Namuogopa dingi, mkali kama pilipili

Namuogopa dingi, mkali kama pilipili

Za siku wanajamvi,

leo nakuja na kisa cha Dingi yangu, ni mkali sana, enzi tunakua ukimuona kwa mbali tu unatafuta pa kutokea, unafurahia zaidi kutokuonana naye kwa kuwa ukionana naye tu lazima utakuwa na hatia ya kujibu, hivyo dawa ni kukwepana hadi akutafute yeye. Kwa sasa mimi ni mtu mzima, nina maisha yangu lakini bado namuogopa sana, siyo mimi tu bali hata ndugu zangu, tumekuwa tukipanga mambo mengi ya kuongea naye na yote yanaishia hewani na mkifanikiwa kwenda kumuona mkifika tu getini kwake mnaanza kupungua na hatimaye mnasmbaratika hata kabla ya kuonana naye.

Siku moja tukachukuana na ndugu zangu ili tukampatie ushauri, wengi wetu tukiwa na miaka zaidi ya 30 na wengine wamegonga 40, tukafanikiwa kuingia getini, akatukaribisha viti, tukasema tunahitaji kuongea naye, ile kuanza tu kuongea mmoja wetu, yakawa ni mawazo tofauti na yeye, hakutaka amalize akamkatisha na kuanza kushusha maneno mazito, mimi nikasema naenda kukojoa nikaunganisha huko huko, ndugu zangu nasikia walitoka pale hawaioni vizuri njia, wanatembea utadhani njia imejaa makorongo. Kifupi kila tukipanga kwenda kumshauri mambo mbalimbali yakiwemo ya namna bora ya kuendesha shughuri zake, tumekuwa tukiishia tu kupanga.

Mwisho nimpongeze Dingi yangu kwa kuwa na uwezo wa namna hii, kwa kweli hiki ni kipaji na ni power kubwa, wachache wana uwezo huu hasa ukizingatia watoto wake wengi tumesoma na kufuzu katika fani mbalimbali, wapo maengeneer, madokta, wanasheria, wahasibu na hata wachumi na wanasiasa, lakini kafanikiwa kutumentain na kutusambaratisha katika kila mkakati wa kumwingia, tumebaki waangaliaji tu.

Je wazee wa aina hii unawaingiaje, maana kinachoniuma kuna mambo mengi hayafanyi kisomi na hivyo sisi watoto kuonekana kama wapuuzi na jamii maana mnaonekana kama hammsaidii baba yenu?.

mtoa mada acha sanaa bana,umeeleza vizuri sn na kuishia kujitapa kuwa mzee kazaa ma engineer,wanasheria na wasomi kibao STAKI kuamini kwa umri wenu(30.....+) eti kabisa mmekosa busara ya kumuweka sawa na unakiri wazi kuwa kila mkimwendea mmejipanga vp anawashinda kwa hoja basi hamna hoja na hamjiandai.Angekua hawaruhusu kuongea nae hapo sawa unles mnambie huwa mnamfata akiwa bwax kalewa
 
Mleta mada Kuna uwezekano ukawa ndugu yangu maana hzo tabia ni za mzee wangu kwa 100% mzee wangu ni mbishi kupindukia kila kitu anajua ni dikteta balaa hta mnapomfuata kumshauri especially khs mambo yke yake ya biashara anakuwa mkali balaa hlf biashara zake zinafeli kila cku ndugu zake washampa mitaj mpk wamechoka coz mzee ni extravaganza Kuna mkutano mmoja kaka yngu alimwambia 'lakini Baba ivo unavyofanya unakosea, du ilikuwa bonge la msala ilibidi tuamulie ugomvi point yke ilikuwa eti kwanini unaniambia mi nakosea
 
Mkuu are u serious? Huyo mfanyieni suprise, kama ni house mjengeeni mkimaliza mpeni funguo, gari zuri (double cabin pick up) mnunulieni muone kama ataleta ukali. Sio mnaenda na kg ya sukari na maneno mengi mnachanganya na kizungu hawezi kuwaelewa

dah ushauri wako umenikuna ingawa sio mimi niliyeomba ushauri
 
Mleta mada Kuna uwezekano ukawa ndugu yangu maana hzo tabia ni za mzee wangu kwa 100% mzee wangu ni mbishi kupindukia kila kitu anajua ni dikteta balaa hta mnapomfuata kumshauri especially khs mambo yke yake ya biashara anakuwa mkali balaa hlf biashara zake zinafeli kila cku ndugu zake washampa mitaj mpk wamechoka coz mzee ni extravaganza Kuna mkutano mmoja kaka yngu alimwambia 'lakini Baba ivo unavyofanya unakosea, du ilikuwa bonge la msala ilibidi tuamulie ugomvi point yke ilikuwa eti kwanini unaniambia mi nakosea
 
serious mkuu, tatizo ni kuwa hakuna kitu mtapatia kikamsuprize, ana kila kitu.

