Nani anaiongoza CCM?

Huu muda ndo mzuri CHADEMA kujipanga kwa haya mapungufu ya CCM tunayoyaona. Wangekuwa na Mgombea mzuri wa URAIS pasingetosha lakini naona bado hawataki kufanya mabadiliko. Kwa CCM sasa hivi wanachemsha JK kimyaa!! Zitto upo!!
 
Leo najiuliza swali jepesi nikiendelea kuandika makala mpya ambayo inakusudia kwa mara nyingine kuamsha mawazo na kuchochea hisia za ndugu zangu watanzania tunapoifikiria nchi yetu. Chama cha Mapinduzi kimekuwa na vinara wake, mashabiki wake n.k Lakini ndani ya chama hicho kuna watu ambao hujulikana kama "Wazee wa Chama", "Magwiji", "Vigogo", "Vingunge" n.k Watu hawa inasemekana 'wakikohoa' wajumbe wengine wanajikwaa, na 'wakimung'unya' vikao vinatikisika. Wanachama hawa ambao wengi ni wa lile kundi la Waasisi wana ujiko wa pekee ndani ya CCM na maneno yao yanabeba uzito mkubwa wakati mwingine kushinda wa mwenyekigoda wa chama hicho! Hata hivyo najiuliza hawa magwiji au vigogo wa CCM hasa ni kina nani? Na je kweli wana uwezo bado wa kulielekeza jahazi la chama wanakotaka wao? Wana CCM kama hawa:

John Malecela
Rashid Kawawa
Jackson Makweta
Chrisant Mzindakaya
Joseph Warioba
Salim Ahmed Salim
Salmin Amour
Kingunge Ngombare Mwiru
Cleopa David Msuya
Dr. Abdalah Kigoda
Getrude Mongella
Pius Msekwa
Joseph Mungai
Brig. Gen (mstf.) Hassan Ngwilizi
Anna Makinda
Philip Marmo

Kwa kuanzia na majina hayo machache, kuna yeyote kati yao mwenye hadhi kuonekana kweli ni "kigogo" wa CCM? Kuna majina niliyoyasahau? Je watu hao bado wanaweza kukitikisa Chama cha Mapinduzi au ujiko wao umeanza kufifia kama mbalamwezi changa? Je CCM bado ina nafasi kwa watu kama hao au ndio imeshakuwa ni chama kinachoongozwa na maslahi ya watu wachache, kikiwaweka pembeni vigogo wake na hakuna mtu mwenye ubavu wa kukinyoshea kidole?


Mkjj, kwa sasa hivi kwa maoni yangu CCM kama ilivyo nchi yetu haina Kiongozi ndiyo maana unaona watu wa juu katika chama hicho akina Sitta, Malecela, Makamba, Kingunge wanajibizana katika vyombo vya habari kwa kutoa kauli ambazo zinapingana hasa kuhusiana na ufisadi.

Kama ilivyo nchi yetu ambayo sasa hivi inayumba kwa kutokuwa na kiongozi hali kadhalika CCM nayo inayumba tena sana tu na ndiyo maana ninaombea sana nchi yetu mwaka 2010 ipate kiongozi mpya ambaye ataweza kupambana na kuyumba kwa nchi yetu na hatimaye kuiweka sawa maana Kikwete kashindwa na hili la kushindwa Kikwete siyo siri.

Na kama Kikwete akirudishwa tena madarakani kwa nguvu za mafisadi basi nchi yetu itakuwa inaelekea mahali pabaya sana kuliko hata hiki kipindi cha 2005 mpaka 2010 ambapo tumeona nchi ikiyumba katika kiasi ambacho hatujawahi kukiona tangu tupate uhuru.
 
