passion_amo1
JF-Expert Member
- Dec 3, 2023
- 1,690
- 3,408
Wakuu Heshima mbele.
Juzi nilikuwa natokea PWANI nikakumbuka kwamba sikuwahi kuchukua cheti changu cha kidato cha sita. Sasa nilikuwa na mama watoto, nikamwambia sababu muda umeenda kesho unisindikize shule nikachukue cheti changu, akasema tutakwenda. Basi tulilala mjini pale na asubuhi yake mida ya saa nne nkawa naelekea shule.
Nilipofika shule nikakutana na mwalimu aliyekuwa akifundisha Jiongrafia alikuwa rafiki yangu sana.
Akaniambia Kama sura inakuja hivi inapotea, nikamwambia Mimi Passion mwalimu tulimaliza na watu fulani(nikiwa namkumbusha viongozi wa mwaka wangu)
Akasema ohoooo! sasa nimekupata
Mwalimu; na huyu dada mzuri hapa pembeni ni nani?
Mimi; Sir huyu ni Mke wangu.
Mwalimu; Hongera sana mwanangu.
Mimi; Ahsante sir.
Mke wangu; shkamoo mwalimu.
Mwalimu; marahaba, Hongereni sana japo passion alikuwa mchafu mchafu Kwa kweli umembadilisha(wote tukacheka ila mm nilicheka usoni nikaona huyu anaanza mazoea ya ovyo)
Nikamuuliza kuhusu mwalimu wa Taaluma akaniambia alihama na sasahivi ni mwalimu mkuu shule fulani, Basi nikaachana nae kuelekea ofisi ya Taaluma.
Nikafika ofisi ya Taaluma nikawasalimia walimu waliokuwepo.
Basi nikamkuta mwalimu wa Taaluma msaidizi.
Mimi; sir nina shida ya ofisi kidogo, nilimaliza mwaka fulani hapa lakini sikuwahi chukua cheti changu.
Msaidizi; sawa, unaitwa nani?
Mimi; Passion xxx xxx
Msaidizi; umekuja na leaving certificates au result slip?
Mimi; Hapana ninazo kwa mfumo wa soft.
Msaidizi; sawa nionyeshe.
Mimi; (nikatoa simu na kumuonyesha)
Msaidizi; Kwa protokali za ofisi unapaswa kuandika barua, haya njoo huku unifate.
Tukaongozana mpaka ofisi ya mkuu wa shule, nikakutana na sekretari wa mkuu wa shule, bas mwalimu akamuelekeza nikampa jina na mwaka akaingia ndani.
Sektetari; Passion xxx xxx
Mimi; yes Madam
Sekretari; Kwanini huku- clear hii clearance form yote?
Mimi; madam sikufanikiwa kukamilisha sababu nilikuwa naumwa na nilifanya mtihani nikiwa naumwa, hivyo sikufanikiwa ku- clear.
Sekretari; kutokana na clearance yako Mr Passion and your beautiful wife unadaiwa kiasi cha shilingi 245000.
Mimi; (nilamuangalia Mke wangu nikacheka na yeye akacheka) madam hilo deni limekujaje? Ninaweza kukutana na Bursar?
Sekretari; sure Mr passion.
Akachukua simu ya mezani akampgia mhasibu.
Sekretari; Passion nenda ofsini kwake, by the way you have a beautiful wife lakini hilo haliondoi uhalisia kwamba lazima ulipe deni.
Mimi; Thanks madam. I’ll be back in a minute to take my cerficate.
Nikatoka kuelekea kwa mhasibu, baada ya kufika nikaingia ofisini.
Mimi; Sir shikamoo?
Mhasibu; Marahaba karibu bwana.
Mimi; ahsante, naitwa Passion xxx xxx nimekuja hapa kuja kuchukua cheti changu nilimaliza mwaka xxxx hapa. Lakini nimekuta deni ambalo binafsi silielewi
Mhasibu; ndugu Passion ile clearance ndio inakuonyesha kwamba wewe unadaiwa kiasi gani, hapo sina cha kukusaidia unapswa kulipa. Halafu nyinyi vijana hamna shukrani, tumekutunzia cheti, tumekufundisha, umeenda kusoma huko na mpaka umeoa lakini shilingi laki 2 tu unaanza kulalamika?!
Mimi; Sir Tatizo si kulalamika, japo sina muda sana, nitalipa hilo deni niondoke na cheti changu.
Mhasibu akaniangalia usoni kuhakikisha nachoongea.
Mhasibu; okay utaipeleka pale kwa sekretari Halafu vitu vingine viendele
Mimi; kupeleka nini Sir?
Mhasibu; utapeleka hiyo pesa kwa mhasibu na utapatiwa cheti chako.
Mimi; kwani mhasibu ananidai nini? Sir ninaomba Akaunti namba ya shule nilipe hiyo pesa hapa.
Akaniambia nsubiri hapa, akanyanyuka kutoka ofisini na mimi nikatoka kumfata. Nikawaona wanateta na sekretari kwa sauti ya chini.
Mhasibu; sasa kwa sasa hatuwezi kupokea kwa mfumo wa kibenki kutumia akaunti namba ya shule, sababu ya wanafunzi waliomaliza kipindi cha zaidi ya miaka MItano
Nikafikiri yale maneno yake nikaona hata mtoto asingeyakubali.
Mimi; Sir mimi sitalipa pesa kwa kumpa mtu hela mkononi. Ninadaiwa na shule na si mtu, hivyo nitalipa pesa yote hapa kwa akaunti namba ya shule.
Bursar akaniita pembeni sababu nilikuwa na Mke wangu karibu.
Mhasibu; sasa Mr passion sikia wewe fanya ulipe deni, Kwanini usilipe in cash sababu sasahiv hata ada imeondolewa hivyo unapswa kulipia.
Kiukweli siwasemi walimu ila binafsi naona wanapitia wakati mgumu, maana saa nne wanakunywa chai wanaletewa na mihogo ya kuchemsha.
Mimi; Sir mimi nitalipa hiyo pesa kwa akaunti namba ya shule(nikamuita Mke wangu anipe simu yangu ili nilipie lakini uhalisia hiyo pesa nilikuwa siwezi kulipa ila niligundua wanahitaji pesa)
Mhasibu; Sawa Basi ngoja nijaribu kuongea na sekretari tuone tunafanya vipi.
Baada ya kama dakika 10 walitoka pale wakiwa na cheti changu.
Mhasibu; Passion hichi hapa cheti chako.
Mimi; mwalimu Ahsanteni sana( nikaingia mfukoni nikakunja elf10 nne nikampatia mkononi)
Mhasibu; Ahsante sana mwanangu.
Nilichogundua ukienda shule walimu wakikuona umevaa umependeza, umenenepa, umeenda na gari magari yenyewe si yetu ya baba mkwe wanaona una pesa kumbe bado tunapambana.
Nani alikutana na kisanga kipindi anaenda kuchukua cheti.l chake shule?