Vibaka, wezi, panya road wanazidi kuadimika mitaani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,929
Ni mkakati unaoratibiwa kwa usiri mkubwa sana! Kwa sehemu sio vibaya kuupongeza japo kuna makosa ya kibinadamu kwa kukosea target ama kuchomekewa asiye husika!

Siku hizi ukipelekwa polisi kwa kesi ya wizi hasa huu wa kupora, kukaba watu vichochoroni, ama kuiba majumbani ukifikishwa huko salama na kufanikiwa kupandishwa kizimbani katambike kwenu kwa mizimu yote yote ya kwenu na ukoo wenu Wote.

Wenye hali mbaya zaidi ni wale ambao tayari wana faili huko police... Watalala wakipumua lakini hawata amka tena...!!! Kuna ziraili mtoa roho hupita mahabusu usiku na kuondoka na watu wake!

Fundi wangu wa ujenzi Twalika kalala mahali pema huko makaburini .. Kumbe alikuwa na kazi nyingine ya overtime kiza kkiingia na wananchi wakiwa wameshalala kabisa

Alitoka kwenye pombe mida ya saa sita usiku lakini saa tisa alfajiri akakutwa kwenye dari ya watu na zana zake za overtime.. Wakamfinya kisawasawa lakini hawakummaliza.. Kulipopambazuka akapelekwa kituo kidogo

Akapatiwa huduma ya kwanza kwenye zahanati karibu na hicho kituo akipata nafuu kidogo.. Wakati ndugu wanajipanga kwa dhamana ya mchongo wakubwa kituoni wakaona ndugu wako mwendo wa kinyonga.. Ilitakiwa 150K

Wakapiga simu kituo kikubwa likaja difenda na wale ndugu wale.. Kufika hawakutaka la mwadhini wala la mnadi swala! Wakamtupia mtuhumiwa kwenye difenda kama kiroba wakaondoka naye..

Hiyo ilikuwa asubuhi ..kabla jua halijazama tukapokea habari za huzuni kubwa! Twaliha alizidiwa kituoni wakati wakijiandaa kumpeleka hospitali kubwa!

Inasemekana pale alikuwa na faili lenye kesi mbili!
Pombe
Kipigo
Njaa.... Hakuna wa kulaumiwa...!!!!
Ikaisha kama hivyo .. Tumezika juzi..

Zaidi soma

Ikaisha kama hivyo .. Tumezika juzi
Wanafinywa bila kelele
 
Safi sana

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningekuwa raisi, aiseee!!!!

Kwanza ningewagonga vibao na stick polisi, vibaka na wezi na majambazi wawashinde askari wangu/wetu ambao tunawasomesha kwa gharama kubwa na wana zana za kivita??
 
Last two weeks tulizika vijana wawili, walijifanya bingwa sana wakaingia dukani mchana kweupe, wakamkata mhudumu mapanga, kilichowakuta...walichomwa pamoja na bodaboda yao.

Likewise, wezi wa kalamu nao waandaliwe namna yao. Wanaliibia taifa kila siku na hatuwezi kufanya lolote tena billions of money.
 
Back
Top Bottom