Naomba kuelimishwa kidogo juu ya hili

Naomba kuelimishwa kidogo juu ya hili

Mara zote najiandalia mwenyewe kitu cha kushtua tumbo asubuhi maana inategemea pombe za jana nimeamka na apetite ya nini,unakuta jana nimepiga pombe kali asubuhi mtoto wa watu akupikie chai na chapati si ntamsimanga tu bure?Mi najua jinsi ya kujitibu
😅😅
Kama ni masuala ya hangover tena, itabidi tu usimamie show mwenyewe hata usimsumbue mama wa watu.!
 
My wife to be, jipange vizuri huko uliko. Mi napenda kula kula, so ni lazima uendane na kasi. Yani nilipe mahari alafu bado nikale kwa mama ntilie? HApana asee
 
wee fanya mpango tuu wa alqasus hamna shida ila sasa usije jikuta unaota ndevu hahahahahaha
Sitaki kwa kweli maana wanaume wana maisha magumu mno walaqhi'.. Bora siye, huwa naona sometimes issa real blessing to be a woman.!
 
Hi guys,
Habari zenu, natumaini mpo salama japo najua hali si shwari, kwani hofu ya corona imetawala kila pande ya dunia, tuendelee kuomba Mungu atulinde wakati huo huo tukifuata maelekezo yote yatolewayo na wizara ya afya..!!

Naomba nitoe hili jambo, katika mfumo wa swali naamini kuna wajuvi wa kutosha humu na watanisaidia barabara katika hili,

Kuna siku asubuhi tulikuwa tupo pahala na baadhi ya wamama watu wazima kama wawili na mkaka mmoja, kila mmoja kaingia mule ndani kwa ajili ya shughuli zake, akaingia mkaka mwingine, alivyomkuta mwenzie pale ndani, akamuambia 'bora hata nimekuona, twende tukapate breakfast, njaa inaniuma mno', na kweli yule mwenzie akamsapoti vyema kabisa kuwa na yeye njaa inamuuma hasa,

Wale wamama wakawashangaa, mmoja akamuambia 'wewe si tumekuozesha tu mwaka Jana? Umeshaanza kutoka nyumbani bila kuandaliwa chai mapema hivyo.!?'
Akacheka, 'hamna bwana nimemuacha amelala sitakagi kumsumbua'.! Mwenzie akachangia kuwa wanatoka wote na mkewe alfajiri na mapema, huo muda wa kuandaa chai asubuhi utatoka wapi.?

Wale wamama wakawasema sema pale, si busara mwanaume mwenye mke kutoka nyumbani bila kupata chochote asubuhi bwaana, wakaongea ongea pale, wale wakaka wakaenda zao.! Kiukweli hata sikuchangia chochote, niliona kabisa hayanihusu, wale wamama wakanigeukia eti 'binti hivyo ndivyo tunavyowafunza mkaishi na waume zenu? Nikajifanya pale 'ujue mama kila familia ina taratibu zake na pia wana makubaliano yao, hivyo kila familia inafanya kile inachoona wao wapo sahihi'.!

Sikutaka kutia comment yoyote katika lile sababu sikujiona kama nipo kwenye position ya ku-judge ama niko na 'eksipiriensi' ya kutosha katika masuala hayo yawahusuyo wanandoa, japo kiukweli sijawahi ona mtu aondoke nyumbani kwa Mama Carleen hata awe mgeni wa kuwahi basi la alfajiri eti atoke bila kutia kinywani chochote kitu, na ndivyo nilivyokuzwa nikaaminishwa hiyo ndiyo busara.!

Je, kiukhalisia kwa kuzingatia mfumo mzima wa maisha yetu ya kudamka hata kabla ya jogoo kuwika hiki kitu kipo applicable? Na kama ni ndiyo, Je, kwa ambao hawafanyi hili, hivi ndiyo inamaanisha kuwa kuna mahali tunafeli sisi kama wanawake?? Japo wanaume wetu baadhi wanaonesha kuridhika na hili, hivii ni kweli wanaume wetu mmeridhika au ndiyo zile za, wacha tu tulisongeshe gurudumu la maisha..??
Hapo kuna mambo kadhaa.

Watanzania wengi tuna tabia ya kufuatilia sana mambo ya watu, hata wasiotuhusu, hata ya nyumba tusizozijua mahusiano yake yakoje. Maisha hayana formula maalum kwamba hivi ndivyo watu waishi.

Kama watu wazima wanaishi vizuri bila tabu, kwa maamuzi yao, wewe mtu baki ni nani uwapangue waishi hivi au vile?

Kama mwanamke ana maruhani hataki kuamshwa asubuhi, akiamshwa anakuwa na kisirani wiki nzima, na mume anaamua kuepusha kisirani, mtajuaje?

Unaweza kuweka formula watu wote wapande ngazi, kutumia lift ni uzembe.

Halafu ikatokea kuna mtu ana kilema hawezi kupanda ngazi, ukawa umemnyanyapaa.

