Nasikia Panya Road wamerejea kwa kasi DSM wanatafuta fedha ya sikukuu; chukua taadhari

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,105
Kuna jamaa yangu kavamiwa jana huko maeneo ya Kinyerezi na kundi la vibaka wakamsachi na kuchukua kila alichokuwa nacho. Anachoshukuru ni kwamba amefanikiwa kuondoka akiwa mzima wa afya na sasa yupo njiani kurejea Mwanza. Naongea naye ananiambia kwa idadi ya vijana waliomvamia aliona kifo kimekaribia; kila akikaa anashtuka akidhani wanamvamia upya aaaaahaaa. Omba yasikukute.

Naamini Kamanda Mlilo Jumanne ataangaika na hawa wajinga wajinga wasiofanya kazi wanaotamani kula bila jasho. Soon nategemea kusikia jambo kutoka kwa Mzee Mlilo ili sisi tunapotegemea kuuza samaki tuwe free kuja kula maisha mwisho wa mwaka jijini huko.

Lakini pia Nimwombe Mzee Mlilo aongeze nguvu kwenye ufuatiliaji wa vifaa kama simu na laptop zinazoibiwa. Zitasaidia sana kukamata huu mtandao. Huyu ndugu yangu kaibiwa simu na laptop ila aliporipoti polisi nadhani wao siyo issue serious sana kuifanyia kazi.

Tukiwekeza kufuatilia simu zilizopotea tutapata wahalifu wengi sana na kuwaadhibu kwa makosa wanayotenda
 
Kuna jamaa yangu kavamiwa jana huko maeneo ya Kinyerezi na kundi la vibaka wakamsachi na kuchukua kila alichokuwa nacho...
Sasa zile kejeli za kuwatania wanaume wa dar nadhani kaziona huwa inakuwaje hali halisi.

Kikubwa ukiingia kwenye tageti za watu wengi namna hiyo sio rahisi kushindana nao labda watake vitu vingine tofauti na pesa na simu hapo mtu unamua kufa na mmoja wao.
 
Waswahili tulivyo kua na upumbavu mtu unajua kabisa mwanao au mtoto wa jirani ni jambazi alafu unamfichia siri eti unaogopa kuonekana mnoko, hao wapumbavu wangekua waki kamatwa adhabu yao iwe kupigwa mapanga hadi kifo kama wao wanavyo fanya wakivamia watu
 
Kuna jamaa yangu kavamiwa jana huko maeneo ya Kinyerezi na kundi la vibaka wakamsachi na kuchukua kila alichokuwa nacho. Anachoshukuru ni kwamba amefanikiwa kuondoka akiwa mzima wa afya na sasa yupo njiani kurejea Mwanza. Naongea naye ananiambia kwa idadi ya vijana waliomvamia aliona kifo kimekaribia; kila akikaa anashtuka akidhani wanamvamia upya aaaaahaaa. Omba yasikukute.

Naamini Kamanda Mlilo Jumanne ataangaika na hawa wajinga wajinga wasiofanya kazi wanaotamani kula bila jasho. Soon nategemea kusikia jambo kutoka kwa Mzee Mlilo ili sisi tunapotegemea kuuza samaki tuwe free kuja kula maisha mwisho wa mwaka jijini huko.

Lakini pia Nimwombe Mzee Mlilo aongeze nguvu kwenye ufuatiliaji wa vifaa kama simu na laptop zinazoibiwa. Zitasaidia sana kukamata huu mtandao. Huyu ndugu yangu kaibiwa simu na laptop ila aliporipoti polisi nadhani wao siyo issue serious sana kuifanyia kazi.

Tukiwekeza kufuatilia simu zilizopotea tutapata wahalifu wengi sana na kuwaadhibu kwa makosa wanayotenda
christmass na mwakampya zimekaribia, watu hawana hela, kila mkoa RPC anatakiwa aandae watu wake wafanye doria sana kwasababu miezi hii uovu huwa unaongezeka kila mwaka. kila mkoa wanalalamika vibaka kuanza kuvamia nyumba za watu. nilikuwa Dodoma jana maeneo yua ilazo wanasema kuna mtu ameuawa kabisa tena mchana, wamekuja na bunduki wakapiga hodi wakaua wakaondoka.
 
Back
Top Bottom