...to be on the safe side ili usiwekwe kiti moto na kuanza kujihami ni bora tu pale ambapo mapenzi yameshamiri kuanika kila kitu unachoona mwenzako anastahili kukijua kwa wakati huo.
...ina maana kumwambia 'udhaifu' wako na wa kwenu...au sio?
Tatizo hatuelewani, hakuna mwanamke anaye omba kichapo kutoka kwa mme wake, na hakuna sheria inayo sema wakubali kupigwa sasa vipi wanyamaze? Hawana mdomo wa kulalamika kwa nini wana nyanyaswa.
FYI, Mwenyezi mungu anasema hapendi wajinga....Sheria za mungu ziko wazi, mwanamke anaye nyanyaswa asikae kwa mme wake sababu mme wake hathamini kuwepo kwake.
Kumshakia mke wako anafanya kitu kibaya ni kosa, vipi ukampige makofi na kumnyanyasa....
Hayo yanayo zabuliwa vibao na kupigwa ni majinga lolo tu, hata kama angekuwa bibi yangu :A S shade:
...Siyo kila GF Babu DC!!! bali yule ambaye unaona kabisa kwamba kuna kila dalili ya wote kufikia maamuzi ya kufunga pingu za maisha.
...'bahati mbaya' na kwa makusudi kabisa, tunapokuwa tu wahitaji hasa kwenye mapenzi...tunajitahidi kwa kila liwezekanalo kutojionyesha tuna dosari yeyote....
...Naam mara nyingi huwa hivyo. Watu hawafikirii kile ambacho wamejaribu kukuficha huweza kumfikia mwenzio kupitia source tofauti na hapo kupunguza imani ambayo alianza kuijenga kwako na hili linaweza kuharibu na hatimaye kuuvunja kabisa uhusiano mzuri wa kimapenzi uliokuwepo.
....inategemeana na utavyojibu baada ya ukweli kubainika. Dont Panic...!
Sote tuna maskendeli na maskeletoni kabatini...mfano, unapohojiwa kwamba unatabia
mbaya ya uzinzi, upigaji, nk...jielezee vizuri tu Umejifunza na umebadilika ili kumjengea imani mpya
mpenzi wako...
Lakini ukijidai kupandisha hasira, Ooohh, "nani kakwambia....sio kweli!"...hapo unatengeneza mazingira
ya mwenza wako mpya ku doubt ukweli wako..Likewise, mapungufu mengineyo ya familia yenu, mfano
mawifi washari,....au 'wanga!'
...to be on the safe side ili usiwekwe kiti moto na kuanza kujihami ni bora tu pale ambapo mapenzi yameshamiri kuanika kila kitu unachoona mwenzako anastahili kukijua kwa wakati huo.
BAK,
Siyo rahisi kujua ni BF/GF yupo mtafikia hatua hiyo mkiwa bado kwenye hatua za awali. Kama ingekuwa hivyo, mauvumi ya mapenzi yasingekuwa yameenea kila kona.....Bado nasisitiza kuwa kuna umuhimu wa kwenda mdogo mdogo ili mtu asijeuza silaha za maangamizi kwa mwenzi wake pasipo sababu!!
Babu DC!!
...ina maana kumwambia 'udhaifu' wako na wa kwenu...au sio?
Mkuu Mbu nazungumzia mfano ambao King'asti ameutumia katika uzi huu.
BAK umeongea kitu muhimu sana. Sio ex tu ama watoto, kuna issue ya wanafamilia wakorofi pia. Hii tabia (hasa ya wadada) ya kujifanya unatokea familia takatifu is really disgusting. Hata kama babako mchawi muambie mwenzio, ajue u don't side with mambo yake. Ili hata huko mbele ya safari akikusakama nao umuambie the loss is his asiwacheke ndugu zako manake nao ni sehemu yenu.
...Hapo hatua za awali zinakuwa zimeshakamilishwa....Kila mmoja karidhika na mwenziye katika idara zote za mahusiano.
Hata mie sielewi mkuu,
Uanze kusema kuwa, unajua sweetie, baba yangu ni mchawi, kaurithi uchawi kwa bibi yake mzaa mama. Na mama yangu ni mwizi namba moja pale mtaani....Halafu, dada yetu mkubwa ni changudoa.....
Huyo GF/BF naamini atakuona kama nati fulani za kichwa zimelegea!!
BAK,
Haina tija kueleza negatives za familia yako, labda kama kuna sababu ya msingi au zitaingia katika equation ya maisha yenu huko mbele ya safari.
Na umri wangu huu, kuna mambo kibao ya familia yetu ambayo sijawahi kumweleza Bibi DC na wala sitamwambia. Naamini hata yeye akija kuyajua hataniuliza kwa sababu yajaadhiri ndoa yetu kwa namna yoyote ile.
Babu DC!!
naomba nimsaidie mkuu DC kujibu, ....mfano kuna "ugonjwa wa wazimu kwenye familia"...
mwache akishaingia kwenye uhondo wa ngoma, aicheze.
Nami Baba Ashrat ntakuja na yangu yaliyomnasisha Mama Ashrat
Kumbe mpo wote humu eeee!! Hapo nimewakubali, hongereni na mzidi kusonga mbele na kutusaidia mauzoefu.Itakuja tu wala usijali mwaya.
Kumbe mpo wote humu eeee!! Hapo nimewakubali, hongereni na mzidi kusonga mbele na kutusaidia mauzoefu.
Tupo tumejaa tele.
Mama Ashrat ndio ubavu wangu
Yeye ndio mwenza wangu
Naombea watu wasituletee majungu
Maana Mwenye'ezi ndio kanitunuku
Kwake mimi taaban
Hata watu wachokoe vipi
Mimi sisikii wala sioni
Kumbe kuna watu wana akili MMU
...Hapo hatua za awali zinakuwa zimeshakamilishwa....Kila mmoja karidhika na mwenziye katika idara zote za mahusiano.