Namuogopa dingi, mkali kama pilipili

Namuogopa dingi, mkali kama pilipili

hawa dawa zao huwa ni nyepesi sana, anza kumuingia kwanza kwa zawadi mbali mbali, jaribu kumpendeza kwa vitu anavyovipenda sana, mtoe out for fun mara kwa mara, hapo ukiwa tu na lengo la kutafuta ukaribu nae..

mfanyie surprise nyingi tu kadiri uwezavyo, ipo siku na ukali wake wote, atazimika tu na kusikiliza ushauri wako kwake,,..

kumbuka simba na ukali wake wooote, when it comes to sex, makucha yake yoote yanatulizwa!!.. use your mom sometimes for this exercise.. ila muwe waangalifu msije mkasababisha talaka kwa mama yenu..

Mkuu hayo yote tumefanya na tukaambulia kuambiwa yeye si wa vizawadi vidogo, very conservative.
 
Jaribu hii, siku yake ya kuzaliwa mfanyieni surprise. Kwa kumtumia mama hakikisheni anaondoka nyumbani kwake, then nyie mnaenda mnamuandalia a small party, akija home anawakuta mmemuandalia cake na zawadi ata kama ndogondogo tu, plus wajukuu (kama mna watoto) aisee nakuhakikishia ukali wake wote utaisha. Sie mzee wetu alikuwa wa design hiyo tulijitaidi kumfanya rafiki na kutomwongopa hadi sasa kama poa saaana, yaani tunamtania kama babu yetu vile

asante kwa ushauri mkuu, ila nikuambie tu, hautekelezeki.
 
Mleta mada Kuna uwezekano ukawa ndugu yangu maana hzo tabia ni za mzee wangu kwa 100% mzee wangu ni mbishi kupindukia kila kitu anajua ni dikteta balaa hta mnapomfuata kumshauri especially khs mambo yke yake ya biashara anakuwa mkali balaa hlf biashara zake zinafeli kila cku ndugu zake washampa mitaj mpk wamechoka coz mzee ni extravaganza Kuna mkutano mmoja kaka yngu alimwambia 'lakini Baba ivo unavyofanya unakosea, du ilikuwa bonge la msala ilibidi tuamulie ugomvi point yke ilikuwa eti kwanini unaniambia mi nakosea

hahahaha, mkuu komeka inawezekana kabisa japo nadhani wamefanana tu.
 
Last edited by a moderator:
mtoa mada acha sanaa bana,umeeleza vizuri sn na kuishia kujitapa kuwa mzee kazaa ma engineer,wanasheria na wasomi kibao STAKI kuamini kwa umri wenu(30.....+) eti kabisa mmekosa busara ya kumuweka sawa na unakiri wazi kuwa kila mkimwendea mmejipanga vp anawashinda kwa hoja basi hamna hoja na hamjiandai.Angekua hawaruhusu kuongea nae hapo sawa unles mnambie huwa mnamfata akiwa bwax kalewa

mkuu hujanielewa, tatizo ni kuwa hatoi nafasi kabisa ya kuwasikiliza, atasikiliza maneno machache tu kisha mambo yanabadilika, hampati nafasi ya kueleza hoja yenu ikaisha.
 
wewe jua tu huwa tunaparaganyika kama ilivyokuwa ujenzi wa mnara wa baberi.

Hahahahaha...umenifurahisha sana kwakweli...
Ila kwenye familia, lazima kutakuwa na kaka ambaye ameowa mke ambaye anafagiliwa sana na mzee...mtumieni huyo!!
NB: Akiwa anapeleka hoja asiseme kuwa ametumwa na nyie i.e Iwe ni sehemu tu ya maongezi.
 
Kama una watoto wasumbufu under 10 yrs wapeleke kwa babu yao msimu wa likizo wakamchangamshe kwa fujo. Atabadilika tu.
 
ndiyo kwa kuwa nilikuonea huruma usije ukanifia kwa kukosa pumzi

poleni sana ndugu, huyo baba yako anafanana na baba yangu, yaani ilikuwa ukisikia sauti ya viatu vyake tu unajibanza somewhere apite usikutane nae..baba yangu alikuwa mkali sna..yaani ni over..na pia alikuwa na mkono wa kupiga..ukikosea siku hiyo utatafuta pa kwenda mana home haparudiki..

ila mimi nilipomaliza form six, siku moja alitaka kunipiga, lkn nikakimbilia chumbani, akanigombeza kwa kosa ambalo hata sikufanya..roho iliniuma sna, nikaanza kulia kwa hasira na siku hiyo niliongea yote huku nalia..nilimsema baba yangu na wala sijaogopa nikasema akija tu chumbani kwetu kunipiga navua nguo anikute uchi mtt wa kike nione km atanipiga..
niliongea sana nikalalmika vile anavyotufanyia, watu wengine wamenyamaza kimya wananisikiliza na walijua siku hiyo ningemalizwa lkn wala haikua hivyo..mzee mwenyewe alinyamaza kimya wakati naongea hajajibu wala hajasema chochote na wala hajaja chumbani kwetu nilikokuwa naongelea..

kuanzia hiyo siku mzee wetu alibadilika sana, alikuwa baba na rafiki yangu mimi na ndugu zangu..ikawa ndio mwisho wa mikwara ya mzee..sasa sijui ndio kilimuingia, sijui..ila alibadilika na kuwa mpole sana..nafikiri hakuwahi kuwaza kama mimi naweza kusema maneno yale dhidi yake..halafu live anasikia..
ndugu zangu baadae walinisifu mana mzee alikuwa ni untouchable kabisa..lkn baada ya pale akawa baba badala ya dicteta..Mungu amlaze mahala pema babangu
 
safi sana aisee hongera kwa kuokoa jahazi
 
kamusi naweza kusema wewe ni jasiri, ulijitoa mhanga, hiyo ya kuvua ama kweli yalikufika shingoni haswaaaa, pole but u made it.
 
hapo kwenye red ulikuwa unatishia nyau tu...
 
aNGEENDA SHULE ANGEKUWA KAMA MUGABE AU CASTRO, ANA NYOTA YA UDIKTETANANGETUFAA SANA WATZ
 
kamusi naweza kusema wewe ni jasiri, ulijitoa mhanga, hiyo ya kuvua ama kweli yalikufika shingoni haswaaaa, pole but u made it.

yani we acha tu, wkt mwingine uchizi unasaidia eti..nakumbuka wakt niko bording form 5-6 kuna rafiki yng aliniambia baba yake alikuwa na tabia ya kumpiga mm yao mara kwa mara sasa yeye siku moja alivua nguo zote akabaki uchi wkt dingi anampiga mm yake, dingi alivyoona hivyo akamuacha na akuanzia siku hiyo hajampiga tena mama yao..kabla ilikuwa ht watoto walie mayowe gani dingi haachi kumpiga mama yao hasa akishalewa ila hiyo ya kuvua nguo ilisaidia, akaacha..ndio na mimi nikachukua hiyo theory nikasema akiingia tu chumbani kunipiga navua nguo zote, bahati yake hakuingia
 
Back
Top Bottom