Namuogopa dingi, mkali kama pilipili

Namuogopa dingi, mkali kama pilipili

hapo kwenye red ulikuwa unatishia nyau tu...

unafikiri nilikuwa natishia, kweli ningevua, bahati tu naye hakuja,...dingi yangu alikuwa mkali sana kiasi kwamba akianza kukupiga wiki nzima huwezi tembea..sasa kuliko nipigwe mdada mzima nimemaliza form six, ningevua nguo zote unafikiri angesubutu tena kunipiga!!!!!! ila hiyo nilikuwa sijasema nilikuwa nawaza moyoni tu kwamba akiingia kunipiga navua nguo...bahati hakuingia
 
Mkuu are u serious? Huyo mfanyieni suprise, kama ni house mjengeeni mkimaliza mpeni funguo, gari zuri (double cabin pick up) mnunulieni muone kama ataleta ukali. Sio mnaenda na kg ya sukari na maneno mengi mnachanganya na kizungu hawezi kuwaelewa

kuna watu wana pressure mkuu, suprise sio kitu poa kabisa
 
unafikiri nilikuwa natishia, kweli ningevua, bahati tu naye hakuja,...dingi yangu alikuwa mkali sana kiasi kwamba akianza kukupiga wiki nzima huwezi tembea..sasa kuliko nipigwe mdada mzima nimemaliza form six, ningevua nguo zote unafikiri angesubutu tena kunipiga!!!!!! ila hiyo nilikuwa sijasema nilikuwa nawaza moyoni tu kwamba akiingia kunipiga navua nguo...bahati hakuingia

namkumbuka Headmaster wetu katika shule moja miaka hiyo alikuwa anazama hadi bwenini kwa kinadada bila aibu, sasa sijui kama yeye aliweza baba yako angeshindwaje.
 
Mzee tulimpa majina ya vituko akawa mama anamwambia watoto wanakuita hivi. Halafu akimaliza tu kugomba mdogo wangu akawa anamuigiza tunacheka, kuna siku alirudi akatukuta tunamuiga halafu tunacheka basi akaacha kutuita mbwa. Baadaye kuna siku alinitukana sana bila kosa halafu nikawa nimelia basi akaanza kunimind kwamba yeye ananishauri tu halafu mi nalia, nikamwambia, "Hivi ulitegemea nifurahi au niseme asante wakati umenitukana?" Akasema ntakuua, nkamwambie niiue sasa hapo mama ndo akaja kuokoa jahazi. Jioni yake akaanza kujieleza ohh wanangu ohh wanangu, huu ndo ukawa mwisho wa matusi. Siku hizi huwa namuuliza hivi ulivyokuwa unatupiga vile ulikuwa unajisikiaje, huwa hata anakosa jibu. Mdogo wangu yeye kuna siku alimchefua akaondoka nyumbani, sasa hapo akabaki na msala wa mama. Alikoma kumtukana na yeye. Hata leo akijichanganya sie tunamwambia live anatutishia tu baadaye maisha yanaendelea.
 
yani we acha tu, wkt mwingine uchizi unasaidia eti..nakumbuka wakt niko bording form 5-6 kuna rafiki yng aliniambia baba yake alikuwa na tabia ya kumpiga mm yao mara kwa mara sasa yeye siku moja alivua nguo zote akabaki uchi wkt dingi anampiga mm yake, dingi alivyoona hivyo akamuacha na akuanzia siku hiyo hajampiga tena mama yao..kabla ilikuwa ht watoto walie mayowe gani dingi haachi kumpiga mama yao hasa akishalewa ila hiyo ya kuvua nguo ilisaidia, akaacha..ndio na mimi nikachukua hiyo theory nikasema akiingia tu chumbani kunipiga navua nguo zote, bahati yake hakuingia

pole sana, hadi kufikia hatua hiyo nadhani kilikuwa kiwango cha juu cha kuchukia na kukata tamaa, wazazi tuache ukali uliopindukia, tuishi na watoto wetu kama friends, hope now una watoto, walee uzuri.
 
Mzee tulimpa majina ya vituko akawa mama anamwambia watoto wanakuita hivi. Halafu akimaliza tu kugomba mdogo wangu akawa anamuigiza tunacheka, kuna siku alirudi akatukuta tunamuiga halafu tunacheka basi akaacha kutuita mbwa. Baadaye kuna siku alinitukana sana bila kosa halafu nikawa nimelia basi akaanza kunimind kwamba yeye ananishauri tu halafu mi nalia, nikamwambia, "Hivi ulitegemea nifurahi au niseme asante wakati umenitukana?" Akasema ntakuua, nkamwambie niiue sasa hapo mama ndo akaja kuokoa jahazi. Jioni yake akaanza kujieleza ohh wanangu ohh wanangu, huu ndo ukawa mwisho wa matusi. Siku hizi huwa namuuliza hivi ulivyokuwa unatupiga vile ulikuwa unajisikiaje, huwa hata anakosa jibu. Mdogo wangu yeye kuna siku alimchefua akaondoka nyumbani, sasa hapo akabaki na msala wa mama. Alikoma kumtukana na yeye. Hata leo akijichanganya sie tunamwambia live anatutishia tu baadaye maisha yanaendelea.

pole sana mkuu, ila tukumbuke tu msitu wa wazazi tunatakiwa tuupite pole pole, maana kuna laana, si unakumbuka katika amri 10 za Mungu, ipo ile ya waheshimu baba na mama yako..... Twende nao ila tuwe makini kudumbukia kwenye mtego wa ile amri.
 
