Nani anaiongoza CCM?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Leo najiuliza swali jepesi nikiendelea kuandika makala mpya ambayo inakusudia kwa mara nyingine kuamsha mawazo na kuchochea hisia za ndugu zangu watanzania tunapoifikiria nchi yetu. Chama cha Mapinduzi kimekuwa na vinara wake, mashabiki wake n.k Lakini ndani ya chama hicho kuna watu ambao hujulikana kama "Wazee wa Chama", "Magwiji", "Vigogo", "Vingunge" n.k Watu hawa inasemekana 'wakikohoa' wajumbe wengine wanajikwaa, na 'wakimung'unya' vikao vinatikisika. Wanachama hawa ambao wengi ni wa lile kundi la Waasisi wana ujiko wa pekee ndani ya CCM na maneno yao yanabeba uzito mkubwa wakati mwingine kushinda wa mwenyekigoda wa chama hicho! Hata hivyo najiuliza hawa magwiji au vigogo wa CCM hasa ni kina nani? Na je kweli wana uwezo bado wa kulielekeza jahazi la chama wanakotaka wao? Wana CCM kama hawa:

John Malecela
Rashid Kawawa
Jackson Makweta
Chrisant Mzindakaya
Joseph Warioba
Salim Ahmed Salim
Salmin Amour
Kingunge Ngombare Mwiru
Cleopa David Msuya
Dr. Abdalah Kigoda
Getrude Mongella
Pius Msekwa
Joseph Mungai
Brig. Gen (mstf.) Hassan Ngwilizi
Anna Makinda
Philip Marmo

Kwa kuanzia na majina hayo machache, kuna yeyote kati yao mwenye hadhi kuonekana kweli ni "kigogo" wa CCM? Kuna majina niliyoyasahau? Je watu hao bado wanaweza kukitikisa Chama cha Mapinduzi au ujiko wao umeanza kufifia kama mbalamwezi changa? Je CCM bado ina nafasi kwa watu kama hao au ndio imeshakuwa ni chama kinachoongozwa na maslahi ya watu wachache, kikiwaweka pembeni vigogo wake na hakuna mtu mwenye ubavu wa kukinyoshea kidole?
 
John Malecela -

John Malecela - Yes
Rashid Kawawa - Yes
Jackson Makweta - Nope.
Chrisant Mzindakaya - May be.
Joseph Warioba - Not really. Too much of an outsider.
Salim Ahmed Salim - Not really.
Salmin Amour - Amesusa.
Kingunge Ngombare Mwiru - Yes
Cleopa David Msuya - Yes
Dr. Abdalah Kigoda - Nope.
Getrude Mongella - Mmh, may be.
Pius Msekwa - On procedural matters, yes
Joseph Mungai - Nope
Brig. Gen (mstf.) Hassan Ngwilizi - Absolutely not
Anna Makinda - Sometimes
Philip Marmo
- Nope.

A good idea will be to take from the members of Central Committee, then hapo utapata who is who ndani ya CCM.

Zamani kulikuwa na Mzee Masudi Mtandika (Pwani), Daudi Semkiwa (Tanga) na wengineo, it was hot kwenye NEC.
 
Nimeangalia Kamati Kuu na majina yaliyopo wengi ni wageni tu ukiondoa wachache... kutokana na "yes" na "may be" zako hapo juu inaonekana siyo zaidi ya watu 10 na si chini ya watu wanne ambao ni vigogo kweli. Unafikiri majina mengine yoyote yasiyo katika orodha yangu but the people still have some political clout kwenye chama?
 
Yeah. Ali Ameir, quintessential kigogo in Zanzibar. Mzee Natepe vilevile. Mikoani Mzee Mtopah wa Lindi na Mzee Ngeze wa Kagera nao wanasikilizwa lakini ni kwasababu ya uzee (and presumed busara). Otherwise, wengi wao wakiongea ni kuji-position kwa vyeo au kutetea vyeo.
 
Mugongo Mugongo,

Hongera.. inaonekana unadata nyingi sana kuhusu hawa vigogo wetu.

unaweza ukatuandikia historia fupi za hao vigogo mkjj aliowataja..
 
Hawa wanne wakizungumza wanaweza kuitikisa CCM?

Rashid Kawawa
John Malecela
Cleopa D. Msuya
Kingunge Ngombare Mwiru

Ni kitu gani kinaweza kuwafanya hawa wasitiliwe maanani?
 
Huyu Cleopa Msuya nadhani yupo nje maanake makosa aliyafanya miaka ileee alipomtoa marehemu Mwaikambo Bima na kumpeleka TIB jambo ambalo alivuna maadui hasa toka kwa wazee na vijana wa mjini (utawala huu uliopo madarakani).
 