Kwa hivyo, hata pale tunapoweka sheria za nani afanye nini, tujibakishie sehemu kwamba "labda kuna kitu sijaelewa hapa, nawaachia wenyewe wanaojielewa zaidi".

Mimi nimeamka asubuhi leo (nafanya kazi kutoka nyumbani kwa sababu ya kuepuka Coronavirus) breakfast naiangalia mpaka sasa saa saba muda wa lunch. Nilikuwa sijisikii kula na nikawa nina mikutano ya kazi mingi. Sasa naweza kupata brunch.

Kuna watu wengine wanakula kwa kujisikia njaa, hawali kwa kuangalia masaa.

Sasa kama mtu anatoka nyumbani asubuhi hajajisikia kula breakfast, anajisikia kula mida ya saa nne, hapo napo utamlaumu mwanamke?

Na hata kama wamekubaliana wenyewe mwanamke asiamshwe, mwanamme akapate breakfast kazini, watu wengine hilo linawahusu nini?

Je, wangeambiwa mwanamme ndiye anamtengenezea mkewe breakfast asubuhi, halafu yeye hali anakula baadaye, si ndiyo wangesema kapikiwa limbwata kabisa?

Live your life, and as long as they don't interfere with your life, let others live their lives.

Life is too short for unnecessary investigations into how other people live.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
My wife to be, jipange vizuri huko uliko. Mi napenda kula kula, so ni lazima uendane na kasi. Yani nilipe mahari alafu bado nikale kwa mama ntilie? HApana asee
Hahaha..
Mr. Kana wewe ndiyo wale kabla jogoo kuwika ushaparamia masufuria jikoni.!?
 
Hapo kuna mambo kadhaa.

Watanzania wengi tuna tabia ya kufuatilia sana mambo ya watu, hata wasiotuhusu, hata ya nyumba tusizozijua mahusiano yake yakoje. Maisha hayana formula maalum kwamba hivi ndivyo watu waishi.

Kama watu wazima wanaishi vizuri bika tabu, kwa maamuzi yao, wewe mtu baki ni nani uwapangue waishi hivi au vile?

Kama mwanamke ana maruhani hataki kuamshwa asubuhi, akiamshwa anakuwa na kisirani wiki nzima, na mume anaamua kuepusha kisirani, mtajuaje?

Unaweza kuweka formula watu wote wapande ngazi, kutumia lift ni uzembe.

Halafu ikatokea kuna mtu ana kikema hawezi kupanda ngazi, ukawa umemnyanyapaa.

Kwa hivyo, hata pale tunapoweka sheria za nani afanye nini, tujibakishie sehemu kwamba "labda kuna kitu sijaelewa hapa, nawaachia wenyewe wanaojielewa zaidi".

Mimi nimeamka asubuhi leo (nafanya kazi kutoka nyumbani kwa sababu ya kuepuka Coronavirus) breakfast naiangalia mpaka sasa saa saba muda wa lunch. Nilikuwa sijisikii kula na nikawa nina mikutano ya kazi mingi. Sasa naweza kupata brunch.

Kuna watu wengine wanakula kwa kujisikia njaa, hawali kwa kuangalia masaa.

Sasa kama mtu anatoka nyumbani asubuhi hajajisikia kula breakfast, anajisikia kula mida ya saa nne, hapo napo utamlaumu mwanamke?

Na hata kama wamekubaliana wenyewe mwanamke asiamshwe, mwanamme akapate breakfast kazini, watu wengine hilo linawahusu nini?

Je, wangeambiwa mwanamme ndiye anamtengenezea mkewe breakfast asubuhi, halafu yeye hali anakula baadaye, si ndiyo wangesema kapikiwa limbwata kabisa?

Live your life, and as long as they don't interfere with your life, let others live their lives.

Life is too short for unnecessary investigations into how other people live.

Sent from my typewriter using Tapatalk
Ahsante Kiranga, you said it well..!
Dunia ingekuwa pahala bora zaidi laiti kama kila mmoja angeishi while minding their own damned business.!
Ila ukhalisia utasimama pale siku zote kuwa kamwe haitakuwa rahisi kwa maisha yetu ya Kibongo maybe a thousands years to come.!
 
Mie katika vitu ambavyo sitagombana kabisa na mke wangu ni suala la kunipikia.
Asipopika wala sina shida huyo kwa mama ntilie wangu buku 2 nimeshiba na wala hamna kuosha vyombo.
Akipika nitaheshimu nitakula chakula chake ila sijui nianze kumuuliza kwa nini hujapika hiho kwangu haipo.

Chakula changu muhimu ni papuchi basi.
Kwakweli nisiwe mnafiki mpaka 'nifurahishwe' ndo nakuwa mtoto mzuri
Mimi bhana asubuhi nikiamka kama hajaandaa fresh tu naamsha zangu ingawa huwa anaadaa breakfast,but kama hamna mwenye mishe atakayewahi kuamka ndo anaandaa na wala siyo kesi.

