X wangu kamwita mwanaye jina langu

mwanyaluke

JF-Expert Member
Jan 22, 2015
473
1,448
X wangu kawa single mother na kampatia mwanae Jina langu, mwaka 2014 ni mwaka nilipata KAZI ya kuajiriwa ya Serikali, kabla ya kupata ajira nilipitia msoto wa kibabe Sana, pamoja na marehemu baba yangu kuacha Mali za kiasi, bi mkubwa hakuniamini kabisaa na alikuwa aniona chenga sana so bada ya kumaliza degree yangu ya Sheria 2010 nilisota hadi kusomea postgraduate ya ualimu na kipindi hicho Cha kusota ndicho pia nilipitia mitihani migumu Sana ya mapenzi.

Wanawake wanataka pesa na pesa huna so unakaa hata miezi mitatu na ukame wako, mwendo wa kuwinda wapya nao akitanguliza Ombi la pesa humpati au utampata mara chache, ukipata demu umzamishe gheto hapo home unakadiria bi mkubwa hayupo ndio unaingiza ndani (wenye mama wa kikinga mnaelewa hili mama zetu wana uchungu Sana na Mali ndio wamefanya wakinga wawe bahili, japo Mimi myakyusa ila mama mkinga) baada ya kukosa ramani nikawa namla tu beki tatu wa jirani(namshukuru Sana yule beki tatu alinifariji sana, ningekuwa jela na kesi za kubaka sijui alienda wapi yule mfariji Nina zawadi yake). Baada ya msoto nilipata kazi hii ya ualimu ndio bi mkubwa alianza kuamini Mimi ni graduate na baada ya kuanza kufanya mambo yangu ndio kaka zangu waliniamini na kunikabidhi project za Mzee.

Nawarudisha nyuma mwaka 2007 nikiwa form six nilianzisha mahusiano na huyu demu nilimuelewa sana na tukawa na mapenzi Moto Moto, nakumbuka nasafiri Toka Iringa natoroka chuo naenda Dar kufuata mahaba, mambo yalikuwa poa sana, baada ya Mimi ku graduate, Mzee kufariki aliyekuwa ananiamini Sana, mambo yaalibadilika Sana ugomvi na huyu demu ukawa mkubwa akiomba kitu Sina mara anite bahilii, mshamba, Sina status ya kuwa na yeye nk.

Kiufupi nilikuwa napewa papuchi Kwa masimango sana na Hali ilikuwa mbaya Sana 2013 hadi tukachaana Baada ya matusi mazito Sana kisa nilishindwa kumchangia nauli ya kurudi Dar kwa ajili ya mahafali, yeye kwao makambako Mimi Njombe, baada ya kuachana hatukuwahi kuonana Tena sababu alisema hata nikimuona nisije mfuata atanimwagia mkojo.

Imepita miaka mingi mwaka huu nimekutana naye Mbeya soko la Mwanjelwa, nilimuona ikabidi nimshitue Kwa sababu najiamini sana Kwa sasa, Cha ajabu alikuwa myenyekevu Sana na kiufupi anajaribu kulinda uzuri wake ila ndio hiivyo hana pesa na kilomita zilishasoma tulibadilishana namba basi huo ndio mwanzo wa mawasiliano yetu.

The good thing, wiki nzima nilikuwepo Mbeya nakoboa mpunga Kwa ajili ya kupeleka Zambia, ilibidi siku moja niombe appointment aje ninapolala, aisee demu alikuja sikuwa na mzuka wa kumla tena, tukawa tunapiga stori za maisha na nini kimetokea kipindi hicho chote.

Demu anakiri alisikia msiba wa baba yangu ila aliona noma kuja kwa sababu tuliachana Kwa matusi yake, mara ananiambia anajuta sana amekubali kuwa single mother na maisha yake yameharibika, kuhusu ajira anadai degree yake ya sociology haijampatia Ajira so anajishikiza kwenye tasisi flani ya fedha inayotoa mikopo pendwa inayoharibu maisha ya watu kwa ukubwa wa riba na yeye ni mkusanyaji madeni huko analipwa Kwa commission.
Kikubwa zaidi alinishtua aliponionyesha picha ya cheti cha mwanae jina la kwanza ni jina Langu, nilipomuliza ilikuwaje anadai alikuja kugundua nilikuwa na upendo wa kweli kwake na tangu tulipoachana alikutana na wahuni tu hata baba mwenye mtoto ni mhuni tu alikuja gundua mwamba ana familia na watoto kibao.

Hakuwahi Lea mimba Wala mtoto, so alipozaa aliona ampe tu jina langu kama kunienzi, nilipomwambia nina watoto wawili na naenda kupata mtoto mwingine anadai yeye Kwa Sasa anataka apate mtoto mwingine ila hajaona mwanaume (sikujibu swala la kupata mtoto (kama vile pm alivyokimya swala bandari, najua huu ni mtego nijichanganye nianze kupasha kiporo akishika mimba nijiandae kulea na Mimi sipo tayari), I wish nimsikilizishe old nyimbo ya man'dojo na domokaya ft jide nikupe nini
 
Last edited:
Wewe hilo jina sio la kwako ulipewa tu kama ambavyo mwanae amepewa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom