There no victory without history

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,805
12,669
Habari ya asubuhi waungwana,bila shaka nyote ni wazima kabisa na kwa wale ambao mmeamka hamko sawa kiafya basi M/Mungu awafanyie wepesi muwe na afya njema..

Bila kupoteza muda ningependa kushare msala uliowahi kunikuta kwenye masomo yangu ambao kutoka na nature ya familia yangu ilibidi nivunge nisiseme kitu maana ningeharibu kabisa.

Nitatumia kodi kueleza lakini nadhani nitaeleweka

Katika familia yetu ina watoto zaidi ya kumi na mzee wangu kiuchumi alhamdulillah yuko vizuri hivyo aliweza kuwamudu wote kuwasomesha watoto wake bahati mbaya watoto wenyewe walishindwa kusoma na wengine walikataa wenyewe kusoma.

Mzee wangu ni mkali sana hivyo ikapelekea kua ngumu sana kua karibu nae na ni mtu mwenye hasira hivyo kila mtoto alimuogopa mno.

Sasa tuanze kisa chenyewe.

Mwaka X nilikua mwaka wa kwanza katika chuo fulani cha afya pale DSM nikichukua kozi ya Clinical Medicine..basi bwana kwakua mimi ndiye nilikua mtoto pekee niliyekubali kusoma basi nilipata full support kutoka kwa mzee katika huo mwaka wa kwanza hasa semista ya kwanza.

Nilianza chuo fresh nilikutana na watu mbali mbali tukawa tunasoma,ule mwaka tulikua 500+ na tuliobahatika kupenya semista ya pili tulikua 186 pekee...panga lilitembea sio mchezo.

Semista ya pili ilipoanza mambo yakaanza kua tofauti kukawa na migogoro mingi pale chuoni kati ya wanafunzi na uongozi wa chuo na kwa bahati mbaya ulipofika muda wa kufanya mtihani wa mwisho wa kumaliza mwaka wa kwanza nikajikuta assignment azionekani tulikua 13 akiwemo na KDG(waliosoma uzi wangu wa mwisho watamkumbuka huyu bwana) na tukakosa sifa za kufanya pepa la mwisho ikawa kimbembe pale kugombana na Academic officer tukaenda kushtaki kwa Director basi ikaamuliwa tutarudia semista hatukua na namna.

Nikarudi mwaka unaofuata hapo nilikua nishawaeleza home kilichotokea nyuma so hakukua na shida ila Mzee alinionya niwe makini vinginevyo atajitoa kwani bado kuna watoto wengi wanamtegemea hivyo niwe makini na miaka ya kusoma.

Basi bwana nikarudi mwaka unaofuata bado kukawa na shida basi kuna mwanangu huyu nitamuita MCHONGO akatoa wazo kua ana jirani yake alimalizaga Mbeya miaka 8 iliyopita yeye anafahamiana na Mkuu wa chuo wa pale kama vipi tukaongee nae atupe connection ya kuhamia hapo..tukaona safi huu ndo mchongo tukiwa Mimi ,Mchongo na Mshikaji wangu mwingine(now fundi gereji) tukaenda kwa huyo jamaa tukamueleza yanayotusibu akasema hiyo kazi ndogo tumpe siku moja afanye connection na Mkuu wa kule kisha atatujulisha.

Baada ya siku moja Mchongo akatuletea majibu mwana amefanikiwa ila amesema tuonane kesho tukaongee. Kesho yake mapema tukiwa watatu tukafika pale jamaa akatueleza ishu fresh ila mkuu wa chuo anataka 200k kwa kila mmoja ili kupata nafasi dah ikawa hela kubwa tukalialia pale basi jamaa akapiga simu kwa huyo mkuu wa chuo akaweka na loud akakubali kwa 150k kila mmoja na kama hatuna basi tusimsumbue. Dah tukajipiga kila mmoja akatoa huo mpunga tukamkabidhi pale pale akaituma baada ya hapo tukasikia yule mkuu anasema jamaa aende mbeya na vielelezo vyetu ili mchakato ufanyike na hawezi kutuma document yoyote mtandaoni,basi ilibidi tumchangie tena yule jamaa laki 1 ya nauli baada ya hapo tukaagana kukutana baada ya siku 3.

Tukiwa tumejawa na furaha tukaenda zetu beach kabisa kufurahi kiufupi tulichoka kua katika kile chuo cha awali..basi hata class tukakacha hivyo tukawa tunafuatilia mchongo wa kuhama tu(kipindi hiko hatujui unahamaje hivyo tulifuata maelekezo tu ya jamaa).

Baada ya siku tatu mwana akarudi akatuletea barua zikiwa na muhuli fresh kua tumepata nafasi hivyo tuanze maandalizi ya kupeleka barua wizara kipindi hiko wizara ndo zimehamia dodoma. Tukamuuliza vipi hakuna process ya kufuatilia chuoni pale matoke nk akasema haina noma hiyo ni muhimu.

