Namuogopa dingi, mkali kama pilipili

Namuogopa dingi, mkali kama pilipili

Sielewi unachomsifia baba yako, unampa sifa za ubishi? Kama mnakwenda kumshauri mambo ya maendeleo na familia kwa ujumla halafu anakuwa stubborn inamsaidia vipi au Ana stahiki sifa kivipi? Wazazi wengi wa Zamani ni wakoloni tu hata baba yangu ni hivyo hivyo! Hawataki ushauri na sio wasikivu kwa watoto wao regardless hata Kama umeshakuwa mtu/watu wazima, wanatengeneza ukuta Kati ya watoto na baba siku zote mtaonekana hakuna mtachoweza kumshauri. Mbaya zaidi Kama ikitokea mnafanya maendeleo zaidi ya kipindi chake huwa wanaona Kama mnataka kumshusha, ubishi na kelele ni njia ya kujihami tu, baba yangu mpaka Leo sehemu anayokaa huwezi kukaa atakuambia ni malezi walivyolelewa! Wakati mwingine unataka kukaa uzungumze na baba yako Kama rafiki lakini haiwezekani! It's very boring relationship, kila kitu wanajua wao.

pole sana mkuu, umeongea kwa hisia kali kama zangu, namsifia kwa hiki kipaji cha kuogopwa maana naona si kawaida mtu mzima kuendelea kumuogopa hivi.
 
Nmecheka sana,.... Lkn umenikumbusha mzee mmoja hivi alikuwa mkali sana mpaka ndugu zake wanamuogopa. Wazee wengi wenye miaka 75's ni madikteta sana hasa ukute enzi za ujana wake alikuwa na cheo fulani/alikuwa nazo, aisee huwa ni wakali hawashauriki/hawaingiliki. Misimamo yao huwa inawasaidia wanaogopwa sana, hata kitu chake hakiguswi na mtu. Lkn pia umesema mzee wako ana kila kitu na hilo ni tatizo, angekuwa hana mkwanja angekuwa mpole sana, kwani ninyi mngekuwa ndio kula yake. Dawa ya mzee kama huyo ni kumuacha tu.. Yani najaribu kuvuta picha na kumlinganisha na mzee ninaemfahamu mimi kwa ukali wake, nacheka sana!.

mkuu hata mimi kuna wakati huwa najifungia nacheka jinsi tunavyomuogopa, ukweli mimi nishaamua kumwacha tu, nimejikalia kwa mbali najifanyia mambo yangu.
 
pole sana mkuu, umeongea kwa hisia kali kama zangu, namsifia kwa hiki kipaji cha kuogopwa maana naona si kawaida mtu mzima kuendelea kumuogopa hivi.

Mimi kumuogopa simuogopi mkuu, ila nimeamua kufanya yangu vinginevyo utapasuka kichwa bure, ila sielewi Kwanini ameweka ukuta Kati ya watoto na yeye ila nisingependa kuwa baba wa style hiyo abadani.
 
Mie ningeshauri kwamba angalieni background yake,na pia stages zake zaukuaji kwa kupitia watu wazima wenzake.
Kama kuna changes ilifanyika ghafla basi akapimwe Akili.
Ulaya wazee kama hawa lazima wapimwe kwanza kabla ya kupewa ushauri wa aina yoyote.Ili wapate chanzo na kujua sababu ya kuwa hivyo.
Mnaweza mkawa mnaongea na mtu kumbe sie.

Maana hakuna bianaadam wa namna hiyo,na anawezaje kufanya biashara na watu kwa namna hiyo,maana sie wengine ni watu wa biashara na kwanza tunaangalia mtu unaefanyanae biashara yupoje,sasa kama ni mkali namnahiyo nani ata deal nae.Na wakati anachofanya wapo wenzio wanafanya kama wewe au zaidi.

Kuna tatizo hapo,ipo namna

mkuu hapo sina jibu, ila ndo hali tunayokumbana nayo, mnaweza mkapanga mipango ila mkimkaribia au mkifika kwake mambo yote yanasambaratika.
 
Mimi kumuogopa simuogopi mkuu, ila nimeamua kufanya yangu vinginevyo utapasuka kichwa bure, ila sielewi Kwanini ameweka ukuta Kati ya watoto na yeye ila nisingependa kuwa baba wa style hiyo abadani.

nimekupata mkuu sokwe , binafsi mwenyewe nishamzoea, najitahidi sana kutokuingia anga zake, nacheza nje ya 18.
 
Last edited by a moderator:
nimekupata mkuu sokwe , binafsi mwenyewe nishamzoea, najitahidi sana kutokuingia anga zake, nacheza nje ya 18.

That's the right thing to do mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Daah nimeishia kucheka tu....

Ina maana huyo mzee hashauriki kabsa??
Maana mke wake umesema hamuwezi
Marafiki hawamuwezi
Je ndugu zenu????
Huyo mzee balaa

naweza kusema kama ni reli mkuu basi tayari tupo kigoma.
 