Last edited:
Ule usemi tuliouzoea

Chama kimeshika Hatamu.........Serikali inafuata.
Chama kimeshika Hatamu za nani..............Serikali?
Chama kimeshika Hatamu.........Kinatoa maelekezo serikalini

Mafisadi wameshika Hatamu......Chama kinafuata
Mafisadi wameshika Hatamu za nani..............Chama?
Mafisadi wameshika Hatamu................Wanatoa maelekezo kwa Chama

Serikali imeshika Hatamu.........Wananchi wanafuta
Serikali imeshika Hatamu za nani........Wananchi?
Serikali imeshika Hatamu............Inatoa maelekezo kwa wananchi

Connecting the dots ..... Mafisadi, Chama, Serikali, .Wananchi......., So sielewi hawa Wananchi itakuwaje maana mkono wa Mafisadi ni lazima uwaguse. Au ni makengeza yangu?
 
Huu muda ndo mzuri CHADEMA kujipanga kwa haya mapungufu ya CCM tunayoyaona. Wangekuwa na Mgombea mzuri wa URAIS pasingetosha lakini naona bado hawataki kufanya mabadiliko. Kwa CCM sasa hivi wanachemsha JK kimyaa!! Zitto upo!!

Changamoto kubwa kwa CHADEMA kwasasa ni uchaguzi wa ndani, wangefanya mapema, wangepata muda mzuri wa kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu. Tatizo chaguzi za ndani huwa haziishi bila kuacha majeruhi.
 
Unajua kila kitu kina enzi na zama zake, kuna wakati kinakuwa kizuri na wakati mwingine kibaya (hadi kuwa sumu). Kila siku ina historia yake na mabo yake. Kusema ndo vigogo au vingunge inategemea ni enzi gani, na pia wanaokubali huo u-vigogo wao.
Jambo kubwa ni kufanya mabadiliko ya zama hizi kwa wakati huu na mahitaji ya jamii ya sasa na sio kuangalia ilikuwaje, umaarufu wa ujamaa, nk. Tujipange tupate wachapakazi, sio watu wa kujigamba kuwa wao ni vigoo, vingunge, nk.
 
Tatizo sio nani anaongoza CCM, tatizo liko kwenye watu na utendaji wenyewe. Kila kitu kina zama na enzi zake, na kila siku ina historia yake. Kitu kinaweza kikawa kizuri leo n akesho kikawa kibaya (hadi kuwa sumu). Hivyo kusema nani kingunge, kigogo, nk, inategemea ni kwa wakati gani tunaongelea. Inawezekana alikuwa enzi hizo ila sasa sio.
Sasa hivi tunahitaji watu wachapa kazi wanaopata uchungu na jamii ya sasa iliyojaa umasikini ukiongozwa na ufisadi. Htutaki vingunge na vigogo. Ni jukumu letu kuibadili hii taswira ya vigogo (ma-tycoon na moguls) kujiita vigogo na kuendelea kututawala kwa zidumu fikra sahihi za ....
 
Malumbano yote yanayoendelea ndani ya CCM, Kikwete Kimyaaaa!

Date::8/13/2009
Makamba awaonya wanaolumbana ufisadi CCM
Na Habel Chidawali,Dodoma
Mwananchi


KATIBU mkuu wa CCM, Yusufu Makamba ameonya wanachama wanaozungumzia nje ya utaratibu mambo ya chama hicho akisema kufanya hivyo ni ukiukaji wa maadili.

Makamba ametoa kauli hiyo wakati mjadala mkali juu ya ufisadi baina ya wanachama ukiendelea huku katibu huyo akijiandaa kwa kikao cha leo cha Kamati ya Maadili ambayo kazi zake ni pamoja na kujadili maadili ndani ya chama na kupanga ajenda za vikao vingine vya juu vya CCM.


Mbunge wa Ukonga, Mahanga Mahanga amekuwa akiandikwa na vyombo vya habari kwa takriban wiki moja sasa baada ya kutoa tamko kuwa wale wanaopiga kelele dhidi ya ufisadi hawana budi kuwataja wanaowatuhumu, kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria au kuwashtaki kwenye chama akisema kufanya hivyo nje ya CCM ni kukichafua chama kwa kuwa wanaotuhumiwa hawazidi wanne.