Za siku wanajamvi,

leo nakuja na kisa cha Dingi yangu, ni mkali sana, enzi tunakua ukimuona kwa mbali tu unatafuta pa kutokea, unafurahia zaidi kutokuonana naye kwa kuwa ukionana naye tu lazima utakuwa na hatia ya kujibu, hivyo dawa ni kukwepana hadi akutafute yeye. Kwa sasa mimi ni mtu mzima, nina maisha yangu lakini bado namuogopa sana, siyo mimi tu bali hata ndugu zangu, tumekuwa tukipanga mambo mengi ya kuongea naye na yote yanaishia hewani na mkifanikiwa kwenda kumuona mkifika tu getini kwake mnaanza kupungua na hatimaye mnasmbaratika hata kabla ya kuonana naye.

Siku moja tukachukuana na ndugu zangu ili tukampatie ushauri, wengi wetu tukiwa na miaka zaidi ya 30 na wengine wamegonga 40, tukafanikiwa kuingia getini, akatukaribisha viti, tukasema tunahitaji kuongea naye, ile kuanza tu kuongea mmoja wetu, yakawa ni mawazo tofauti na yeye, hakutaka amalize akamkatisha na kuanza kushusha maneno mazito, mimi nikasema naenda kukojoa nikaunganisha huko huko, ndugu zangu nasikia walitoka pale hawaioni vizuri njia, wanatembea utadhani njia imejaa makorongo. Kifupi kila tukipanga kwenda kumshauri mambo mbalimbali yakiwemo ya namna bora ya kuendesha shughuri zake, tumekuwa tukiishia tu kupanga.

Mwisho nimpongeze Dingi yangu kwa kuwa na uwezo wa namna hii, kwa kweli hiki ni kipaji na ni power kubwa, wachache wana uwezo huu hasa ukizingatia watoto wake wengi tumesoma na kufuzu katika fani mbalimbali, wapo maengeneer, madokta, wanasheria, wahasibu na hata wachumi na wanasiasa, lakini kafanikiwa kutumentain na kutusambaratisha katika kila mkakati wa kumwingia, tumebaki waangaliaji tu.

Je wazee wa aina hii unawaingiaje, maana kinachoniuma kuna mambo mengi hayafanyi kisomi na hivyo sisi watoto kuonekana kama wapuuzi na jamii maana mnaonekana kama hammsaidii baba yenu?.

Wanasema dawa ya baba mkali ni kumsifia sana. Jifanye unamkubali na kumuapreciate sana and all that, mwisho wa siku atakuweka karibu naye halafu utaanza kumshauri mambo ya msingi. Madingi wa namna hiyo wapo wengi sana.
 
aNGEENDA SHULE ANGEKUWA KAMA MUGABE AU CASTRO, ANA NYOTA YA UDIKTETANANGETUFAA SANA WATZ

Mkuu upo sahihi kabisa, huyu mzee huwa natamani kweli angepiga shule, naamini angekuwa kiongozi mzuri sana, ana ile commanding power, kama Sokoine tu, kama nchi tumepoteza fursa kwa dingi yangu.
 
Pole na hongereni kwa kuwa na baba wa aina hiyo kwani kwa njia hiyo ndio maana mko hapo mlipo. Ni kweli wapo wazee wa namna hii. nyie mpendeni tu, na ebu jitahidini kutoonyesha mnamuogopa, yaani hata akigomba nyie mko sawa tu tEna mnafurahi na mnaleta vichekesho fulani fulani, hivi hamuwezi hata kumchekesha halafu akifurahi tu hamkai sana mnaondoka.

Pia kama mna miji yenu msiende kumtembelea mara kwa mara, mnakaa kama mwaka mmoja hivi hata mamuendi kumtembelea hata kama mnakaa mkoa mmoja,then mnapanga kwa pamoja woote mnaenda kusalimia sikukuu moja mkiwa mmebeba zawadi mbalimbali kwa njia hiyo naamini anaweza kubadilika, na atafurahi hata ukali atapunguza.

Kwa uzoefu wangu, wazee wakali watoto wao wakianza kujitegemea tu huwa wanaacha ukali wanabaki kuwa rafiki wa karibu na washauri wa maisha
 
pole sana mkuu, ila tukumbuke tu msitu wa wazazi tunatakiwa tuupite pole pole, maana kuna laana, si unakumbuka katika amri 10 za Mungu, ipo ile ya waheshimu baba na mama yako..... Twende nao ila tuwe makini kudumbukia kwenye mtego wa ile amri.