Kaka kwanza ni furaha kua na mzee kama huyo kwa ukal wake na ubabe wake ndio maana mmefanikiwa bila yy kua hivyo. Sasa jinsi ya kuuingia muende na hoja za maana kwelikweli ukizingatia wazee siku hizi hawatuamin kabisa japo hayo mazingira tunayatengeneza ss wenyewe.

mkuu soma vizuri hoja yangu, hatoi nafasi ya kusikiliza hadi mwisho, mbaya zaidi ushauri wenyewe ni ule wa kwenda tofauti na yeye, mkisema kwenda naye anavyotaka mshaharibu, mbaya zaidi ukijichanganya kwa neno anatoa tafsiri mbaya, utajuta, utatafuta mlango wa kutokea usiuone.
 
ukweli malezi ya aina hayo mimi siyapendelei.ni vizuri mlee mtoto sometimes awe kama rafiki yako.akikosea kumrekebisha sio vibaya.matokeo yake mtoto akitaka ushauri anaogopa kukuuliza,ukali ukali utafikiri mpo jeshini.kwa upande wangu yalikuwa hayo hayo,matokeo yake nipo close na mama.nyumba nyengeni baba akikaa sitting room,watoto taratibu wanaondoka,ila wababa wengine wakizeeka wanabadilika.

pole sana dada yangu kisukari.
 
Last edited by a moderator:
Baba yako haambiliki halafu unampongeza?

You deserve each other.
 
Nami mzee wangu alikuwa tuko mbali naye sana yaani hamuwez kukaa sehem mkaongea, nilikuwa namuendea nikiwa na shida tu, labda ada au maelezo yoyote ya shule.
Ila ukaribu wangu na yeye ulianza soon baada ya mimi kumaliza form 6 na kuanza chuo, ndipo akawa sio bandidu tena kwangu hata akikuta mahali napata moja moto moja baridi ananiagizia "muongeze akimaliza" au akikuta nimekaa tu home nimedoro ananitoa kama buku 10 anakuambia hebu kapige story na wenzio huko, hapo anajua nimefulia. Mi mwenyewe nilishangaa huyu ndo yule mzee kweli. Nashukuru kuanzia kipindi hicho cha kumaliza form 6 mwaka 2007 hadi leo tuko nae peace balaa.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Za siku wanajanvi, leo nakuja na kisa cha Dingi yangu, ni mkali sana, enzi tunakua ukimuona kwa mbali tu unatafuta pa kutokea, unafurahia zaidi kutokuonana naye kwa kuwa ukionana naye tu lazima utakuwa na hatia ya kujibu, hivyo dawa ni kukwepana hadi akutafute yeye. Kwa sasa mimi ni mtu mzima, nina maisha yangu lakini bado namuogopa sana, siyo mimi tu bali hata ndugu zangu, tumekuwa tukipanga mambo mengi ya kuongea naye na yote yanaishia hewani na mkifanikiwa kwenda kumuona mkifika tu getini kwake mnaanza kupungua na hatimaye mnasmbaratika hata kabla ya kuonana naye. Siku moja tukachukuana na ndugu zangu ili tukampatie ushauri, wengi wetu tukiwa na miaka zaidi ya 30 na wengine wamegonga 40, tukafanikiwa kuingia getini, akatukaribisha viti, tukasema tunahitaji kuongea naye, ile kuanza tu kuongea mmoja wetu, yakawa ni mawazo tofauti na yeye, hakutaka amalize akamkatisha na kuanza kushusha maneno mazito, mimi nikasema naenda kukojoa nikaunganisha huko huko, ndugu zangu nasikia walitoka pale hawaioni vizuri njia, wanatembea utadhani njia imejaa makorongo. Kifupi kila tukipanga kwenda kumshauri mambo mbalimbali yakiwemo ya namna bora ya kuendesha shughuri zake, tumekuwa tukiishia tu kupanga. Mwisho nimpongeze Dingi yangu kwa kuwa na uwezo wa namna hii, kwa kweli hiki ni kipaji na ni power kubwa, wachache wana uwezo huu hasa ukizingatia watoto wake wengi tumesoma na kufuzu katika fani mbalimbali, wapo maengeneer, madokta, wanasheria, wahasibu na hata wachumi na wanasiasa, lakini kafanikiwa kutumentain na kutusambaratisha katika kila mkakati wa kumwingia, tumebaki waangaliaji tu. Je wazee wa aina hii unawaingiaje, maana kinachoniuma kuna mambo mengi hayafanyi kisomi na hivyo sisi watoto kuonekana kama wapuuzi na jamii maana mnaonekana kama hammsaidii baba yenu?.

msubirini afulie tu atakuwa mdogo
 
Alafu wazee kama hawa akikusema/kukukaripia utaona bora angekupiga... Ila bado nacheka huyu mzee anavyosambaratisha hoja zenu..
 
Sasa umekuja hapa kumsifia baba yako au unaomba ushauri? Manaake kama tabia hiyo imewasaidia kusoma sana, basi ni nzuri lakini kama kumwogopa ni tatizo, basi labda ndiyo tukusaidie ushauri hapo.
 
Kazi kweli kweli,
Jitahidini muwe mnaongea naye tu;
Vinginevyo naye anajenga ugonjwa wa moyo
kwani kila siku kifua kinajaa bure mtamkosa hata kabla
ya umri wake timilifu.
 
aiseeee mtoa mada hivi wewe na mimi tuna shea ukoo nini maana mshua wangu ndo tabia zake ma ananilizaga mara nyingi hakuna mtu mwenye sauti kwake ili hali sisi watoto wake ndo tumesoma inaumiza,, yaani hatuna sauti mbele yake zaidi ya kujibu NDIO yaani hilo limenifanya niwe makini na mume nitakae mpata(mchakato huo nauendesha kwa umakini) MAANA NAWAZA HIVI MAMA ALIWEZAJE??????? KUISHI MA HUYU MZEE MUDA WOTE HUU
 
Back
Top Bottom