Nani anaiongoza CCM?

Mzee ES, kama nimekuelewa vizuri ni kuwa JM bado ana influence kubwa kwenye chama, lakini haikumsaidia kwenye uchaguzi uliopita kwa vile aligeuka kinyume na ahadi aliyoitoa (ya kutokugombea nafasi hiyo). Jambo hilo ni kama lililomkuta Mzee Msekwa na mambo yote ya Uspika na ikarudi kumuuma. Sivyo?

Mangula ameripotiwa kwenye Mwananchi akitaka JK avunje mtandao uliosalia tangu uchaguzi, je huyu bwana anaweza kumfanya JK ageuze sikio kumsikiliza?
 
Whether Mangula ameongea hayo kwa vile naye ni majeruhi wa harakati za wanamtandao au ni kweli ana uchungu na chama chake left to be seen,lakini binafsi nampongeza kwa kufanya kile ambacho hata huyo Malecela anaedaiwa kuwa na influence ameshindwa kukifanya hadharani:daring to speak out his mind.

Let's go beyond ushabiki na hamasa.Moja ya mambo yaliyomjengea heshima Mwalimu baada ya kustaafu ni ile tabia ya kutowaonea aibu wale aliodhani wanataka kuipeleka nchi yetu pabaya.Malecela huyohuyo ni mmoja wa waliokumbana na hasira za Mwalimu.Let's ask ourselves,apart from vijembe vyake kwa vyama vya upinzani,ni lini Malecela amesimama hadharani kukemea yale ambayo yanaelekea kupeleka Taifa letu pabaya?Au lini amekemea hadharani maovu yanayofanyika ndani ya CCM.Jibu ni jepesi:hawezi kukemea kwa vile yeye mwenyewe ni sehemu ya mchezo huo mchafu japo pengine sio kwa kiwango cha wanamtandao.Nani asiyejua kuwa harakati zake za kutaka kupitishwa kuwa mgombea wa CCM hazikuwa tofauti na harakati za wagombea wengine?Dhamira inamsuta.

Kama miongoni mwa vigezo vya influence yake ni hizo safari za nje basi hata Mama Sitti anasafiri sana,na pengine zaidi ya Malecela.

Kuna good/positive influence na bad/negative influence.Huyu Mzee licha ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa ni mbunge (wa maisha?) wa kuchaguliwa.Majuzi tumesikiwa kikundi flani cha wabunge kikihangaika kuibana serikali kuhusu ishu ya Richmond.Inawawia vigumu kutimiza azma yao kwa vile kuna kundi jingine lenye nguvu ambalo linajitahidi kuona suala hili haliguswi japo Spika ameahidi litashughulikiwa kwenye kikao kijacho.Assuming Malecela ana influence,then influence yake ni negative kwa sababu kama ingekuwa positive angeitumia kuhakikisha suala hilo linajadiliwa kwa maslahi ya wapigakura wake na Taifa kwa ujumla.
 
Mlalahoi, kwenye hili la Richmond umegusia jambo moja ambalo tunaweza kulisahau. Kwenye hili suala Malecela yuko upande gani? Waziri Mkuu amelizuia hili kuzungumzwa Bungeni (akiwa ni mwenyekiti wa kakasi ya wabunge wa CCM), hata hivyo JM ni Makamu M'kiti wa CCM ambaye yuko Bungeni kati ya hawa wawili ni nani ana influence kubwa kwa wabunge wa CCM? Kama JM angetaka suala hili lijadiliwe Bungeni je lingejadiliwa kwa uhuru hata kama EL hataki?

Vipi kwa upande wa mikataba, mzee JM yuko upande gani? Je yeye ni mtetezi wa mikataba ya madini, ya nishati, na wa rada? Je anakerwa na mikataba hii au haoni jinsi inavyotuumbua? Iliposemwa kuwa Bunge halina uwezo wa kupitia mikataba yeye amekubali hoja hiyo na yuko tayari kuitetea?

Hivi kweli JM ana influence ya kubadilisha utendaji wa chama chake na kupata matokeo ambayo yeye anayataka.
 
Hivi ni wapi matatizo ya nchi yakatatuliwa kwa kushadidia personalities zaidi ya issues? Ningelikuwa mimi ningebadili hii topic na kuita Issues, interests and actors in Post Nyerere CCM. Kwa wanafunzi topic ya Thesis hiyo.