Jaribu hii, siku yake ya kuzaliwa mfanyieni surprise. Kwa kumtumia mama hakikisheni anaondoka nyumbani kwake, then nyie mnaenda mnamuandalia a small party, akija home anawakuta mmemuandalia cake na zawadi ata kama ndogondogo tu, plus wajukuu (kama mna watoto) aisee nakuhakikishia ukali wake wote utaisha. Sie mzee wetu alikuwa wa design hiyo tulijitaidi kumfanya rafiki na kutomwongopa hadi sasa kama poa saaana, yaani tunamtania kama babu yetu vile
 
Unaweza ukakuta ambavyo hana ni vile asivyokuwa na hobby navyo! LAkini hata hivyo nadhani mzee yuko safi kwani inaonyesha ni well off na mwelewa ndiyo maana hata watoto wake wote kawasomesha na kuwafikisha pazuri! Hata hivyo wamfuatilie wajue anapendelea vitu gani hasa ili wavitumie kuweza kumwingia! Vinginevyo mzee yupo safi tu na mengine ni matatizo madogo madogo tu yakutofautiana kimtizamo na wanawe ambacho ni kitu cha kawaida!
cc. JEKI
"Ana kila kitu?"
Mpelekee iPad air banaa hata hiyo anayo?
 
Mleta mada Kuna uwezekano ukawa ndugu yangu maana hzo tabia ni za mzee wangu kwa 100% mzee wangu ni mbishi kupindukia kila kitu anajua ni dikteta balaa hta mnapomfuata kumshauri especially khs mambo yke yake ya biashara anakuwa mkali balaa hlf biashara zake zinafeli kila cku ndugu zake washampa mitaj mpk wamechoka coz mzee ni extravaganza Kuna mkutano mmoja kaka yngu alimwambia 'lakini Baba ivo unavyofanya unakosea, du ilikuwa bonge la msala ilibidi tuamulie ugomvi point yke ilikuwa eti kwanini unaniambia mi nakosea

Hahahaha huyo mzee ni nouma kwa kweli. Ila ipo njia ya kumtuliza tu. Mtafutieni dhawadi ya kitu anachokipenda na tena chenye thamani alafu hapo hapo onganisheni na ushauri wenu. Atawasikiliza tu.
 
We huwajui wazazi wa aina hiyo, yani hiyo zawadi yenu mtairudisha mlikoitoa na atakimbilia kuwaambia mnaringa kwa sababu mna uwezo na mnamdharau. Hapo wamuache tu.
 
Za siku wanajamvi,

leo nakuja na kisa cha Dingi yangu, ni mkali sana, enzi tunakua ukimuona kwa mbali tu unatafuta pa kutokea, unafurahia zaidi kutokuonana naye kwa kuwa ukionana naye tu lazima utakuwa na hatia ya kujibu, hivyo dawa ni kukwepana hadi akutafute yeye. Kwa sasa mimi ni mtu mzima, nina maisha yangu lakini bado namuogopa sana, siyo mimi tu bali hata ndugu zangu, tumekuwa tukipanga mambo mengi ya kuongea naye na yote yanaishia hewani na mkifanikiwa kwenda kumuona mkifika tu getini kwake mnaanza kupungua na hatimaye mnasmbaratika hata kabla ya kuonana naye.

Siku moja tukachukuana na ndugu zangu ili tukampatie ushauri, wengi wetu tukiwa na miaka zaidi ya 30 na wengine wamegonga 40, tukafanikiwa kuingia getini, akatukaribisha viti, tukasema tunahitaji kuongea naye, ile kuanza tu kuongea mmoja wetu, yakawa ni mawazo tofauti na yeye, hakutaka amalize akamkatisha na kuanza kushusha maneno mazito, mimi nikasema naenda kukojoa nikaunganisha huko huko, ndugu zangu nasikia walitoka pale hawaioni vizuri njia, wanatembea utadhani njia imejaa makorongo. Kifupi kila tukipanga kwenda kumshauri mambo mbalimbali yakiwemo ya namna bora ya kuendesha shughuri zake, tumekuwa tukiishia tu kupanga.

Mwisho nimpongeze Dingi yangu kwa kuwa na uwezo wa namna hii, kwa kweli hiki ni kipaji na ni power kubwa, wachache wana uwezo huu hasa ukizingatia watoto wake wengi tumesoma na kufuzu katika fani mbalimbali, wapo maengeneer, madokta, wanasheria, wahasibu na hata wachumi na wanasiasa, lakini kafanikiwa kutumentain na kutusambaratisha katika kila mkakati wa kumwingia, tumebaki waangaliaji tu.

