JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,968
Za siku wanajamvi,
leo nakuja na kisa cha Dingi yangu, ni mkali sana, enzi tunakua ukimuona kwa mbali tu unatafuta pa kutokea, unafurahia zaidi kutokuonana naye kwa kuwa ukionana naye tu lazima utakuwa na hatia ya kujibu, hivyo dawa ni kukwepana hadi akutafute yeye. Kwa sasa mimi ni mtu mzima, nina maisha yangu lakini bado namuogopa sana, siyo mimi tu bali hata ndugu zangu, tumekuwa tukipanga mambo mengi ya kuongea naye na yote yanaishia hewani na mkifanikiwa kwenda kumuona mkifika tu getini kwake mnaanza kupungua na hatimaye mnasmbaratika hata kabla ya kuonana naye.
Siku moja tukachukuana na ndugu zangu ili tukampatie ushauri, wengi wetu tukiwa na miaka zaidi ya 30 na wengine wamegonga 40, tukafanikiwa kuingia getini, akatukaribisha viti, tukasema tunahitaji kuongea naye, ile kuanza tu kuongea mmoja wetu, yakawa ni mawazo tofauti na yeye, hakutaka amalize akamkatisha na kuanza kushusha maneno mazito, mimi nikasema naenda kukojoa nikaunganisha huko huko, ndugu zangu nasikia walitoka pale hawaioni vizuri njia, wanatembea utadhani njia imejaa makorongo. Kifupi kila tukipanga kwenda kumshauri mambo mbalimbali yakiwemo ya namna bora ya kuendesha shughuri zake, tumekuwa tukiishia tu kupanga.
Mwisho nimpongeze Dingi yangu kwa kuwa na uwezo wa namna hii, kwa kweli hiki ni kipaji na ni power kubwa, wachache wana uwezo huu hasa ukizingatia watoto wake wengi tumesoma na kufuzu katika fani mbalimbali, wapo maengeneer, madokta, wanasheria, wahasibu na hata wachumi na wanasiasa, lakini kafanikiwa kutumentain na kutusambaratisha katika kila mkakati wa kumwingia, tumebaki waangaliaji tu.
Je wazee wa aina hii unawaingiaje, maana kinachoniuma kuna mambo mengi hayafanyi kisomi na hivyo sisi watoto kuonekana kama wapuuzi na jamii maana mnaonekana kama hammsaidii baba yenu?.