Naomba kuelimishwa kidogo juu ya hili

Naomba kuelimishwa kidogo juu ya hili

Hapo kuna mambo kadhaa.

Watanzania wengi tuna tabia ya kufuatilia sana mambo ya watu, hata wasiotuhusu, hata ya nyumba tusizozijua mahusiano yake yakoje. Maisha hayana formula maalum kwamba hivi ndivyo watu waishi.

Kama watu wazima wanaishi vizuri bika tabu, kwa maamuzi yao, wewe mtu baki ni nani uwapangue waishi hivi au vile?

Kama mwanamke ana maruhani hataki kuamshwa asubuhi, akiamshwa anakuwa na kisirani wiki nzima, na mume anaamua kuepusha kisirani, mtajuaje?

Unaweza kuweka formula watu wote wapande ngazi, kutumia lift ni uzembe.

Halafu ikatokea kuna mtu ana kikema hawezi kupanda ngazi, ukawa umemnyanyapaa.

Kwa hivyo, hata pale tunapoweka sheria za nani afanye nini, tujibakishie sehemu kwamba "labda kuna kitu sijaelewa hapa, nawaachia wenyewe wanaojielewa zaidi".

Mimi nimeamka asubuhi leo (nafanya kazi kutoka nyumbani kwa sababu ya kuepuka Coronavirus) breakfast naiangalia mpaka sasa saa saba muda wa lunch. Nilikuwa sijisikii kula na nikawa nina mikutano ya kazi mingi. Sasa naweza kupata brunch.

Kuna watu wengine wanakula kwa kujisikia njaa, hawali kwa kuangalia masaa.

Sasa kama mtu anatoka nyumbani asubuhi hajajisikia kula breakfast, anajisikia kula mida ya saa nne, hapo napo utamlaumu mwanamke?

Na hata kama wamekubaliana wenyewe mwanamke asiamshwe, mwanamme akapate breakfast kazini, watu wengine hilo linawahusu nini?

Je, wangeambiwa mwanamme ndiye anamtengenezea mkewe breakfast asubuhi, halafu yeye hali anakula baadaye, si ndiyo wangesema kapikiwa limbwata kabisa?

Live your life, and as long as they don't interfere with your life, let others live their lives.

Life is too short for unnecessary investigations into how other people live.

Sent from my typewriter using Tapatalk
Mzee baba huwa napenda sana nondo zako. Tunatofautiana kwenye suala la imani tu
 
Eti dada Kwa nini nimsumbue mtu na usingizi wake kama Mimi sipendi kusumbuliwa ?

Halafu ukute wote sasa ni waajiriwa mnaitajika kuwahi kwenye shughuli zenu in fact hata kama sio muajiriwa ni mama wa nyumbani

akiwahi kuamka akipika sawa akichelewa asipopika pia ni sawa tu naweza nikanywa mgahawani



Na hivi ninavyopenda kula mgahawani kuna mama lishe Fulani site ni fundi wa mapishi nadhani siku nikioa nitakuwa nakula cha usiku tu kwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani kidume kabla ya kuoa nilikuwa najitengenezea chai mwenyewe alafu eti nimeoa nitegemee mke au nigombane nae kisa hajaamka kunitengenezea chai... Hilo kwangu wa sio ishu

Ishu kwangu mie aninyime papuchi tuu. Hapo ndio ajihesabie hana chake.
Kwenye ubora wako wa kutaka papuchi
 
Kwenye ubora wako wa kutaka papuchi
😂😂😂😂 Sasa kwani tunao ili tupikiwe au tuwe na uhakika wakupata papuchi ata kama tumefulia..... Kugegeda ndio raha ya dunia bwana.
 
Yaani mtu ninawahi alfajiri nisubiri chain jamani?Hayo ni Maisha ya zamani sana kwa sasa wala hayawezekani tena.kwa WK end sawa ila kwa WK days ni ngumu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii inawezekana ata kama unatoka SAA 11 alfajir nilijifunza kwa mama angu yaan sa 11 kasoro chai tayar tena kwenye mkaa, anasubiri mister anywe ndo anarudi kulala.
 
Hii inawezekana ata kama unatoka SAA 11 alfajir nilijifunza kwa mama angu yaan sa 11 kasoro chai tayar tena kwenye mkaa, anasubiri mister anywe ndo anarudi kulala.
So nawewe unaweza fanya hivyo dunia ya leo, mwendo mpela mpela? asipo kunywa utajiskia vibaya?
 
Hi guys,
Habari zenu, natumaini mpo salama japo najua hali si shwari, kwani hofu ya corona imetawala kila pande ya dunia, tuendelee kuomba Mungu atulinde wakati huo huo tukifuata maelekezo yote yatolewayo na wizara ya afya..!!