Tukafuatilia pale chuo tukapata uhamisho na matokeo yetu fresh baada ya hapo tukasepa,,tukamkabidhi jamaa yule akadai tumpe sasa nauli ya kwenda Dodona nauli,gesti na ya kula tukasema fresh tukampa akasepa..hapo kila hatu nilikua namshirikisha mzee na hakua na noma japo sikumwambia kama kuna mtu ndo anafuatilia badala ya sisi..basi bwana jamaa akaenda zake Dom aliondoka mchana kufika kule usiku akalala akatutaarifu ,ilipifika asubuhi akatuambia ndo anaenda wizarani basi tukasubiri siku nzima hakuna majibu na simu hazipokelewi. Ilipofika saa 2 usiku nikaona simu ya MCHONGO inaingia akatuambia jamaa ameenda wizara ila wamegoma kutuhamisha kwa sababu dedlinie imeshavuka lakini kaongea nao kuna mtu anataka kutusaidia amesema amuone kesho hivyo tuwe na subira dah hapo nikaanza kuhamaki maana nilijua lazima atataka hela na ukicheki mpaja hapo laki 3 na point ishakatika kumuhudumia jamaa na hela niliyotoa kwa yule mkuu wa chuo. Basi kesho yake majira ya mchana tukiwa wote watatu jamaa akapiga simu kwa jamaa na akaanza kuteleza hali ilivyo ila kuna jamaa anasema yupo tayari kutusaidia kwa 700k dah tukashtuka maana hela nyingi sana na kibaya pale chuo ilikua zimetimia siku 21 bila kua darasani na uhamisho tushachukua tukapagawa kupoteza tena muda dah tukalia sana hadi 500k jamaa wakakubali

Tukapambana mimi nilitoa 200k na jamaa wakatoa 300k.Tukawapa basi wakafanya mambo,,kesho yake jamaa akasema amesihiwa akatumiwa 50k naulia hii mimi sikutoa chochote basi jamaa akasema tujiandae na safari sasa ya Mbeya. Hapo mwezi na wiki ushakata tangu semista imeanza na hatukuwahi soma chochote basi jamaa akarudi na barua zetu za uhamisho zikiwa na muhuli kabisa tukafurahi mno ile siku jamaa akasema haya wadogo zangu nimewapambania sana mpaka sasa basi nipeni mpunga tuliokubaliana maana kazi imesha. Wakati tunampa hii kazi tulikubaliana tungempa 150k ila jamaa akasema kwa tabu niliyopata tuongeze 50k dah tukalia mpaka 180k tukatoa kila mmoja 60k hizo pesa zote kumbuka tulikua tunaomba angalau mimi nilikua kidogo ninazo mfukoni mpaka hapo sikua nimeomba hela yoyote nyumbani..basi akapiga tena kwa yule mkuu tukaambiwa tuwahi tuko nje ya muda kwani CAT zimekaribia sana bado 2 weeks zianze na akatuambia ada ya kila mmoja ni 395k akatoa akaunti namba ilipwe kabisa ajabu ile ilikua akaunti binafsi tulivyohoji imekuaje tukakumbushwa kua muda uliishaisha so wao wanafanya msaada isingewezekana kutengeneza control namba kwa wakati ule so sisi tulipe mengine tumuachie yeye mkuu.

Basi tukatawanyika ili kesho tuanze safari nakumbuka mzee wangu alinipa 650k na kesho yake jamaa tulikubaliana tukutane Ubungo atusindikize hasi mbeya basi bwana tukiwa watatu tuko zetu ubungo jamaa akawa hatokei piga simu hapokei hadi saa 1 asubuhi akapokea akasema amepata dharura mwanae alikua hoi ila kwa sasa americover hivyo tutaondoka saa 4 kwa gari ya binafsi ya jamaa yake tutoke ubungo tukutane Kimara suka bahati nzuri hatukua tumekata tiketi. Basi tukafika zetu suka tukamkuta sehemu kuna kigrosari anapiga sumu akatukaribisha tukapiga supu pale akasema sasa tukalipie ada kabisa si vizuri kusafiri na hela bora tusafiri na risiti na copy zake basi tukatumbukiza pesa zote 395k kila mmoja tukarudi tena kwenye grosari ilikua saa 5 asubuhi jamaa anapiga simu pale kuongea na jamaa anamwambia afuate gari shekilango ipo tayari anatuaga anafuata tumsubiri dah ndo akawa katuachia manyoya hapo(TULIFANYA YOTE KWA SABABU MCHONGO ALISEMA YULE NI KAMA KAKA YAKE PALE MTAANI NA JAMAA HAKUONESHA NJAA WALA NINI MAANA HATA SIMU ZAKE ZA MADILI TULIMUAMINI SANA NA MCHONGO ALITUAMINISHA MBAYA).