Tanzanianjema
 
Mlalahoi na Mzee Es,

Woote mna points points, safi sana. Mimi kwa upeo wangu mdogo kichama, JM anasikilizwa kwa kuwa ni makamu Mwenyekiti wa chama. Once akiondoka kwenye hicho cheo, he is out!, hizo ni fikra zangu, kwa sasa hawa jamaa wanafanya unafiki tu kujifanya wanampenda na kushirikisha huyu mzee wa watu, mioyo yao haiko hivyo. Mfano bomba ni jinsi walivyo mfanyia kupitia BM kwenye uchaguzi.

Siasa at its best!

FD
 
Nimefuatilia mjadala huu tangu mwanzo na ni wazi kwamba hakuna kigogo mwenye influence ndani ya CCM baada ya JKN.

Hii ni ishara tosha kwamba CCM kutokana na muundo wake inafanya kazi kama taasisi (Institution); yaani hakuna mtu mmoja au kundi dogo ndani ya chama wanaweza kukiyumbisha chama iwapo wataoondoka; si wana-mtandao wala vigogo!

Hata huyo mzee JM ambaye amesemwa hapo juu, kwa sasa anasikilizwa kupitia nafasi yake ya umakamu mwenyekiti, nje ya hapo hana lolote.

Yetu macho, mwaka huu CCM wanachaguana, tuwaona hao vigogo watatoka vipi?

Mnakumbuka miaka ile vigogo wakiitwa 'Vingunge?'
 
Kazi ya makamu wa mwenyekiti wa ccm, ni kumaliza au kupunguza nguvu za upinzani na ndio kazi ambayo anaonekana kuiweza sana kuliko nyingine zote,

Wazee wekeni facts au data za wenye influence, mbona so far imekuwa hadithi tuuuu, swali la mzee MMJ ni vigogo wa ccm now sio wa kesho au zamani, kama hakuna data wala facts basi turudi kwenye ishus zingine otherwise tutaishisa kubadili majina weeee hapa na hakuna kitu!!
 
ES,
Usichukie wala isukuume sana kama JM anajadiliwa hapa, because he is not being discussed/spoken of ,in isolation. Ni mazungumzo tuuu, Swahili style, barazani na kahawa? Chai au soda.

Very healthy for the brain, otherwise tutaitwa BONGOLALA or NOBONBO land.
 
sifikiri kama kuna hoja nyingine na data nyingine. Nataka nifunge mjadala huu rasmi (siyo kufunga thread). Sasa tuhitimishe vipi? Je bado kuna vigogo na wana influence ndani ya chama kuweza kukionya kikasikia au baada Mwalimu chama hakina tena watu wenye political clout?
 
Sasa kama kazi ni hiyo mzee Es baada ua Uchaguzi akiwa yuko nje ataifanya nani maana umesema anaiweza zaidi . Yaani CCM wanampa nafasi ya umakamu kwa hilo tu la kuua upinzani ? Je kuua Upinzani ni sifa ? Kwa nini wana hangaika na kuua upinzani badala ya kuliendeleza Taifa ?
 
MKJJ,
There is some confussion in my mind re - " Political Clout" In Tz the only person with political clout is the Predisent. In CCM post election, again its only the Chairman.One and the same person.When 10yrs have lasped of his term in office the when we see King Makers emerging within yhe party viz. CCM.That when we will see who has poitical clout in CCM.
 
naomba kuuliza: KWANINI MKAPA ILIBIDI ATUMIE UBABE KUMZUIA MALECELA ASIPIGIWE KURA NA HALMASHAURI KUU YA CCM? Je, alikuwa anaogopa kwamba Mzee Malecela angeweza kushinda?
 
Baada ya JKN hakuna mtu mmoja mwenye sauti kama aliyokuwa nayo yeye. Hata kama JK akisema anaondoka CCM leo itakuwa tu kama Mrema 1995 alipojiunga NCCR lakini mwishowe atakwisha kisiasa. Hivyo hakuna...CCM inaelekea kugawanyika
 
Mwanakijiji,

Unajua Jokakuu kauliza swali moja zito sana... Kwa nini JM alikataliwa na kamati (Mkapa) kuingiza jina lake kati ya wagombea?.. why maanake hata Salim lilikwenda kwa wajumbe wakapiga kura NOT - JM.

