Kweli au naota?? Nikiisha ondoka weye utakuja chemsha yako au utapika chai yako weye??
Ndio maana wanaume wakionja tu mchepuko huzamia huko huko. Nina experience na michepuko. Kamwe, mchepuko hawezi kukuambia "Pole kazini" akiwa ameketi kwenye sofa. Atasimama na mkono kanyoosha kukupokea gazeti lako la Mwana spoti.
Huko nyumbani, akikuambia pole unatamani laiti hata angelinyamaza. Hiyo sauti utadhani ni dume limeingia kwako siku hiyo.
Wamama, jifunzeni kunyenyekea. Wanaume tunatamani kubembelezwa. Tumekwazwa kazini, tumepigwa vikumbo njiani, tumechoka halafu hata sauti ya kubembelezwa hatupati??
Mleta hoja; Kama hujaolewa; Ukiolewa usikubali mumeo atoke home bila kunywa chai yenye kitafunwa hata kiporo cha wali kidogo. Hatakaa ale kwa mama ntilie. Utaiponya ndoa yako.
Jitahidi kuamka mapema zaidi kama ni kurudi kulala iwe baadaye akishatoka. Kama mnatoka wote kwenda kutafuta; Wewe amka mapema zaidi huku ukimwandalia vyema. Hatakaa akurupushwe na viruka njia vya ofisini kwake. Atakutafuta mchana mkale wote.
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji109][emoji109][emoji109]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kwangu sio tatizo japo anaweza niandalia mda wowote, wakati nikiishi karibu na kazini nilikua napikiwa kila siku ila sasa tumehamia mbali saa 11 kasoro natakiwa niwe kituoni...
Tumepururana usiku adi saa 7 au 8, au tumekurupushana mida ya wanga kwa ajili ya morning glory mda wa kunywa tu hiyo chai haupo tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitaki kwa kweli maana wanaume wana maisha magumu mno walaqhi'.. Bora siye, huwa naona sometimes issa real blessing to be a woman.!
Ah wapi nyie ndio mna ugumu kwenye maisha.. Maana ukikosa chura tuu imekula kwako hahaha
 
Mimi katika kitu nisichojali ni hicho, kama niko na ratiba yangu ya kuamka saa kumi nikamsumbue mwenzangu aniandalie chai siwezi kwa kweli. Kama ni muhimu sana huwa naandaa mwenyewe.
Mwanamke ni zaidi ya hayo mambo ya vyakula na kula.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha..!
So Mr. Sayoo kumbe kuna wengine hamridhiki wakati naona wengi wanasapoti na Mimi nimeshaanza kushangilia kabisa.!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mm nimekopy tu hiyo sentesi yako ya mwisho ,maisha yenyewe yako speed Sana haya, kuna vitu vingine sio lazima kufanyika ili kupunguza ugumu Wa maisha,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikifurahishwa nadamka saa kumi na moja chai tayari ikiwa kinyume kwakweli ni ngumu kupata hiyo mood ya kuamka mapema kuandalia mtu chai

Kwa wageni inategemeana na aina ya mgeni

Itategemea na saikolojia yako ilikuwaje wakati wa kufurahishwa ,na jamaa alitumia mbinu lakini hukifurahi na hapo hutopika chai?
 
Kutokana na mfumo wetu wa maisha na miundombinu mibaya ya usafiri wa kufika kazini wengi hulazimika kutoshiriki kifungua kinywa (breakfast) au chakula cha jioni (dinner) pamoja kama familia.

Kama hakuna kikwazo kama hicho ni kosa kubwa sana kutoshiriki milo hiyo pamoja.
Mkiwa hamjapata watoto inaonekana sio tatizo lakini mazoea hujenga tabia, ina maana mkishapata watoto kuna uwezekano mkubwa sana mkaendeleza tabia hiyo ya kutoshiriki hiyo milo pamoja.

Hii milo ndiyo sehemu nzuri sana za kuitambua familia yako na kujenga desturi na mila, na tamaduni za familia.
Wakati huu ndio sehemu muafaka kugundua kama mmojawapo wa wanafamilia yako ana tatizo lolote lile, sura na uchangamfu wa mtu hueleza mengi sana.

Kuna yana yanayo weza kutokea ndani ya familia yako usiyajue au anayo pitia mtoto wako hapo nyumbani au shuleni ukakosa kuyajua.
Huu ndio muda wa kumfundisha mtoto tabia flani kama kutoongea wakati wa kula n.k.
Huu ndio muda wa kujua mwenza wako hapendi chakula gani au mtoto wako ana tatizo la kiafya kapoteza hamu ya kula n.k.

Family values nyingi hujengwa na kuzungumzwa wakati huu, hapa ndo hukumbushwa vitu walivyo sahau watoto kama kuchana nywele au kunyosha nguo za shule n.k.

Unfortunately mimi mwenyewe wakati mwingi nakosa muda wa hii milo (meal time) pamoja na familia na siku nikikaa nao naona na kusikia mengi sana.

Mapenzi, familia na ndoa ni zaidi ya ngono.

Namkumbuka sana mwalimu flani wa hizi shule za kimataifa Mr. Ryan raia wa kigeni, tulikuwa tunafanya kazi online kwa Team Viewer application, Yeye akiwa mkoani mimi nikiwa hapa Dar, kila siku ikifika saa 12 jioni lazima asitishe kazi anawahi kula chakula (dinner) na familia wakiwa pamoja.

Kuna muitaliano flani pale Mikocheni Reagent Estate ana sehemu yake kama Pub anauza vinjwaji na nyama za kuchoma au kuku, ikifika saa 12:30 jioni anaandaa meza moja kwenye vibanda vyake vya makuti kwa ajili ya dinner, muda huo hata uje na oda ya milioni haupati huduma mpaka amalize kula yeye na familia yake na wafanyakazi wake.

We were doing the same at home when I was a kid, I remember they used to put me on the table because I was too young to reach my food on top of the dinning table.
My dad would never allow us to converse in middle of the meal or kids never drink too much water before finishing your meal.

Unajua kwanini alitukataza mambo hayo?
Sababu kuongea wakati wa kula unarusha vyakula ovyo toka kinywani ni uchafu na hatari ya kuambukizani COVID-19, pia unaweza kukwamwa au kupaliwa na chakula kooni, au una onesha chakula cha mdomoni ni kinyaa.

Kwanini usinywe maji mengi katikati ya chakula?
Sababu utashiba maji badala ya kushiba chakula kisha utadhohofisha mwili.
Kitaalamu sio vema kunywa maji wakati wa chakula bali unatakiwa ule matunda yenye majimaji kama tikiti au mengineyo, au juice kidogo.

Hivyo ndivyo unafundisha watoto wakati wa chakula, kama vile kutopuliza chai kwa midomo n.k.
Haya tunapuuza, na wamama wengi wa sasa hawapikii watoto chakula nyumbani, wanapenda kuwapa chips ndio maana unakuta mtoto kibonge lakini kinga dhaifu.
Kila siku kwa dokta Massawe pale Morocco kulipia 50K hadi 100K.
Mama anaona uvivu kupika anamwambia baba fulani urudi na chipsi na junk food zingine.

That was too long to be here!
Mtanisamehe wadau hasa Carleen mwenye mada.

NB: Breakfast siyo lazima aandae mama hata mzee baba ukiweza na mila yenu inaruhusu unazama jikoni.
Au mama majukumu yamemzidia na hamna msaidizi unamsaidia wife.
Mkuu umenikumbusha mbali sana, life la utotoni, ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom