SoC01 Namna ya kufanikisha mapinduzi ya kilimo kuelekea 2025

Stories of Change - 2021 Competition

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Nyanja: Kilimo
Andiko hili linapendekeza kwmb ili kuleta mapinduzi makubwa ya sekta ya kilimo yatayoendana na muda waDira ya Taifa 2025; sekta ambayo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi ambao kw mantiki hiyo basi Dira hiyo inaitegemea ili kuliingiza taifa ktk pato la kati-la-juu. Kimsingi ni ukweli usiokanushika hata kw kanuni za kisayansi kwmb Tz ina mazao mengi, nchi ni kbw na kilimo ndiyo kimeajiri watu wengi pia, hivyo basi, ili kuleta mapinduzi ya kilimo, ni budi km taifa tukachukuwa hatua za makusudi kabisa za dharura za kuokoa kilimo chetu. Mojawapo ya hatua zitazochukuliwa na Srkl ktk utendaji wake, andiko linapendekeza pia kwmb yafuatayo yafikiriwe:-

Srkl itumie kanda zake zilizopo za utawala au ibuni kanda mpya za kilimo kw kutumia vigezo vya jiografia, uoto wa asili & hali za hewa.

Srkl ikishirikiana na wadau wa kilimo ianzishe mazao ya kimkakati ya kanda kw kanda zote, mfano:-

  • Kanda ya Ziwa - zao la kanda linaweza kuwa ama pamba, miwa au mibuni.

  • Kanda ya Kati - zao la kanda linaweza kuwa ama karanga, alizeti, nafaka au mizabibu.

  • Kanda ya Magh - zao la kanda linaweza kuwa ama tumbaku au michikichi.

  • Nyanda za Juu Kzn - zao la kanda linaweza kuwa ama mibuni, migomba, mpira au mpunga.

  • Kanda ya Pwani - zao la kanda linaweza kuwa ama viungo vya vyakula, matunda, mihogo, katani, mwani au vanila.

  • Kanda ya Kus - zao la kanda linaweza kuwa ama korosho, tumbaku au mihogo.

  • Nyanda za Juu Ksn - zao la kanda linaweza kuwa ama pareto, nafaka, chai au miti ya mbao.

  • Kanda ya Mashariki - zao la kanda linaweza kuwa ama miwa au nafaka aina za mpunga & mahindi.

  • Uteuzi wa mazao ya kimkakati ya kanda uzingatie ujumuishaji wa mazao ya ama biashara au chakula pia.

  • Mazao mengine yote ambayo hayataangukia kwy kundi la mazao ya kimkakati ya kanda yatabaki kuwa ni mazao ya ziada ambayo yaendelee kulimwa kw utaratibu uliopo.

  • Taifa ligatue kilimo: Srkl kuu ishughulike na mazao ya kimkakati ya kanda tu na TAMISEMI ishughulike na mazao ya ziada pekee.

  • Ziwepo bodi au wakala (ziwajibike kw Srkl kuu) wa mazao ya kimkakati ya kanda na pia bodi au wakala (ziwajibike kw TAMISEMI) wa mazao ya ziada.

  • Kuwepo ushirikiano wa krb kati ya Srkl kuu na TAMISEMI.

  • Mazao ya kimkakati ya kanda yalimwe na mikoa yote iliyopo ndani ya kanda husika kw sababu jiografia zao zinashabihiana na hiki kiwe moja ya vigezo vikuu vya kugawa kanda hizi za kilimo.

  • Srkl pia licha ya mkulima mmoja mmoja au kampuni, ianzishe mashamba yake (ambayo yatatumika km mashamba-darasa pia) ya mazao ya kimkakati ya kanda kw kila kanda km ambavyo tunaona inamiliki mashamba ya mifugo sambamba na wafugaji mmoja mmoja. Hii ni kw sababu Srkl inayo nguvu kbw ya mtaji, wataalam, lkn pia kisheria ndiyo mmiliki-mama wa ardhi yote ya nchi na vyanzo vyote vya maji. Km mashamba binafsi yatashindwa kufanya vzr kutokana na changamoto za mtaji, wataalam, majira au hata eneo la kutosha, basi mavuno yatokanayo na mashamba ya Srkl yatafidia pengo hilo la mavuno toka ktk mashamba binafsi ambayo yatashindwa kufanya vzr. TAMISEMI nayo pia hali ikiruhusu iwe na mashamba yake ya umma kw kila wilaya.