Naomba nitoe hili jambo, katika mfumo wa swali naamini kuna wajuvi wa kutosha humu na watanisaidia barabara katika hili,

Kuna siku asubuhi tulikuwa tupo pahala na baadhi ya wamama watu wazima kama wawili na mkaka mmoja, kila mmoja kaingia mule ndani kwa ajili ya shughuli zake, akaingia mkaka mwingine, alivyomkuta mwenzie pale ndani, akamuambia 'bora hata nimekuona, twende tukapate breakfast, njaa inaniuma mno', na kweli yule mwenzie akamsapoti vyema kabisa kuwa na yeye njaa inamuuma hasa,

Wale wamama wakawashangaa, mmoja akamuambia 'wewe si tumekuozesha tu mwaka Jana? Umeshaanza kutoka nyumbani bila kuandaliwa chai mapema hivyo.!?'
Akacheka, 'hamna bwana nimemuacha amelala sitakagi kumsumbua'.! Mwenzie akachangia kuwa wanatoka wote na mkewe alfajiri na mapema, huo muda wa kuandaa chai asubuhi utatoka wapi.?

Wale wamama wakawasema sema pale, si busara mwanaume mwenye mke kutoka nyumbani bila kupata chochote asubuhi bwaana, wakaongea ongea pale, wale wakaka wakaenda zao.! Kiukweli hata sikuchangia chochote, niliona kabisa hayanihusu, wale wamama wakanigeukia eti 'binti hivyo ndivyo tunavyowafunza mkaishi na waume zenu? Nikajifanya pale 'ujue mama kila familia ina taratibu zake na pia wana makubaliano yao, hivyo kila familia inafanya kile inachoona wao wapo sahihi'.!

Sikutaka kutia comment yoyote katika lile sababu sikujiona kama nipo kwenye position ya ku-judge ama niko na 'eksipiriensi' ya kutosha katika masuala hayo yawahusuyo wanandoa, japo kiukweli sijawahi ona mtu aondoke nyumbani kwa Mama Carleen hata awe mgeni wa kuwahi basi la alfajiri eti atoke bila kutia kinywani chochote kitu, na ndivyo nilivyokuzwa nikaaminishwa hiyo ndiyo busara.!

Je, kiukhalisia kwa kuzingatia mfumo mzima wa maisha yetu ya kudamka hata kabla ya jogoo kuwika hiki kitu kipo applicable? Na kama ni ndiyo, Je, kwa ambao hawafanyi hili, hivi ndiyo inamaanisha kuwa kuna mahali tunafeli sisi kama wanawake?? Japo wanaume wetu baadhi wanaonesha kuridhika na hili, hivii ni kweli wanaume wetu mmeridhika au ndiyo zile za, wacha tu tulisongeshe gurudumu la maisha..??


Matusi ya nini dada yangu, tumia busara.
 
Nimependa hapa jinsi ulivyomalizia. Ok kukujibu tu ni kwamba mfumo wenyewe wa maisha unasupport kuwa hivyo kwa vile hakuna mwanaume anaependa kutoka nyumbani bila kuandaliwa kifungua kinywa na mkewe ampendae.

Wengi wetu ni waajiriwa na hutakiwa tufike vibaruani mapema hivyo tukisema tusubirie kuandaliwa kifungua kinywa tunaweza kuchelewa kazini pia ukizingatia kama usafiri mtu anaotumia ni wa public.

Waajiri (Mabosi) pekee zao ndio wanaosubiri kuandaliwa vifungua vinywa na wake zao tena usikute hata mabosi wengine pia wanahisi watachelewa vibaruani mwao hivyo hujikuta wakipata vifungua kinywa maofisini mwao.
Nawasilisha....




ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
emoji377.png

So nawewe unaweza fanya hivyo dunia ya leo, mwendo mpela mpela? asipo kunywa utajiskia vibaya?
Naweza na napenda ale kabla ajaondoka..ndomana majukumu hayatakiwi kuingiliana mama yake nyumba na kumtunza mume..mnavokazanaga kutaka nasisi tuwajibike kulisha familia ndo mnapo......sana.
 
Nikifurahishwa nadamka saa kumi na moja chai tayari ikiwa kinyume kwakweli ni ngumu kupata hiyo mood ya kuamka mapema kuandalia mtu chai

Kwa wageni inategemeana na aina ya mgeni
hapa ndio mnapoharibu,kutunisha misuli. Me sio mwanachama wa kila kitu afanye wife,i fix my on tea,maji ya kuoga,kubrush,kupasi n.k Lakini kwa kauli hii naweza kukurudisha kwenu,nyoko zako
 
hapa ndio mnapoharibu,kutunisha misuli. Me sio mwanachama wa kila kitu afanye wife,i fix my on tea,maji ya kuoga,kubrush,kupasi n.k Lakini kwa kauli hii naweza kukurudisha kwenu,nyoko zako
Pole kwa yaliyokupata nawa mikono mara kwa mara na epuka misongamano isiyo ya lazima
 
Back
Top Bottom