Je kuna uwezekano kwamba jina la JM lingefika kwa wajumbe ingekuwa shida kubwa kwa JK kuchaguliwa?.. na hata baada ya kuondolewa round ya kwanza how come he ends up kuwa makamu mwenyekiti.
 
Mkandara,
Naamini mbele ya mpiga kura wa kawaida Tanzania, siamini kama Kikwete,Salim,Kigoda,Sumaye,Mwandosya, walikuwa na uwezo wa kupambana, hoja-kwa-hoja, na huyu Mzee John Malecela.

Kuhusu "laana" ya Mwalimu kwa Malecela, hivi "laana" hiyo haimhusu kila Mtanzania anayependa/anayependekeza kuwepo kwa serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano?

Mwalimu mwenyewe alishindwa kuizuia hoja ya Tanganyika ndani ya vikao halali vya kikatiba. Mwalimu aliitwa kuzungumza na Wabunge lakini hawakumsikiliza. Badala yake akatumui "mazingaombwe" ya kura ya maoni ya wanachama wa CCM. Mpaka leo sijakutana na mwanachama wa CCM aliyepiga kura ya maoni kupinga kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.

Mwalimu alikuwa na matatizo gani na Mzee Malecela? Kwasababu baada ya Malecela kujiuzulu/kutolewa Uwaziri Mkuu, Njelu Kasaka ambaye alikuwa mtoa hoja ktk kudai serikali ya Tanganyika alipewa nafasi ya Unaibu Waziri. Hata baada ya hapo wabunge kama Sebastian Kinyondo walikuwaja kupewa Uwaziri kamili!!

Kila anayedai serikali ya Tanganyika ajue kama na yeye ana "laana" ya Baba wa Taifa.
 
hata mie natamani dola la tanganyika au watu wa mrima lirudi, kwa hiyo nnazani laana ya nyerere imenipata, ila na sisi laana yetu huko aliko itampata tu iko siku
 
sifikiri kama kuna hoja nyingine na data nyingine. Nataka nifunge mjadala huu rasmi (siyo kufunga thread). Sasa tuhitimishe vipi? Je bado kuna vigogo na wana influence ndani ya chama kuweza kukionya kikasikia au baada Mwalimu chama hakina tena watu wenye political clout?


Jibu langu ni kwamba baada ya Mwalimu hakuna mwanasiasa mwenye infuence ya kusikilizwa bali tuna kundi la wahuni waliojivika kofia ya uanasiasa (wanamtandao) ambao,just like the mafia,kutekelezwa matakwa yao sio suala la hiari kwetu.Wanafanya chochote wanachotaka na hakuna mwenye jeuri ya kuwazuia au kuwauliza.Urais na uenyekiti wa CCM unastahili kumfanya Muungwana awe na influence lakini kwa bahati mbaya hapo ndipo kwenye ardhi yenye rutuba lakini hakuna mkulima.Huyu ni mtu wa porojo na mwanamaigizo.Alishasema anawajua wala rushwa lakini akawapa INDEFINITE TIME to change,akapewa majina ya wala rushwa akauchuna,akapewa majina ya wauza unga akauchuna.
 
Jibu langu ni kwamba baada ya Mwalimu hakuna mwanasiasa mwenye infuence ya kusikilizwa bali tuna kundi la wahuni waliojivika kofia ya uanasiasa (wanamtandao) ambao,just like the mafia,kutekelezwa matakwa yao sio suala la hiari kwetu.Wanafanya chochote wanachotaka na hakuna mwenye jeuri ya kuwazuia au kuwauliza.Urais na uenyekiti wa CCM unastahili kumfanya Muungwana awe na influence lakini kwa bahati mbaya hapo ndipo kwenye ardhi yenye rutuba lakini hakuna mkulima.Huyu ni mtu wa porojo na mwanamaigizo.Alishasema anawajua wala rushwa lakini akawapa INDEFINITE TIME to change,akapewa majina ya wala rushwa akauchuna,akapewa majina ya wauza unga akauchuna.

Kwa hiyo unafikiri hili lijamaa lina mdomo mkubwa usio na jino hata moja?
 
Back
Top Bottom