Yayumkinika kusema u-kigogo umeathiriwa na ujio wa uanamtandao.I stand to be criticized,but nadhani kila mwananmtandao mwenye wadhifa ndani ya CCM ni "kigogo wa CCM".Yayumkinika pia kusema kuwa "ukongwe" ndani ya chama hicho sio suala lenye umuhimu tena.Most probably umuhimu wa "ukongwe" ulifutika baada ya kifo cha Mwalimu.Kawawa,Malecela,Makweta,etc wamebaki kuwa figures tu lakini trendsetters ni the likes of Rostam Aziz,Mwanri,Nchimbi,etc.Mantiki ni nyepesi:katika Tanzania ya leo it's not about what you know or how long you've been in the know but rather what you have (in monetary terms) or what you know about who you know.
Malecela alikumbatia watu ambao kwa tafsiri ya zamani ndio walikuwa vigogo wa CCM eg wenyeviti wa CCM wa mikoa,nk lakini akakumbana na watu wenye jeuri ya fedha (wanamtandao) ambao kwa namna flani wametuonyesha kuwa sio kweli kuwa in every long run it's experience that counts but money does.
 
...............katika Tanzania ya leo it's not about what you know or how long you've been in the know but rather what you have (in monetary terms) or what you know about who you know....
....................

Mlalahoi, hapo umenena.
Nimeona mengi katika siasa za bongo ambayo fedha imepindisha sera. Yanatokea na yanaendelea kutokea, na siyo CCM tu. Waulize Kawawa, Kisumo, Kingunge, Warioba, Mzee Ndejembe (Dodoma) na wengine lukuki.
 
Mlalaho, now you have brought in a very interesting twist to this... Sasa kati ya hawa neo-vigogo.. nani anaweza kuikemea CCM kama anaona inakwenda mrama...?
 
Yayumkinika kusema u-kigogo umeathiriwa na ujio wa uanamtandao.I stand to be criticized,but nadhani kila mwananmtandao mwenye wadhifa ndani ya CCM ni "kigogo wa CCM".Yayumkinika pia kusema kuwa "ukongwe" ndani ya chama hicho sio suala lenye umuhimu tena.Most probably umuhimu wa "ukongwe" ulifutika baada ya kifo cha Mwalimu.Kawawa,Malecela,Makweta,etc wamebaki kuwa figures tu lakini trendsetters ni the likes of Rostam Aziz,Mwanri,Nchimbi,etc.Mantiki ni nyepesi:katika Tanzania ya leo it's not about what you know or how long you've been in the know but rather what you have (in monetary terms) or what you know about who you know.
Malecela alikumbatia watu ambao kwa tafsiri ya zamani ndio walikuwa vigogo wa CCM eg wenyeviti wa CCM wa mikoa,nk lakini akakumbana na watu wenye jeuri ya fedha (wanamtandao) ambao kwa namna flani wametuonyesha kuwa sio kweli kuwa in every long run it's experience that counts but money does.

Mlalahoi

U spot it on! Mambo sasa ni u-mtandao na zaidi fedhwa!

Mwakjj

Hao neo-vigogo wote wananuka! hakuna mwenye uwezo wa kusimama na kumnyooshea kidole mwenzie kama anaenda mchomo. Mifano ndio hiyo wala huna haja ya kwenda mbali sakata la AC V ZK.

Finger crossed twendeni hivi hivi ado ado tutafika tu.

Kwenye list mbona mzee wangu RUKHSA hamkumtaja?
 
Duh tena nilimsahau tu.. je na yeye ni kigogo anayeweza kusema neno likasikika? Vipi kuhusu Mzee Mkapa naye?
 
Mimi nina mrazamo tofauti....hapo mmeangalia sana upande wa "public figures", kuna watu wana sauti kuliko hao mliowataja lakini hawapo kwenye Public...mfano RA. Huyu mtu ana sauti sana na sasa hivi akikohoa basi CCM inasikiliza. Hawa mliowataja wana julikana kwa sura kila kona...lakini kuna ambao hawajulikani hao ndio wale wanaoshikilia bajeti ya ccm na fedha za kampeni za chama. Hawa kwa namna moja au nyingine wanalindwa na pia wanaogopwa wakati huo huo.

Hao kwenye hiyo list ni kama vile Nyerere ameganywa mara nyingi; nikiwa na maana kwamba hakuna mmmoja wao aliyekuwa na "Balls" kama JKN...inahitaji kuweka nguvu zao pamoja ili kupata sauti moja ambayo JKN alikuwa nayo kwenye chama. Wakati huo Power kwenye chama ilikuwa inategemea sana kuwa na "influence"...JKN hakuwa na hela lakini alikuwa na influence ya kutosha kuliko kufanya atakalo...sasa leo hii chama kimebadilika sana na sio kuhusu influence tena bali CASH...Je hao mliowataja hapo juu wana CASH....au wenye cash hawajulikani na pengine hata sera za chama hawazijui?

