Ulifanya kosa gani shule hadi kengele ikagongwa wanafunzi wakusanyike kwa ajili yako?

kataza

Member
Sep 5, 2014
20
50
Hello ladies and gentlemen,

Katika maisha ya shule kuna visa na mikasa mingi sana tupe kisa chako.

Changu mimi ni;

Kuna siku tulichelewa kurudi shule kulikuwa na ile ratiba ya unatoka shule saa sita then unarudi saa saba kasoro. Sasa mimi nilipoenda home bi mkubwa ndio kwanza anabandika mboga dah, nikaanza msaidia kupika nikachelewa.

Sasa nafika shule nakuta shule nzima ipo kimyaaaaaaa, nikaona sio kesi ngoja niambae na korongo then nitokee class kwa nyuma.

Sasa nimeambaa na korongo ile natokeza tu ghafla teacher on duty huyu hapa, dah akaniita we fulani nimekuona njoo hapa then nifuate ofisi ya nidhamu. Dah, ticha mnoko kinoma, sasa tumefika ofisini nikajua nikiingia tu ni stiki tu so nikaacha atangulie then nikafunga mlango kwa nje nikasepa class.

Sasa kumbe nyuma ticha kaita sana msaada lakini wapi, maana ofisi ilikuwa imejitenga kidogo but anakuja kufunguliwa mlango muda ushaenda kama saa tisa hivi. Ghafla kengele ikagongwa na mimi nikasepa zangu home muda huohuo. Dah, assembly natangazwa popote nilipo nijisalimishe na wanafunzi wanoko wakatumwa waje home.

Maisha haya, kesho yake nikaenda na namba nikawahi nikaulizwa kwanini ulimfungia mwalimu, nikasema sio mimi maana jana sikuja shule, dah sir ...... Mungu anakuona huko ulipo.

Tililika yako.

Sent from my SM-A145F using JamiiForums mobile app
 
Mimi? Dah sio poa,

Rector, alinikuta napiga ubundi ( night study nje ya ratiba za shule) mida ya saa 8 usiku mle ndani Library na mwanangu wakuitwa Kelvin. Seminarini hapo Mzee Baba....aseee...tukapelekwa ofisini kwake...tukaambiwa tujiandae kuondoka Asubuhi kurudi home....

Kesho yake adhabu ikapunguzwa, kwakua tulikua vipanga class..wakaona kufukuza vichwa potential haitakua poa.

Tukapewa adhabu ya kuchimba vichuguu na kujaza molamu pale mbele ya smart area...

Mwanangu Kelv alikua mtoto wa kishua...akaanza kulia lia...wakamtimua....Mimi nikakomaa kinomanoma....

Kelv akaenda zake shule ya private huko TANGA....alikua mbele yangu class Moja....na sisi wote wawili tulikua ma in charge wa libray hiyo.

Tulikamatwa kipindi Mimi kama siku nne zijazo nipige pepa la form two kuingia 3...

Kwà hasira ...nikapiga misonge yote babaake...nikawa nambari 3 kikanda na nambari mmoja kimkoa. Nakumbuka huyo huyo Rector akanisifia mbele ya wanafunzi wenzangu..na kunipa Dollar 10 ya kimarekani ( ndo ilikua first time kuishika hela aina ya dollar USD )

Baadae tukiwa form 3 ...nikasikia mwanangu Kelv kafanya wonders ....one ya point 7 ( kitu ambacho hata kama angebaki hapo seminary asingeipata )

Note: Currently, mwanangu Kelv ni Daktari Bingwa katika Moja ya Hospital kubwa hapa Nchini...

Mimi ni misheni town tu....mambo ya kudang dang huku na kule ....dadeki wallah bongo salala...cha moto nakiona! Maisha yamenipiga kidole wallah hata siamini!!! Haki Mama ANAUPIGA MWINGI!!!!
 
hatari kweli kweli. Mimi paredi iliitishwa kwa ajili mapenzi. Niliandika barua ya mapenzi kwenda kwa demu. Demu akaipeleka kwa Mwalimu Mkuu kunishtaki. Kwa jinsi barua ilivyosukwa Mwl Mkuu hakuamini kama ile barua niliiandika mimi mwenyewe. Akaitisha kengele na paredi ya wanafunzi wote na walimu kuwasaka wataalamu wa barua za mapenzi. Nilitandikwa viboko hadi Mwl Mkuu alichoka mwenye kwa jinsi niliweka msimamo wa kufa peke yangu bila kusailitiana.

KIUKWELI ILI BARUA TULIISUKA KWA KUSAIDIANA TUKIWA WANNE.
Kwa siku tatu mfululizo sikeweka kukaa wala kuoga maana makalio yalikuwa na vidonda.
 
Haujamalizia vizuri paragraph ya mwisho au tukuache kwanza uugulie maumivu ya fimbo?.
Hello ladies and gentlemen
Katika maisha ya shule kuna visa na mikasa mingi sana tupe kisa chako.Changu mimi ni

Kuna siku tulichelewa kurudi shule kulikuwa na ile ratiba ya unatoka shule saa sita then unarudi saa saba kasoro....sasa mimi nilipoenda home bi mkubwa ndio kwanza anabandika mboga dah.....nikaanzq msaidia kupika nikachelewq.....sasa nafika shule nakuta shule nzima ipo kimyaaaaaaa....nikaona sio kesi ngoja niambae na korongo then nitokee class kwa nyuma
Sasa nimeambaa na korongo ile natokeza tu ghafra teacher on duty huyu hapa....dah akaniita we fulani nimekuona njoo hapa then nifuate ofisi ya nidhamu dah ticha mnoko kinoma sasa tumefika ofisini nikajua nikiingia tu niu stiki tu so nikaacha atangulie then nikafunga mlango kwa nje nikasepa class .....
Sasa kumbe nyuma ticha kaita sana msaada lakini wapi maana ofisi ilikuwa imejitenga kidogo bt anakuja kufunguliwa mlango muda ushaenda kama saa tisa hivi ... ghafra kengele Ikagongwa na mimi nikasepa zangu home muda huohuo dah assembly natangazwa popote nilipo nijisalimishe na wanafunzi wanoko wakatumwa waje home.....
Dah maisha haya kesho yake nikaenda na namba nikawahi nikailizwa y ulimfungia mwalimu nikasema sio mimi maana jana sikuja shule.....dah sir ......mungu anakuona huko ulipo...
Tililika yako....

Sent from my SM-A145F using JamiiForums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nilikua mfanyabiashara

nilikua nanua vitu dukani siku duka linafunguliwa, afu siku duka limefungwa naviuza mara mbili ya bei yake... nilikua nanua magendo kwa wanaoruka ukuta afu nauza mara mbili yake, mfano chapati moja nanunua 1000, nauza 2000...
afu pia nilikua nakopesha kwa riba ya 100%

kuna dogo mmoja alinisemea kwa mwalimu wa nidhamu kesi ndo ikaanza hapo.....
 
Back
Top Bottom