Jasusi, viongozi waliotajirika siyo wote walijinufaisha kwa madaraka yao. Baadhi ya uliowataja walikuwa na pesa yao kabla ya kuupata uongozi.Mzee ES,
Nilishawahi kusema kuwa BM is Iskariot. Tanzania hakuna kiongozi aliyetajirika kihalali. Akina EL, akina Karamagi, na sasa akina Diallo wote wametajirika kwa kuhujumu nchi. Na ndiyo maana watu wanakimbilia ubunge wa CCM (Masha) hata kama mtazamo wao haujawahi kuwa wa Ki-CCM ili nao wapate nafasi ya kujitanua.
Joka Kuu, swali langu haswa kwenye hii mada ni kujaribu kufikiri kama hao watu wanne uliowataja wakisimama hadharani na kusema "CCM hapa imekosea" na "kuikemea hadharani" kama alivyofanya Mwalimu wanaweza kusikilizwa na wananchi? Je wakifanya hivyo wanaweza kubadilisha mwelekeo mzima wa CCM?