  • Uwekezaji mkubwa wa kilimo cha skimu uanzie kwy mashamba haya ya mazao ya kimkakati ya kanda kwz na hasa mashamba ya Srkl.

  • Kila Mtz mwenye rika stahiki, afya ya mwili na akili awe na shamba lisilopungua hekari 1 au pia wanaweza kumiliki hata kw utaratibu wa vikundi vya ushirika.

    Manufaa yatokanayo:-
  • Ubunifu huu utafanya wakulima waione Srkl pia ikiwa ndani ya kazi ya kilimo kivitendo na siyo kinadharia/kisera tu. Dhana ya siasa-ni-kilimo (Azimio la Iringa) itahuishwa na kutekelezwa kivitendo.

  • Mageuzi haya au ugatuaji huu wa kilimo utaleta urahisi ktk kusimamia tasnia hii kw tija. Ni rahisi kw Srkl (kuu) kusimamia mazao ma-8 tu (zao 1 kw kila kanda) kuliko utaratibu wa hivi sasa ambapo inasimamia utitiri wa mazao yasiyokuwa na idadi na bado kilimo kisifanye vzr.

  • Uchache wa bodi za mazao (mfano mazao ma-8 tu ya kimkakati ya kanda) utapunguzia Srkl mzigo mkubwa wa kuratibu utitiri wa bodi za mazao.

  • Srkl kuu kwy ilani zijazo za uchaguzi isisitize mazao ya kimkakati ya kanda tu na TAMISEMI nayo ikampenie kwy uchaguzi wa SM mazao ya ziada tu. Srkl 2 hizi kw habari ya kilimo zikutane tu kuwa wamoja kwy malengo mapana ya taifa yaliyo kwy dira yake.

  • Ubunifu huu utashamirisha na utafanikishwa na shughuli za tafiti-pana ktk masoko ya mazao na mitaji, pembejeo, viuatilifu, udongo, mafunzo ya maafisa-ugani na wakulima pia, skimu nk.

  • Km ambavyo falsafa ya ulinzi na usalama ya nchi inavyosisitiza kwmb kila raia ni mlinzi wa Tz, basi kilimo nacho kije na falsafa ya kila raia ni mkulima licha ya kazi yake nyingine rasmi au binafsi.

  • Ubunifu huu ukitekelezwa kw tija utaifikisha nchi kw miaka ya baadaye ktk viwango vya kuweza kulisha walau ukanda 1 wa bara la Afrika mfano EAC au hata GLR km ambavyo India nchi 1 tu inao uwezo wa kujitosheleza kw chakula na kw wakati huo mmoja kulilisha bara la Afrika, hivyo India ina uwezo wa kulisha 33% ya watu wote wa dunia yaani India 17% & Afrika 16%. Mwl. Nyerere, enzi za uhai wake, yeye mtu 1 tu aliweza kulima na kulisha kijiji kizima cha Butiama. Kilimo chake hakikuwa cha kutengeneza faida bali cha msaada aghalabu kw watu wasiojiweza kwnza akitekeleza kw vitendo falsafa ya itikadi ya ujamaa-wa-kiTz inayopinga faida kbw ya mtu 1badala ya faida ya umma mzima.

  • Uwekezaji makini ktk kilimo utafunguka ghafla kw kiwango kikubwa ambapo huenda taifa likashuhudia utitiri wa viwanda vya mazao ya kilimo, pembejeo, viuatilifu, maghala na taasisi za utafiti vikianzishwa.

  • Ni rahisi kw Srkl kw kushirikiana na wadau-wawekezaji wakajenga viwanda vi-8 tu kw kuanzia (ki-1 kw kila kanda ya kilimo) ambavyo vitachakata mazao ya kilimo aina ya zao la kimkakati la kanda. Ili kufanikisha hili kw urahisi na kw haraka, Srkl iingie ubia na sekta binafsi ktk kuvianzisha viwanda hivi vinane vya kuanzia.