Ila unamwachaje mwenzako ndani unaenda kunywa chai yeye hajanywa halafu unarudi nyumbani,ni tabia mbaya na ubinafsi

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
Kutokana na mfumo wetu wa maisha na miundombinu mibaya ya usafiri wa kufika kazini wengi hulazimika kutoshiriki kifungua kinywa (breakfast) au chakula cha jioni (dinner) pamoja kama familia.

Kama hakuna kikwazo kama hicho ni kosa kubwa sana kutoshiriki milo hiyo pamoja.
Mkiwa hamjapata watoto inaonekana sio tatizo lakini mazoea hujenga tabia, ina maana mkishapata watoto kuna uwezekano mkubwa sana mkaendeleza tabia hiyo ya kutoshiriki hiyo milo pamoja.

Hii milo ndiyo sehemu nzuri sana za kuitambua familia yako na kujenga desturi na mila, na tamaduni za familia.
Wakati huu ndio sehemu muafaka kugundua kama mmojawapo wa wanafamilia yako ana tatizo lolote lile, sura na uchangamfu wa mtu hueleza mengi sana.

Kuna yana yanayo weza kutokea ndani ya familia yako usiyajue au anayo pitia mtoto wako hapo nyumbani au shuleni ukakosa kuyajua.
Huu ndio muda wa kumfundisha mtoto tabia flani kama kutoongea wakati wa kula n.k.
Huu ndio muda wa kujua mwenza wako hapendi chakula gani au mtoto wako ana tatizo la kiafya kapoteza hamu ya kula n.k.

Family values nyingi hujengwa na kuzungumzwa wakati huu, hapa ndo hukumbushwa vitu walivyo sahau watoto kama kuchana nywele au kunyosha nguo za shule n.k.

Unfortunately mimi mwenyewe wakati mwingi nakosa muda wa hii milo (meal time) pamoja na familia na siku nikikaa nao naona na kusikia mengi sana.

Mapenzi, familia na ndoa ni zaidi ya ngono.

Namkumbuka sana mwalimu flani wa hizi shule za kimataifa Mr. Ryan raia wa kigeni, tulikuwa tunafanya kazi online kwa Team Viewer application, Yeye akiwa mkoani mimi nikiwa hapa Dar, kila siku ikifika saa 12 jioni lazima asitishe kazi anawahi kula chakula (dinner) na familia wakiwa pamoja.

Kuna muitaliano flani pale Mikocheni Reagent Estate ana sehemu yake kama Pub anauza vinjwaji na nyama za kuchoma au kuku, ikifika saa 12:30 jioni anaandaa meza moja kwenye vibanda vyake vya makuti kwa ajili ya dinner, muda huo hata uje na oda ya milioni haupati huduma mpaka amalize kula yeye na familia yake na wafanyakazi wake.

We were doing the same at home when I was a kid, I remember they used to put me on the table because I was too young to reach my food on top of the dinning table.
My dad would never allow us to converse in middle of the meal or kids never drink too much water before finishing your meal.

Unajua kwanini alitukataza mambo hayo?
Sababu kuongea wakati wa kula unarusha vyakula ovyo toka kinywani ni uchafu na hatari ya kuambukizani COVID-19, pia unaweza kukwamwa au kupaliwa na chakula kooni, au una onesha chakula cha mdomoni ni kinyaa.

Kwanini usinywe maji mengi katikati ya chakula?
Sababu utashiba maji badala ya kushiba chakula kisha utadhohofisha mwili.
Kitaalamu sio vema kunywa maji wakati wa chakula bali unatakiwa ule matunda yenye majimaji kama tikiti au mengineyo, au juice kidogo.

Hivyo ndivyo unafundisha watoto wakati wa chakula, kama vile kutopuliza chai kwa midomo n.k.
Haya tunapuuza, na wamama wengi wa sasa hawapikii watoto chakula nyumbani, wanapenda kuwapa chips ndio maana unakuta mtoto kibonge lakini kinga dhaifu.
Kila siku kwa dokta Massawe pale Morocco kulipia 50K hadi 100K.
Mama anaona uvivu kupika anamwambia baba fulani urudi na chipsi na junk food zingine.

That was too long to be here!
Mtanisamehe wadau hasa Carleen mwenye mada.

NB: Breakfast siyo lazima aandae mama hata mzee baba ukiweza na mila yenu inaruhusu unazama jikoni.
Au mama majukumu yamemzidia na hamna msaidizi unamsaidia wife.
 
Wooow'..!!
Kwahiyo ninyi wakaka wa hivii wa kutuandalia bf on bed mshawahiwa siyo.!?[emoji28]
Hizi purukushani za maisha nitakuandalia saana ngapi nikuletee...

Naamka mapema naandaa maana siwezi andaa yangu tu... kisha utaikuta panapotakiwa.
 
Hahaha..
Mr. Kana wewe ndiyo wale kabla jogoo kuwika ushaparamia masufuria jikoni.!?
mwanamke mvivu kupika atanikimbia. Japo mara moja moja nitakua naingia mwenyewe jikoni. Sijawahi kuelewa kwa hii jamii ya kiafrika mtoto wa kike anakuaje mvivu kupika?
 
Back
Top Bottom