Namna mshikaji wangu anavyoishi ukweni kwa furaha na amani tele

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,818
Sio mpenzi wa jf na hafagilii mitandao mitandao hii so hakuna noma.

Mwamba huyu alikutana na demu wa kishua yaan kishua haswa, mwana ni un employee kwa sasa, kama ujuavyo mjini maisha ni gharama na mapenzi ni gharama haswa, sasa hakujua kama huyu binti ni wakishua yaan mama baba tajiri ni zali tu nazani, ila baadae ndo akastuka demu anakaa kwao ghorofani ndo akajua kile kina kirefu sasa mbinu za kivita zinahitajika.

Demu wazazi wazungu wazungu hawana hiyana, so akawa anampeleka mshikaji hapo kwao, kamtambulisha na nini, mwana nae mchangamfu sana, uongo mwingi, akawachangamkia sana wazazi yaani akifika kwao na demu ni anazungumza na kila mtu pale ana msifia kila mtu pale.

Sasa siku moja kamkuta mama mkwe anaumwa miguu imevimba, mshikaji bila haya bila uoga akaomba mafuta ya masaji, akaanza kumkanda bi maza na kumchua vizuri mbele ya familia yote, baba mkwe anashangaa iki nini? demu kapigwa butwaa, kaka zake wanashangaa ebhana hii kali, mwana yuko bize anamkanda bi mkubwa miguu huku ana mwambia "wewe ni mama angu mzazi siwezi kuona unateseka hivi na mie kijana wako nipo hapa".

Sasa ikawa ile familia ata itake nini, msela atajitolea kwa asilimia 100, akija hivi mchana akamkuta baba mkwe amekaa kwenye sofa anatizama tv anaenda kwenye friji anamletea mzee maji anamwambia "baba kunywa maji mchana huu mwanadamu analoose maji mengi mwilini", halaf anampa demu care ya ajabu, akiwa home kwao pale hata mtu alalamike bando limemuishia yeye anasema ngoja nikakuchukulie vocha dukani na anaenda haigizi. Sasa katengeneza dependency ya ajabu, familia nzima inamtegemea mno.

Sasa imefikia point familia nzima inamuamini haswa, baba mkwe siku hizi anamtuma mwana akamchukulie kodi kwenye nyumba zake za wapangaji huko Tabata na mwana ni muaminifu haswa.

Ananiambia january hapo anaanza kazi shirika flani hivi la mafuta lipo kigamboni, baba mkwe kamconnect, na anaishi kwao na demu safi kabisa na wazazi wa demu wameshamwambia demu kwamba hatoolewa na mtu mwingine isipokua huyu na wazee wana mcount kama blessing mpya kwenye familia yao.

Hitimisho
Vijana igeni mifano, mambo yakiwa hayaeleweki wewe jizime data tu, swallow ur pride. Habari hii ni ukweli kwa asilimia 100, ni hapa hapa dar, hakuna neno ata moja la uongo nililo liongezea, nimeshuudia kwa macho yangu na sasa ata huyu demu wake ni rafiki angu pia.
 
Jamaa Yako hayupo JF? Je wakwe na shemeji zake hawapo huku? Achilia mbali mpenzi wake maana tayari mapenzi upofu.

Ujumbe mzuri unawafundisha nyie vijana, ila upo wazi sana. Kiasi mmoja wa wanafamilia akiona, anaweza kuhisi kumbe jamaa yako vyote anavyofanya ni maigizo ili mambo yake yaende na akitoka hapo anaenda kutangaza Kwa watu.

Jifunze namna ya kulifikisha jambo bila kuleta athari Kwa muhusika mkuu au watu anaofahamiana nao.
 
Jamaa Yako hayupo JF? Je wakwe na shemeji zake hawapo huku? Achilia mbali mpenzi wake maana tayari mapenzi upofu.

Ujumbe mzuri unawafundisha nyie vijana, ila upo wazi sana. Kiasi mmoja wa wanafamilia akiona, anaweza kuhisi kumbe jamaa yako vyote anavyofanya ni maigizo ili mambo yake yaende na akitoka hapo anaenda kutangaza Kwa watu.

Jifunze namna ya kulifikisha jambo bila kuleta athari Kwa muhusika mkuu au watu anaofahamiana nao.
Familia ile uzungu uzungu sana, wako exposed na life la nje, hawana mtimanyongo, pili mwanangu hana baya na he is for real na wao wanajua.

Halafu mambo hayo alianza kwao muda mrefu kidogo na ata mwanangu aliniambia kwamba kuna ndugu ndugu walimletea gozi gozi na maneno mengi yalishasemwa so hakuna noma na niliyazingatia haya wakati najiuliza kuandika hapa.
 
Back
Top Bottom