Tulikaa pale hadi saa 8 mchana jamaa anasema nakuja nakuja mwisho simu ikawa off dah tukavurugwa tukakaa hadi saa 10 kimya mi nikaamua kumcheki bro wangu aliyekua anaishi kinyerezi nikamuelezea akasema Dah hebu mpe simu huyo jamaa yako nikampa akaongea nae akahoji maswali akawa anajing'atang'ata akinipa simu bro akasema Dogo hebu njooni home mimi nipo nione hizo barua.

Huyu bro kuna siku nitaeleza ana umuhimu gani kwangu maana si kaka wa damu ila alikua msaada sana mpaka leo ni kama ndugu yangu... Basi tukaenda alivyoona akasema tushatapeliwa hiyo ilikua saa 12 jasho linatutoka vibaya dah tushapoteza hela kibao kila mmoja akawa na hofu tufanye nini..tukaanza kumuuliza MCHONGO vizuri bado akawa hana majibu ..tukiwa hasira na hofu zimetukaba bro alitushauri tujipe muda kwanza angalau kesho basi asubuhi kesho piga simu mambo yale yale haipatikani basi tukamwambia Mchongo aende kwao akamtafute salale anasema hapajui yule kuna mtu alimuanganisha nae tu dah tukammaindi sana ikabidi amcheki yule aliyemconnect nae nae hakua na majibu anajing'atang'ata tu .

Baada ya hapo wale jamaa wakasepa nikabaki mimi sasa kwa bro alinishauri nisiondoke maana tayari nishavurugwa ila kwa jinsi anavyomjua mzee wangu akasema nivunge nikithubutu kusema jua ndo mwisho wangu wa kusoma.

Basi maisha mapya yakaanza pale kinyerezi nikiwa mafichoni huku nyumbani wakijua nipo chuo na ada washalipa yote..nilijaribu kumcheki yule jamaa kila siku ila sikumpata na Mchongo alibaki kusema tu samahani na yeye alikua kwa dada yake huko kajificha ni Mosha peke yeye alirudi kwao akamwaga mchele na baba yake akasema atafute shuguli ya kufanya chuo basi(mwana leo fundi gereji na maisha yanaenda) basi nilikaa kinyerezi kutoka mwezi wa 5 hadi wa 9 ndipo nikarudi home kama vile nimetoka Chuo na ni likizo.

Nilikaa likizo sasa kimbembe ikawa natakiwa nirudi chuo maana tayari likizo imeisha basi tarehe 14/10 mwaka huo basi nikapewa laki 550k hii ndo ilikua pesa ya mwisho kupewa na mshua kwani baadae ilipojulikana niliisoma namba...basi nilisindikizwa na bro wangu hadi stand ya ubungo akaniuliza umekata bus lipi nikasema Newforce basi nikapanda saa 12 kasoro 7 kabla bus hazijasepa bro akaondoka nikashuka kwa bus kwani sikua na tiketi..nikiwa nimekaa chini naweza niende wapi nikapata wazo la kwenda Mkoa fulani kusini mwa tanzania kwa mpenzi wangu lakini sikua nimempa taarifa na safari ikaanzia hapo....

Ilikua miongoni mwa safari ngumu kwmi sikumsemesha mtu na wala sikula chochote kwa mawazo mazito kwa masa yote 16 niliyosafiri nilifika usiku sana nikiwa getini nikampigia anifungulie akashangaa akaja chap nikaingia ndani akaniuliza vipi mbona umekuja hujaniambia na unaonekana hauko sawa nikamwambia nitamsimulia asubuhi...kesho yake asubuhi akaenda kazini aliporudi jioni basi nikamueleza alinihurumia sana mwishowe akaniambia atanisaidia kupambana...

Saa 8 usiku wa siku hiyo hiyo napokea sms whatsapp niende DSM kuna mama mmoja atanisaidia yeye anaconnection na watu wa wizara . Wakati nilipokua njiani kuna jamaa mmoja nilipewa namba na bro yule wa kinyerezi nimtafute yule jamaa nilipiga sana simu hakupatikana ila niliamua kumtumia ujumbe mrefu whatsapp ndo akawa amejibu saa 3 usiku ila nilifungua data saa 8 usiku ndo ujumbe ulikua umeingia..jamaa yeye alikua nje ya nchi wakati huo.

Basi sikulala ikanilazimu saa 10 alfajiri nigeuze kurudi Dar kwa siri kuonana na huyo mama ake na huyo jamaa kwani alishamwambia kila kitu..bus chap nikafika stand bahati nzuri nikapata siti japo ya mwisho safari nayo ilikua ngumu sana sikula chochote mpaka nafika..nilifika kwake saa 5 usiku akanipokea akanipa pole kisha akaniambia kuna mtu kesho itakua siku yake ya kwisho kukaa ofisini kwani anachukua likizo ikiwezekana niondoke asubuhi kwenda Dodoma haraka nikamuone..nikashukuru sana hapo Ndo ikaja stori ya KDG.

Dah nimechoka kuandika lakini nilikoma mpaka kurudi chuo ilinigharimu pakubwa mno...

Nitaendelea nikipata chance now bize kidogo kazini.
 
Back
Top Bottom