Kusema kweli isingekuwa hapo, siku nyingi tungeweza hata kumpiga. Hapa mama ametusaidia pia kutulinda tumheshimu. Na ni katika utu uzima huu nilielewa na yeye pia ni binadamu mwenye udhaifu kama sie. Kama binadamu kuna wakati anatuumiza mno tunashindwa act hivyo. Mara nyingi tulinyamaza mpaka tulipoona haitusaidii sisi wala yeye.
 
JEKI mkuu naona una bahati kuwa baba sampuli hiyo, huyo ni mzuri mfano wa kuigwa ,angewadekeza msingefika hapo mlipo sasa!!
Bado anahitaji muwe marafiki zake kama itazidi kunyenyekea na kumpenda!!
Usitafute kushindana naye jenga urafiki simple!!
 
Last edited by a moderator:
Inatuhusu nini sasa? Kwanini msimalizane kifamilia huko? By the way baba yako ni mbabe nyumbani kwenu tu, si ajabu akifika kwa mama yenu mdogo anaosha vyombo!
 
Acheni uoga,hata me dingi yupo ivo na tulikuwa hatupumui but siku moja nilimkazia mpaka alidata,alitetemeka kupita maelezo.Hata hivyo nilikuwa sahihi kwa yale madai ya watoto.Alitekeleza na mpaka leo hesïma kwa mtoto mie ipo na wenzangu wananiona shujaa lao
 
Serious? kweli unampa huu ushauri ukiwa serious au unatania? Hata kama ni utani, kweli? Kweli akili zako zimeenda na Mapolomoko! You are really brain washed!

Hahahahahaha!! humu ndani ukiingia usipocheka utakuwa na matatizo.Hahaha, akili zimeenda na maporomoko!?, ya maji,ya mawe,au udongo?? Hahaha nimecheka sana aisee.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, ID ya jamaa niliyem quote ni Mapolomoko! Ushauri wake pia unaonyesha ni ule tu unaoweza kutolewa na mtu ambaye akili yake imeenda na Mapolomoko!
Hahahahahaha!! humu ndani ukiingia usipocheka utakuwa na matatizo.Hahaha, akili zimeenda na maporomoko!?, ya maji,ya mawe,au udongo?? Hahaha nimecheka sana aisee.
 
Last edited by a moderator:
Inatuhusu nini sasa? Kwanini msimalizane kifamilia huko? By the way baba yako ni mbabe nyumbani kwenu tu, si ajabu akifika kwa mama yenu mdogo anaosha vyombo!

sasa mkuu kama kila mtu atamalizana kivyake hili jukwaa litakuwa la nini sasa, au labda hujui umuhimu wa majukwaa kama haya? hapa tunachangia mawazo na kupeana ushauri na kushare taarifa. Au kwa nini wewe umeandika kwa nini usingekaa kimya tu.
 
Inatuhusu nini sasa? Kwanini msimalizane kifamilia huko? By the way baba yako ni mbabe nyumbani kwenu tu, si ajabu akifika kwa mama yenu mdogo anaosha vyombo!
inatuhusu sana ndg yangu, inakupa kuelewa aina ya wazazi tulionao na jinsi ya kuishi nao kama watoto, heshima ni muhimu kwa mzazi hata aweje! yapo mengi ya kujifunza kwenye post hii na hata comment za watu, mimi nimejifunza mengi na nimefurahi sana JEKI kutuletea hii post, kwanza nilicheka sana sana lakini baadae nikajikuta naona huruma sana na nikajiweka katika position ya watoto wa huyu mzee, kweli nimejifunza mengi sana.

we hujajifunza kitu kweli? ona pamoja na ukali wake huo, amesomesha watoto wake wote na amejipatia wataalam kibao na sasa wanafanya kazi na kwa vyovyote vile watamsaidia tu hata kama ana uwezo ipo siku atahitaji msaada wao, na hata akistaafu wao ndio walezi wake
 
Mimi mshua wangu alikuwa mpole kama Moyes wa Man, Ila bi mkubwa ilikuwa shida, anakudunda baada ya muda anasahau kama alishakudunda anakugonga tena kwenye kosa lile lile!
 
aisee, hongera sana mkuu, mimi nimetumia njia zote hizo, nimeandika barua lakini hazijibiwi, nimetuma hela na kununua vinguo, siku ukimuudhi anasema unadhani kangu ulonipa au tule tuhela ni kitu kwangu, mimi siyo wa vitu vidogo hivyo, kwa namna hiyo nimeamua tu kuwa mpole kwa kuwa sina uwezo wa kumjengea ghorofa.
hahahaha eti nimeandika barua hazijibiwi
 
Back
Top Bottom