Naomba kutoa hoja.
 
Yebo Yebo.. umekuja na hawa ambao tunawaita ni vigogomamboleo! Watu ambao ujiko wao kwenye CCM hautokani ni historia yao katika chama bali uwezo wao. Tatizo langu na ambalo ndilo swali langu la msingi ni je watu hao wanauwezo wa kuikemea CCM wakasikilizwa? je RA kwa uwezo wake wote wa kifedha anaweza kuwaambia CCM "jamani hapa mmepotoka" akasikilizwa?
 
Mwanasiasa mbona unaongeza maneno yako kwenye quote ya msomi Edmund Burke??...Joke-though noted!
 
Yebo Yebo.. umekuja na hawa ambao tunawaita ni vigogomamboleo! Watu ambao ujiko wao kwenye CCM hautokani ni historia yao katika chama bali uwezo wao. Tatizo langu na ambalo ndilo swali langu la msingi ni je watu hao wanauwezo wa kuikemea CCM wakasikilizwa? je RA kwa uwezo wake wote wa kifedha anaweza kuwaambia CCM "jamani hapa mmepotoka" akasikilizwa?

CCM ya leo sidhani kama ina mtu mmoja mwenye jeuri ya kuinyooshea kidole. Huyo alikuwa JKN peke yake. Hawa waliopo leo hawana nguvu, kwanza kwa kiasi kikubwa naona wanatemeana na kulindana sana...JKN hakuwa na haja ya kumtegemea mtu au kulindwa na mtu kisiasa. Kwa kifupi ccm watake wasitake..chama kimegawanyika, wachache wenye influence kidogo ndani ya chama bado wamo (hao uliwataja), lakini asilimia kubwa ni "vigogo mamboleo". Hawa ndio wanashika madaraka leo, japo kwa "remote control" lakini wana sauti ya nguvu. Baraza la JK halikuundwa kwa sababu ya sababu za kisiasa, bali zaidi kwa nani alichangia nini katika kampeni either ndani au nje ya chama. Hiyo inatoa picha kubwa kuwa era ya vigogo inakwisha/imekwisha tena haraka...sasa ni zama za vigogo mamboleo.

Hawa hawawezi kunyoosheana vidole kwa sababu wote ni wachafu. Msingi wa kuwepo hapo walipo sio influence kwa wananchi bali ni cash either waliyonayo au walioweza kukitafutia chama...enzi za kunyoosheana vidole vimepita, sasa ni enzi za kuchukua chako mapema.
 
Ukweli ni kwamba ndani ya ccm as maamuzi ya chama kama ni vigogo ni wawili tu, Muuungwana na JM, ndio wenye uamuzi wa mwisho kwenye ishu zote za ndani ya ccm,

kwa mfano Muuugwana alikuwa ameamua kuwaondoa makatibu wote wa ccm wa mikoa mpaka wilaya, na Mangula, ikiwa ni revenger ya mafaili ya maadili kule Chimwanga, JM akasafiri usiku kumuwahi kabla ya kesho yake kutangazwa toka Dodoma, akaishia kuwatema kamati ya usalama ya kina Sozigwa, na Mangula, na viognozi wote wa chini wa ccm,

Mfano mwingine Muuungwana aliamua kumpa Blaza Ditto, ukatibu wa ccm, Jm akaweka mguuu chini kuwa atajiuzulu kabla Muuungwana hajatangaza, compromise ikaishia kuwa Makamba kwa muda, mpaka Kinana atakapokuwa tayari kuichukua nafasi hiyo, ikabidi asigombee tena u-Spika wa EAC,

mjadala wowote huanza na hao wawili, wengine hupelekewa baadaye kuongezea utamu na propaganda, maamuzi mengi ya serikali huamuliwa na Muuungwana peke yake, baadaye humpasia RA ambaye kwanza humbonyeza el, na wengineo hufuatia baadaye,

Kwa mfano Muuungwana ndiye pekee aliyeamua Membe awe waziri wa nje, nguvu ya Msuya ilimalizwa na Kisumo!

As far as I know!
 
Mzee ebnny mbona mmemsahau ! mzee es wewe ni mtu wa karibu sana wa malecela ( kama unavyodai mwenyewe ) kama kweli mbona husemi sasa kwamba mzee benny alimwambia laivu mzee malecela kwamba ndani ya ccm hawamtaki ? ingawa inasemekana katika kura za kumchagua mgombea wa ccm alishinda malecela na jk alibwagwa, lakini sasa hiyo inaprove kwamba mzee benny ana sauti over malecela !!

ukikubali hilo nadhani nitamwaga mengi !!

na hadi hivi leo maamuzi anayofanya jk huwa anashauriwa na mzee benny !!

source: jamaa mmoja hivi kitengo cha PSU na usalama wa taifa
 
Back
Top Bottom