Mahanga alienda mbali zaidi kwa kusema watu hao wanatoa tuhuma kwa sababu ya chuki na wivu na kwamba hawana budi kujiondoa kwenye chama, kauli iliyopokelewa kwa hisia kali na wanachama wengine wa CCM waliodiriki kumwelezea mbunge huyo wa Ukonga kuwa ni mchanga wa kisiasa.


Lakini jana Makamba alionekana kuegemea upande wa Mahanga aliposema kuwa jambo hilo linatakiwa kukemewa na kwamba vitendo hivyo havipaswi kuigwa na kiongozi au mwananchama yeyote ndani ya chama.

Katibu huyo alisema hayo jana mjini hapa, lakini hakutaka kuhusisha na malumbano yanayoendelea hivi sasa baina ya wanachama hao wa CCM.


Mjadala huo ulianzishwa na mbunge wa Mtera, John Malecela aliyesema kuwa wabunge wengi wa CCM wako hatarini kupoteza viti vyao kwenye uchaguzi ujao kutokana na tuhuma za ufisadi na baadhi kutoenda kwenye majimbo yao na kwamba CCM itakuwa kwenye wakati mgumu.

Malecela, ambaye mke wake Anne Kilango ni mmoja wa vinara ya vita ya ufisadi, alisema wapo viongozi wa chama hicho ambao wanapinga kwa nguvu zote mambo ya ufisadi, lakini wanapingwa na watu ambao kwa namna moja wako kimya au ambao wana urafiki wa karibu na watuhumiwa.

Kauli ya waziri huyo mkuu wa zamani ilipokewa kwa hisia tofauti baina ya wanachama wa CCM, baadhi wakiunga mkono na wengine, akiwemo Mahanga wakipinga kwa madai kuwa wanaofanya hivyo wanaichafua CCM.


Mahanga alisema wapiga kelele hao wanafanya kazi ya upinzani ndani ya CCM hivyo akawataka kuondoka ndani ya chama na kuwaacha watu wenye maadili na mapenzi mema ndani ya chama.

Jana Makamba alionekana kuwa mjanja na kukataa kujibu swali kuhusu ajenda za kikao cha leo cha Kamati ya Maadili, lakini akasema kuwa mambo yote yatawekwa hadharani baada ya kumalizika kwa kikao hicho leo.


"Aksante kwa swali lako kijana, lakini ujue kuwa watu wanaozungumza nje ya vikao vya chama wanakiuka maadili ya chama chetu. Nikiongea na mimi leo hii nitafanana na watu hao," alisema. "Subiri kikao ni kesho (leo) itajulikana kama tutazungumza kuhusu watu hao ambao wanazungumza mambo ya chama nje ya vikao au kama hatutazungumza hilo. Mara tutakapomaliza kikao, katibu wa Itikadi na Uenezi, Bwana Chiligati atazungumza na waandishi."
 
“Aksante kwa swali lako kijana, lakini ujue kuwa watu wanaozungumza nje ya vikao vya chama wanakiuka maadili ya chama chetu. Nikiongea na mimi leo hii nitafanana na watu hao,” alisema. “Subiri kikao ni kesho (leo) itajulikana kama tutazungumza kuhusu watu hao ambao wanazungumza mambo ya chama nje ya vikao au kama hatutazungumza hilo. Mara tutakapomaliza kikao, katibu wa Itikadi na Uenezi, Bwana Chiligati atazungumza na waandishi.”

CCM ina maadili kwenye lipi hasa!? :confused: Makamba acha kuudanganya umma wa Watanzania kwa kudai CCM ina maadili. CCM ya sasa imejaa ufisadi na mafisadi na hakuna maadili yoyote ndani ya CCM. Kama chama chenu kingekuwa na maadili basi mafisadi wote ndani ya CCM wangekuwa wameshafukuzwa siku nyingi, lakini bado mmewakumbatia tu hata kuwaonyesha vidole mnaogopa.
 
