Panya aliyefungwa kengele kuzivuta sharubu za panya

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,900
4,624
Nikienda kwenye hoja moja kwa moja niseme. CCM ni panya aliyejifunga kengele kuzikamata sharubu za paka.

Roman katoliki ni taasisi inayoheshimika duniani na kuogopwa na watawala wengi. Kikubwa cha kuogopwa kwao ni usomi na ubobezi wa kuweza kuleta mageuzi ya kimfumo na utawala wa nchi nyingi katika sayari yetu.

Siku chache zilizopita baraza la maaskofu Tanzania lilitoa waraka wa kukataa mkataba wa bandari na DP World. Katika waraka wao uliosomwa makanisani kote kwa jumla ya majuma 6 haukuwa na option ya kuridhia ikiwa kutakuwa na marekebisho katika mkataba basi wangebadili msinamo. Wao walikuwa na kauli moja tuu kwamba mkataba ufutiliwe mbali.

Wananchi tumepigwa na butwaa kuona jeuri ya ccm ikiongozwa na rais Samia kuendelea na mchakato wa kuwakabidhi waarabu bandari huku mshehereshaji mkuu wa waraka wa TEC fadher Kitima akiwa miongoni mwa wageni waalikwa kwenye sherehe hiyo ya kukabithi bandari.

Hatujui kama fadher alienda kwa hiari au alitekwa maana hata wakati hayo yakiendelea kulikuwa na tambo za ccm kuwa hata wale waliokuwa wakipinga suala la bandari wapo nasi hapa shereheni kushiriki na kula ubwabwa.

Maneno yaliyosikika ni kwamba eti ccm imezingatia maoni ya wananchi katika kelele yao ya kupinga mkataba. Lakini swali linabaki ni nani aliyeona hayo maandishi ya maoni yaliyozingatiwa?

Labda baraza la maaskofu TEC walipewa hayo yaliyozingatiwa kwa maandishi wakayasoma na ndio maana wametuma mwakilishi kwenye kukabidhi bandari kwa Muarabu. Kama sii hivyo kwamba waliwalaghai mbele ya umma waliokuwa wakijaribu kutetea rasilimali asili za Taifa, basi ni wazi kuwa hawana hofu na hii taasisi na wamejipanga kwa lolote.

Kwetu raia tubaki tukiamini waraka wa TEC ulimaanisha kile walicho demand la sivyo itakuwa TEC wamesaliti haki ya kuwatetea wasio na sauti na kuungana na kikundi cha wachache wasiozidi watu 100 wanaotaka kuitafuna nchi kwa mikono michafu.

Ndio maana nasema panya sisiem kajivika ujasiri wa kuvaa kengele dhidi ya paka TEC. Kama panya akishinda hii vita basi itakuwa historia kwa kizazi kilichoamini kuwa paka (RC) ni taasisi makini na yenye nguvu duniani imefutwa.

Lakini ikiwa vinginevyo kwamba paka amefia katika jaribio la kuvuta ndevu za paka basi ukweli wa milenia mbili utabaki pale pale juu kuwa hakuna mamlaka inayoweza kuwajaribu RC ikabaki kuwa salama.

Assalamualaikum, Bwana Yesu asifiwe, tumsifu Yesu Kristo.
 
Peleka huko Mikwara yako Mbuzi,hii Nchi ni huru inayoongozwa kwa kufuata Katiba Sheria n'a kanuni zake.

Haiongozwi kwa kufuata Biblia Wala maagizo yeyote kutoka popote pale duniani.Ina viongozi makini wanaojua NN Cha kufanya na wakati Gani.

Hiyo mihemko Yako ya kidini ipeleke huko mnakokutana na kudanganyana.
 
Peleka huko Mikwara yako Mbuzi,hii Nchi ni huru inayoongozwa kwa kufuata Katiba Sheria n'a kanuni zake.

Haiongozwi kwa kufuata Biblia Wala maagizo yeyote kutoka popote pale duniani.Ina viongozi makini wanaojua NN Cha kufanya na wakati Gani.

Hiyo mihemko Yako ya kidini ipeleke huko mnakokutana na kudanganyana.
Kupeleka makubaliano bungeni ndio kufuata sheria na katiba?
Rais wetu kasikika akisema ikiwa vitabu vitakatifu vinavunjwa na wahusika sembuse katiba ambayo ni kijitabu tu.
Maana ya maneno haya ni kwamba katiba ya nchi kuvunjwa na mamlaka sii hoja.
Unaposema katiba na sheria kufuatwa ni kwa sababu hujajua kuwa bunge halijadili makubaliano kwa mujibu wa katiba ila mikataba.
 
Waraka wa TEC umeisha muda wake. Amka kutoka usingizini acha watu wapige kazi bandarini kuondoa utapeli na ufisadi.
 
Waraka wa TEC umeisha muda wake. Amka kutoka usingizini acha watu wapige kazi bandarini kuondoa utapeli na ufisadi.
Tapeli na fisadi ni wafanyakazi bandarini au serikali?
Kama ufisadi wa nchi hii unafanywa na watawala tutajiridhishaje kuwa huo mkataba ni wa kifisadi
 
Back
Top Bottom