Naomba kuelimishwa kidogo juu ya hili

Naomba kuelimishwa kidogo juu ya hili

Ni sawa Myahudi, ila hujaona wanaume wengi wamesapoti wake zao kuwa wapo sahihi kwa kutokufanya hivyo.!?

Changamoto ni Mazoea aliyoyaona binti wakati anakua, kama mama ake alikua anatengeneza chai asubuhi basi ataendelea nayo, vivyo hivyo kwa mwanaume.

kwa upande wangu whatever ni jibu sahihi, sitamlaumu.
 
Kutokana na mfumo wetu wa maisha na miundombinu mibaya ya usafiri wa kufika kazini wengi hulazimika kutoshiriki kifungua kinywa (breakfast) au chaula cha jioni (dinner) pamoja kama familia.

Kama hakuna kikwazo kama hicho ni kosa kubwa sana kutoshiriki milo hiyo pamoja.
Mkiwa hamjapata watoto inaonekana sio tatizo lakini mazoea hujenga tabia, ina maana mkishapata watoto kuna uwezekano mkubwa sana mkaendeleza tabia hiyo ya kutoshiriki hiyo milo pamoja.

Hii milo ndiyo sehemu nzuri sana za kuitambua familia yako na kujenga desturi na mila, na tamaduni za familia.
Wakati huu ndio sehemu muafaka kugundua kama mmojawapo wa wanafamilia yako ana tatizo lolote lile, sura na uchangamfu wa mtu hueleza mengi sana.

Kuna yana yoweza kutokea ndani ya familia yako usiyajue au anayo itia mtoto wako hapo nyumbani au shuleni ukakosa kuyajua.
Huu ndio muda wa kumfundisha mtoto tabia flani kama kutoongea wakati wa kula n.k.
Huu ndio muda wa kujua mwenza wako hapendi chakula gani au mtoto wako ana tatizo la kiafya kapoteza hamu ya kula n.k.

Family values nyingi hujengwa na kuzunguzwa wkati huu, hapa ndo hukumbushwa vitu walivyo sahau watoto kama kuchana nywele au kunyosha ngu za shule .

Unfortunately mimi mwenyewe wakati mwingi nakosa muda wa hii milo (meal time) pamoja na familia na siku nikikaa nao naona na kusikia mengi sana.

Mapenzi, familia na ndoa ni zaidi ya ngono.

Namkumbuka sana mwalimu flani wa hizi shule za kimataifa Mr. Ryan raia wa kigeni, tulikuwa tunafanya kazi online kwa Team Viewer application, Yeye akiwa mkoani mimi nikiwa hapa Dar, kila siku ikifika saa 12 jioni lazima asitishe kazi anawahi kula chakula (dinner) na familia wakiwa pamoja.

Kuna muitaliano flani pale Mikocheni Reagent Estate ana sehemu yake kama Pub anauza vinjwaji na nyama za kuchoma au kuku, ikifika saa 12:30 jioni anaandaa meza moja kwenye vibanda vyake vya makuti kwa ajili ya dinner, muda huo hata uje na oda ya milioni haupati huduma mpaka amalize kula yeye na familia yake na wafanyakazi wake.

We were doing the same at home when I was a kid, I remember they used to put me on the table because I was too young to reach my food on top of the dinning table.
My dad would never allow us to converse in middle of the meal or kids never drink too much water before finishing your meal.

Unajua jwanini alitukataza mambo hayo?
Sababu kuongea wakati wa kula unarusha vyakula ovyo toka kinywani ni uchafu na hatari ya kuambukizani COVID-19, pia unaweza kukwamwa au kupaliwa na chakula kooni, au una onesha chakula cha mdomoni ni kinyaa.

Kwanini usinywe maji mengi katikati ya chakula?
Sababu utashiba maji badala ya kushiba chakula kisha utadhohofisha mwili.
Kitaalamu sio vema kunywa maji wakati wa chakula bali unatakiwa ule matunda yenye majimaji kama tikiti au mengineyo, au juice kidogo.

Hivyo ndivyo unafundisha watoto wakati wa chakula, kama vile kutopuliza chai kwa midomo n.k.
Haya tunapuuza, na wamama wengi wa sasa hawapikii watoto chakula nyumbani, wanapenda kuwapa chips ndio maana unakuta mtoto kibonge lakini kinga dhaifu.
Kila siku kwa dokta Massawe pale Morocco kulipia 50K hadi 100K.
Mama anaona uvivu kupika anamwambia baba fulani urudi na chipsi na junk food zingine.