Katika enzi tulizonazo wenye pesa ndio wenye nchi kwaa hiyo mi naona mafisadi ndio wanaoweza kuzungumza na kusikilizwa hapa nchini na wala si hao mnaowataja,hawa ni kama Rostam Aziz,Edward Lowasa,Jitu Patel,Somaiya and the likes........
 
Yayumkinika kusema u-kigogo umeathiriwa na ujio wa uanamtandao.I stand to be criticized,but nadhani kila mwananmtandao mwenye wadhifa ndani ya CCM ni "kigogo wa CCM".Yayumkinika pia kusema kuwa "ukongwe" ndani ya chama hicho sio suala lenye umuhimu tena.Most probably umuhimu wa "ukongwe" ulifutika baada ya kifo cha Mwalimu.Kawawa,Malecela,Makweta,etc wamebaki kuwa figures tu lakini trendsetters ni the likes of Rostam Aziz,Mwanri,Nchimbi,etc.Mantiki ni nyepesi:katika Tanzania ya leo it's not about what you know or how long you've been in the know but rather what you have (in monetary terms) or what you know about who you know.
Malecela alikumbatia watu ambao kwa tafsiri ya zamani ndio walikuwa vigogo wa CCM eg wenyeviti wa CCM wa mikoa,nk lakini akakumbana na watu wenye jeuri ya fedha (wanamtandao) ambao kwa namna flani wametuonyesha kuwa sio kweli kuwa in every long run it's experience that counts but money does.
U got it right!!!

mtandandao kwa sasa ndo mama na baba ya CCM...hamna cha ukongwe, ukigogoo wa ukingungee zaidi ya masilahi ya fedha kupitia mtandao ambao RA ameuratibuu kufikia hapo ulipooo..

wale wanaopinga ufisadi walio na nyadhifa ndani ya ccm kama ubunge nk hawajitambui au wameshakosaa mvutoo wa kimtandaooo na wanakamilisha ile kauli ya mfa maji haachii....................

Uhai wa CCM unatokana na ufisadi kwa sasa iweje mwanachama upinge na uendelee kuukumbatiaaa???
 
Hakuna anayeongoza kipo kipo tu kama chombo baharini, kesho huyu kashika paddles leo, kesho huyu, kinaenda KiMunguMungu, mwenye wazo zuri lenye kulinda maslahi yao anapendwa. Usikute kazi za kila siku zinafanywa na nyumba zao ndogo!

Kipo kipo tu
 
Yebo Yebo.. umekuja na hawa ambao tunawaita ni vigogomamboleo! Watu ambao ujiko wao kwenye CCM hautokani ni historia yao katika chama bali uwezo wao. Tatizo langu na ambalo ndilo swali langu la msingi ni je watu hao wanauwezo wa kuikemea CCM wakasikilizwa? je RA kwa uwezo wake wote wa kifedha anaweza kuwaambia CCM "jamani hapa mmepotoka" akasikilizwa?

MM heshima yako mkuu, swali lako ni je watu wa sampuli ya RA wenye uwezo wa fedha lakini hawana historia ya chama kama wanaweza kukemea mambo kichama na kusikilizwa? Maoni yangu ni kamba kukemea ni lazima utoe kauli kwenye vikao na yale unayopendekeza yakasikilizwa na kukubalika lakini pia unaweza usitoe kauli yeyote lakini kwa vile una uwezo wa fedha ukainfluence yale mambo usiyokubaliana nayo yasifanyike!! Hapo ndipo wakina Mohamed Enterprise, Rostam na wengine wengi wenye fedha wanapokiyumbisha chama.Consequently, the most powerful people who can influence policy decisions in CCM now through their cronies ni Rostam Aziz na Manji [These two are collabolators katika ufisadi wao , ndio maana Manji alinunua kesi ya KAGODA/EPA toka kwa Rostam}
 
Back
Top Bottom