  • Ubunifu huu utaboresha mnyororo wa thamani ya mazao na hivyo kupata bei nzuri sokoni.

  • Ukubwa wa kanda za kilimo km zikilima kw bidii kbw utaweza kukidhi viwango vya mahitaji ya mazao ya kuchakatwa na viwanda hivyo vya mazao hayo ya kimkakati kw mwk mzm. Hivyo viwanda havitasimamisha uzalishaji kw kigezo cha malighafi kukosekana na pia ajira kwy viwanda hivi kw mantiki hiyo hazitasimama.

  • Viwanda hivi vitapanua wigo wa ajira mashambani na viwandani.

  • Aidha, ubunifu huu utaongeza thamani ya ardhi ambapo wale wasioweza kulima lkn wanamiliki ardhi za mashamba wataweza kuzikodisha kw makampuni ya kilimo, mkulima mmoja mmoja au hata vikundi vya ushirika vya kilimo na wakapata mapato mazuri ya kodi ya kuendesha maisha yao.

  • Utekelezaji wa mkakati huu km taifa litanunua wazo hili utaleta matumizi bora ya ardhi nchini na mazingira yatahifadhiwa.

  • Ni rahisi kw Srkl kuanzisha bima ya kufidia mazao ma-8 tu ya kimkakati ya kanda kuliko kufidia mazao mengi yasokuwa na idadi.

  • Wakulima wote nchini watafikiwa na kuhudumiwa na Srkl kupitia mazao ya kimkakati ya kanda tu kw sababu kila mkulima atalazimika kulima zao la kimkakati la kanda yake mbali na mazao mengine ya ziada.

  • Mahala pengine duniani zao 1 tu linaweza kuendesha uchumi wa nchi nzima, Tz ikiwa na mazao ma-8 makuu yatayolimwa kw kiwango cha kuliingiza taifa kwy rekodi ya dunia nchi hii itaweza kuinuka zaidi kiuchumi. India ni maarufu duniani kw zao la pamba tu, Brazil zao la karafuu tu, Bangladesh zao la katani tu, Burma zao la mpunga tu, Cote D’ ivoire & Ghana zao la kakao tu, Nigeria zao la mchikichi tu, Liberia zao la mpira tu, Kenya zao la chai tu, Zim zao la tumbaku tu, Malawi zao la chai tu, Znz mazao ya karafuu, mwani na vanila tu, mazao mengine hata yakilimwa yanabaki kuwa ni ziada tu lkn siyo nembo ya taifa husika.

Andiko linapendekeza kw Srkl kutafuta ushirikianao na mataifa yaliyofanya vzr kwy kilimo aghalabu km Israel, China, India, Afrika Kusini, Marekani, Thai, Braz, Burma & Misri kw uchache. Hii itahusu pia miradi ya skimu za umwagiliaji, ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao na uzalishaji wa pembejeo na viuatilifu, uboreshaji na upanuzi wa taasisi za utafiti wa kilimo na mafunzo. Kw makusudi kabisa kuna haja ya taifa kutengeneza masetla wachache wa mfano wa kutunza/kujibu dharura ya Dira ya Taifa 2025 kw habari ya kilimo.

Tunaposema Dira ya Taifa 2025, tunamaanisha kilimo kupiga hatua hadi kuwa chanzo kikubwa cha kwz cha mapato ya taifa, kw sababu kilimo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi na ndiyo mwajiri wa Watz wengi, na siyo kwmb viwanda ndiyo uti wa mgongo wa uchumi kw sababu pia sekta hii ya viwanda inamilikiwa na watu wachache kulinganisha na kilimo. Tukihimiza viwanda tunawafikia watu wachache, tukihimiza kilimo tunafikia 80% ya wote. Tunaposema uti wa mgongo wa uchumi maana yake ni taifa kujipambanua kw shughuli ya uzalishaji ambayo ndiyo inayoshirikisha walio wengi kwy mfumo wa uchumi wake.

Naomba kura zote.
 
Back
Top Bottom