Carleen
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 8,592
- 29,545
Hi guys,
Habari zenu, natumaini mpo salama japo najua hali si shwari, kwani hofu ya corona imetawala kila pande ya dunia, tuendelee kuomba Mungu atulinde wakati huo huo tukifuata maelekezo yote yatolewayo na wizara ya afya..!!
Naomba nitoe hili jambo, katika mfumo wa swali naamini kuna wajuvi wa kutosha humu na watanisaidia barabara katika hili,
Kuna siku asubuhi tulikuwa tupo pahala na baadhi ya wamama watu wazima kama wawili na mkaka mmoja, kila mmoja kaingia mule ndani kwa ajili ya shughuli zake, akaingia mkaka mwingine, alivyomkuta mwenzie pale ndani, akamuambia 'bora hata nimekuona, twende tukapate breakfast, njaa inaniuma mno', na kweli yule mwenzie akamsapoti vyema kabisa kuwa na yeye njaa inamuuma hasa,
Wale wamama wakawashangaa, mmoja akamuambia 'wewe si tumekuozesha tu mwaka Jana? Umeshaanza kutoka nyumbani bila kuandaliwa chai mapema hivyo.!?'
Akacheka, 'hamna bwana nimemuacha amelala sitakagi kumsumbua'.! Mwenzie akachangia kuwa wanatoka wote na mkewe alfajiri na mapema, huo muda wa kuandaa chai asubuhi utatoka wapi.?
Wale wamama wakawasema sema pale, si busara mwanaume mwenye mke kutoka nyumbani bila kupata chochote asubuhi bwaana, wakaongea ongea pale, wale wakaka wakaenda zao.! Kiukweli hata sikuchangia chochote, niliona kabisa hayanihusu, wale wamama wakanigeukia eti 'binti hivyo ndivyo tunavyowafunza mkaishi na waume zenu? Nikajifanya pale 'ujue mama kila familia ina taratibu zake na pia wana makubaliano yao, hivyo kila familia inafanya kile inachoona wao wapo sahihi'.!
Sikutaka kutia comment yoyote katika lile sababu sikujiona kama nipo kwenye position ya ku-judge ama niko na 'eksipiriensi' ya kutosha katika masuala hayo yawahusuyo wanandoa, japo kiukweli sijawahi ona mtu aondoke nyumbani kwa Mama Carleen hata awe mgeni wa kuwahi basi la alfajiri eti atoke bila kutia kinywani chochote kitu, na ndivyo nilivyokuzwa nikaaminishwa hiyo ndiyo busara.!
Je, kiukhalisia kwa kuzingatia mfumo mzima wa maisha yetu ya kudamka hata kabla ya jogoo kuwika hiki kitu kipo applicable? Na kama ni ndiyo, Je, kwa ambao hawafanyi hili, hivi ndiyo inamaanisha kuwa kuna mahali tunafeli sisi kama wanawake?? Japo wanaume wetu baadhi wanaonesha kuridhika na hili, hivii ni kweli wanaume wetu mmeridhika au ndiyo zile za, wacha tu tulisongeshe gurudumu la maisha..??