Nani kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar baada ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad?

Kuhusu Babu Duni nadhani ni suala la muda tu atakuwa makamu wa kwanza wa rais huko Zanzibar

Juma Duni ndio natural Hair wa Maalim Seif. Japo kuwa Umri umekwenda, na pia amepoteza ushawishi kwenye chama na kwa wafuasi ukilinganisha na miaka ya nyuma. Lakini bado anabaki kuwa ndie most deserved one
 
Juma Duni ndio natural Hair wa Maalim Seif. Japo kuwa Umri umekwenda, na pia amepoteza ushawishi kwenye chama na kwa wafuasi ukilinganisha na miaka ya nyuma. Lakini bado anabaki kuwa ndie most deserved one
Hili yawezekana liko wazi lakini kuna wanasiasa wengine wakongwe wengi sawa na Duni kina Bimani na Mnyaa japo hawafiki level ya Babu Duni
 
Sawa lakini ccm watakuwa tayari kushirikiana na Mansour iwapo jina lake litapendekezwa ?

Je wapemba watakuwa tayari kumtanguliza Mansour kuipigania Zanzibar yenye haki na usawa ?

Mansour ana madhaifu mengi ya kumfanya asikidhi vigezo kuwa kiongozi mkuu wa upinzani. Kiufupi hafai, ijapokua anao ushawishi kidogo maeneo ya mjini Unguja
 
Yote kwa yote siasa za Zanzibar zitachukua mwelekeo mpya sana.

Ni mwelekeo upi ni suala la kusubiri muda utupatie majibu
kwa jinsi SUK ilivyoanza kazi ndani ya siku 100 maalim alikuwa anakwenda kumtengenezea njia ya ushindi mkubwa bwana hussein mnamo 2025.

maalim hakuwa na nguvu tena ya kuwa mgombea wa uraisi mnamo 2025 hivyo angelikosekana mwanadamu sahihi aliyetoka kwenye system ya serikali mwenye uwezo wa kumchalenge hussein kwenye jukwaa lijalo
 
Hao huwezi linganisha na duni, Kwa karibu miaka 20 Duni amekua ndio mrithi wa Maalim Mtarajiwa.
Lakini Duni umri umemtupa mkono sana na huenda ACT wakateua mtu ambaye atakuwa karata yao kwenye uchaguzi ujao wa 2025.

Na huenda 2025 asiwe karata muhimu kwa ACT visiwani humo hili wewe unalitazama vipi ?
 
  1. Mansour Yussuf Himid
  2. Juma Duni Haji
Maandalizi ya siasa zijazo baada ya Maalim
kumbuka anatakiwa atoke chama pinzani.lakini pia uteuzi huu unamuangalia yule mwenye nguvu na ushawishi kutoka vyama pinzani namaanisha chama kikuu Cha upinzani,ambacho ni ACT WAZALENDO,swali je ni Nani kutoka act WAZALENDO ambaye anaushawishi mkubwa Kama alivyokuwa seif???
 
Maalim Seif alikua analeta balance kubwa kwenye siasa za upinzani Zanzibar, kiasi kwamba sasa wasipokua makini mambo yanaweza kuvurugika
ukisoma comment za wachangiaji juu ya maalim na uamuzi wake halafu ukaamua kufanya ziara ndogo mitaani unakutana na dunia tofauti.

nilikuwepo pemba nikapata kushuhudia mkutano wa ndani aliofanya maeneo ya KONDE.
watu walijitokeza kwa wengi sana kumsikiliza kana kwamba si wao waliouliwa na majeshi.

maalimu ni taasisi iliokuwa imara sana
 
kumbuka anatakiwa atoke chama pinzani.lakini pia uteuzi huu unamuangalia yule mwenye nguvu na ushawishi kutoka vyama pinzani namaanisha chama kikuu Cha upinzani,ambacho ni ACT WAZALENDO,swali je ni Nani kutoka act WAZALENDO ambaye anaushawishi mkubwa Kama alivyokuwa seif???
  1. juma duni haji
  2. mansour yussuf himid
  3. hamad massoud
  4. kwa waliokuwa chamani pamoja na zitto akiwemo mgombea mwenza wa bernard membe
 
Sawa nimekupata vizuri lakini Mansour inaonekana bado ni mchanga katika siasa za upinzani itawezekana kweli ACT kupendekeza jina lake ?

Mazurui ndio kiongozi mwenye sifa za kuvaa viatu vya Maalim Seif kuliko wote.
Mana ndio Most influenced person ndani ya chama, Pia Kwa wafuasi wa wachama na hata kwa wafadhili wachama.

Ila ni bora abaki kuwa King Maker kuliko kujaribu kuchukua uongozi wa juu.
Yoyote atakae kuwa na support ya Mazurui ndio atakaekaa.
 
Fafanua kidogo hoja yako hii

Uongozi mkuu wa chama majority yao ni watu wa Unguja, na wao ndio wenye sauti ndani ya chama.
Wakati majority ya wafuasi wa Chama ni wapemba na wakati huohuo wafadhili wa chama kwa maana ya wafanya biashara na diasporas pamoja na wachangiaji wadogo wadogo wengi wao Zaidi ya 90% ni wapemba.
Sasa hapo ndipo unapoona balance ya Maalim, Hao wapemba wote walikua wanasimama na Maalim, sasa kuondoka kwa Maalim kunaweza kuleta hofu kidogo visiwani.
Matukio kama yaliyofanywa na Hamad Rashid na Lipumba bila ya uwepo wa maalim lazima chama kingelipasuka vipande viwili.
 
Lakini Duni umri umemtupa mkono sana na huenda ACT wakateua mtu ambaye atakuwa karata yao kwenye uchaguzi ujao wa 2025.

Na huenda 2025 asiwe karata muhimu kwa ACT visiwani humo hili wewe unalitazama vipi ?

hilo ndio tatizo. Ila wise decision ni kumuacha Duni akamalizia umakamo huu wa miaka mi 5 then 2025 chama kikajipanga upya nani wakukivusha. Na pia Duni awe ndio mwenyekiti mpya wa Chama.
 
Hakuna ubishi Maalim Seif (R.I.P) alijipambanua kama kiongozi asiyekuwa kigeugeu, mkweli, jasiri, anaetabirika, asiye muoga, na anaeipenda Zanzibar kutoka kwenye ufungu wa moyo wake. Alichokisema jana, atakisema leo na atakirudia hichohicho kesho.

Sasa hatunae Tena, je Zanzibar Yuko anaeweza kuvivaa viatu vyake?
 
Back
Top Bottom