That was too long to be here!
Mtanisamehe wadau hasa Carleen mwenye mada.

NB: Breakfast siyo lazima aandae mama hata mzee baba ukiweza na mila yenu inaruhusu unazama jikoni.
Au mama majukumu yamemzidia na hamna msaidizi unamsaidia wife.
How I like the way unajua ku-present ideas zako Mr. Titicomb.! you nailed it mkuu..!!
Umeongea kweli tupu, mbio za maisha zimefanya familia nyingi mno wazazi kuwa mbali na watoto wao,
Kila kitu kimebadilika kuanzia malezi ya nyumbani, kwenye jamii mpaka shuleni.!!
Kuna namna ni lazima wazazi wakubali kuendana na hii kasi wakati huo huo wakikazana kuhakikisha watoto wao wakipata makezi bora na lishe bora.!
Umenigusa mpaka nimetoka nje ya mada sema ahsante sana ilikuwa kwa nia njema ya kujenga.!!
 
Sijui wengine lakini mimi kunywa chai alfajiri siwezi aisee.
Ila kifamilia naonaga ni vyema asubuhi na jioni familia kujumuika pamoja inakuwa vyema zaidi.
Mnapata kifungua kinywa then wa shule na makazini wanakwenda.
Jioni mnapata dinner then kila mtu anaelekea kulala.
Hii hujenga ukaribu na mshikamano zaidi katika familia

Inaweza kuwa ngumu kutokana na mazingira ya huku kwetu hasa maswala ya usafiri. Waweza jikuta unachelewa kazini na mashuleni kila siku.
 
Mimi nikiwa nyumbani huwa nakula kila kitu Cha mke SI chai Cha mchana bila kushahau Cha usiku Niko radhi niwashe gari kuwai mesosi wa mama(__),na nikiwa mkoani naya miss mnooo,ilifika pointi rafiki zangu kunishangaa nikawajibu achana na mapishi ya kidigo

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Wala huhitaji kuringa, neatness ni character, ndivyo ulivyo.

Nakumbuka niliwahi kuizungumzia hii kwa thread yako nyingine.

Unasababisha mtu asome hata kama amechoka.
Ndiyo nakumbuka uliwahi kuniambia Don C, and it has been appreciated..!!
 
Hizi purukushani za maisha nitakuandalia saana ngapi nikuletee...

Naamka mapema naandaa maana siwezi andaa yangu tu... kisha utaikuta panapotakiwa.
Hata hiyo ya kukuta tu imeandaliwa ni bonge ya baraka pia Mr. Daby..!!
 
Kama mke anapika makachakacha lazima wote mtimke Kama mandege John muwai majalalani(migahawani)

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Ahsante Kiranga, you said it well..!
Dunia ingekuwa pahala bora zaidi laiti kama kila mmoja angeishi while minding their own damned business.!
Ila ukhalisia utasimama pale siku zote kuwa kamwe haitakuwa rahisi kwa maisha yetu ya Kibongo maybe a thousands years to come.!
Usijiapize sana dadangu. Dunia inabadilika.

Mreno alisema Msumbiji na Angola haziwezi kuwa huru kwa miaka mia tano ijayo. Alisema hilo mwaka 1970.

Miaka mitano baadaye Msumbiji na Angola zikapata uhuru. Miaka mia tano ikawa miaka mitano.

Ngoja tuangalie kama Corona itatufunza adabu kwanza.

Moja ya sababu watu wa Ulaya wamekuwa na adabu iliyowaletea maendeleo ni ukweli kwamba wenzetu walipata majanga ya vifo sana kwenye plagues, hudusan The Black Death iliyoua kati ya 30% na 60% ya wakazi wa Ulaya

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
mwanamke mvivu kupika atanikimbia. Japo mara moja moja nitakua naingia mwenyewe jikoni. Sijawahi kuelewa kwa hii jamii ya kiafrika mtoto wa kike anakuaje mvivu kupika?
Being African lady si sababu ya kubadilisha mtu tabia, ni mabinti wengi sana wa kizazi cha sasa hawajui kufanya kazi za nyumbani, na case ni ile ile malezi na lifestyle!
 
Back
Top Bottom