Je wazee wa aina hii unawaingiaje, maana kinachoniuma kuna mambo mengi hayafanyi kisomi na hivyo sisi watoto kuonekana kama wapuuzi na jamii maana mnaonekana kama hammsaidii baba yenu?.

mi mzee wangu alikuwa hivyo hvyo. yaan mpaka 35 years ulikuwa humsogelei hata kuongea nae. ila mi namshukuru Mungu nilichofanya nilianza kwa kumletea zawad nzur nzur. nguo, viatu, saa, cku moja nikamtumia barua nikamwelezea hisia zangu. kuwa nampenda sana, nataman wakat mwingine anipe muda wa kuongea nae ili anipe uzoefu wake wakat akiwa kijana ni mambo gan aliyafanya na akafanikiwa na yap alifeli ili na mimi nicfeli. nikmwambia nataman Mungu ampe miaka mia mbili ili azid kuwa kiongoz wetu bora. huwez kuamin yule mzee alikuwa mosh alipanda gar akaja mpaka dar akakaa kwangu cku 5 akanipa wosia wake mzito na niseme tu ckuwa namfaham kama nilivyomfaham cku zile tano baba yangu. neno la mwisho aliniambia haya. ucje ukawekea kitu chochote tumain lizidilo huku dunian coz cku ukilikosa au ufe au uwe kichaa hata mkeo au wanao. ucje sema namsomesha mwanangu ili nikizeeka anisaidie. wewe timiza wajibu wako wa kihistoria tu. then akaniambia ukiwa mwanaume ukifikisha miaka 65 anza kupangilia nyumba yako na kutoa wosia coz binadam tumepewa miaka ya kuish 70 ikizidi 80. miez 7 baadae yule mzee alifariki bila kuumwa. mpaka leo namkumbuka sana.
 
hawa dawa zao huwa ni nyepesi sana, anza kumuingia kwanza kwa zawadi mbali mbali, jaribu kumpendeza kwa vitu anavyovipenda sana, mtoe out for fun mara kwa mara, hapo ukiwa tu na lengo la kutafuta ukaribu nae..

mfanyie surprise nyingi tu kadiri uwezavyo, ipo siku na ukali wake wote, atazimika tu na kusikiliza ushauri wako kwake,,..

kumbuka simba na ukali wake wooote, when it comes to sex, makucha yake yoote yanatulizwa!!.. use your mom sometimes for this exercise.. ila muwe waangalifu msije mkasababisha talaka kwa mama yenu..
 
If u obey ALL THE RULES u miss ALL THE FUN...
 
mi mzee wangu alikuwa hivyo hvyo. yaan mpaka 35 years ulikuwa humsogelei hata kuongea nae. ila mi namshukuru Mungu nilichofanya nilianza kwa kumletea zawad nzur nzur. nguo, viatu, saa, cku moja nikamtumia barua nikamwelezea hisia zangu. kuwa nampenda sana, nataman wakat mwingine anipe muda wa kuongea nae ili anipe uzoefu wake wakat akiwa kijana ni mambo gan aliyafanya na akafanikiwa na yap alifeli ili na mimi nicfeli. nikmwambia nataman Mungu ampe miaka mia mbili ili azid kuwa kiongoz wetu bora. huwez kuamin yule mzee alikuwa mosh alipanda gar akaja mpaka dar akakaa kwangu cku 5 akanipa wosia wake mzito na niseme tu ckuwa namfaham kama nilivyomfaham cku zile tano baba yangu. neno la mwisho aliniambia haya. ucje ukawekea kitu chochote tumain lizidilo huku dunian coz cku ukilikosa au ufe au uwe kichaa hata mkeo au wanao. ucje sema namsomesha mwanangu ili nikizeeka anisaidie. wewe timiza wajibu wako wa kihistoria tu. then akaniambia ukiwa mwanaume ukifikisha miaka 65 anza kupangilia nyumba yako na kutoa wosia coz binadam tumepewa miaka ya kuish 70 ikizidi 80. miez 7 baadae yule mzee alifariki bila kuumwa. mpaka leo namkumbuka sana.

aisee, hongera sana mkuu, mimi nimetumia njia zote hizo, nimeandika barua lakini hazijibiwi, nimetuma hela na kununua vinguo, siku ukimuudhi anasema unadhani kangu ulonipa au tule tuhela ni kitu kwangu, mimi siyo wa vitu vidogo hivyo, kwa namna hiyo nimeamua tu kuwa mpole kwa kuwa sina uwezo wa kumjengea ghorofa.
 
Back
Top Bottom