SoC01 Namna bora na ya kisasa kupambana na janga la moto

Stories of Change - 2021 Competition

JJoh

New Member
Sep 1, 2012
1
0
SEKTA: MAENDELEO NA TEKNOLOJIA

Historia Fupi yakweli:


Mnamo Sept 6 2017 saa 6 kasoro mchana, Mimi mwandishi nilipata janga la moto. Ilikuwa ni safari ya Dar Es Salam kwenda Arusha kwa basi la kampuni ya “LIM SAFARI’S” lilishika moto eneo la MANGA. Uhalisia moto ulianza mdogo sana lakini kukosekana kwa “KIZIMA MOTO” kwenye gari hilo napia kwenye mabasi mengine yaliyokuwa yanapita ilipelekea gari kuteketea kabisa. Nilipotelewa na Vyeti na mali zingine nawengine walipotelewa na mizigo yao mingi yathamani hadi zaidi ya mil 20.

Hichi kisa ndicho kilinifanya niwaze na kufanya utafiti wa njia bora, rahisi, yaharaka na nayakisasa yakupambana na moto. Fuatana nami kujua maendeleo haya ya namna yakuzima moto kama patatokea janga la moto

JANGA LA MOTO NI NINI?

Ni mabadiliko ya kikemikali ambayo hutoa joto na mwanga na kisha kufwatana na moto yote haya yanatokea hasa pale dutu inayowaka itapata oksidi nachanzo cha moto. Majanga yamekuwa yakirekodiwa kuwa mengi nakuleta hasara nyingi lakini ukifwatilia kiundani wengi watasema "Ule moto ulianza mdogo sana kama mamlaka husika wangewahi usingefika huku".

Je ni kweli mamlaka za Uzimaji moto ndo taasisi zakwanza kushughulikia majanga haya. Jibu ni hapana. Kwa waliopitia migodini na sekta nyingine kuna kitu kinaitwa "USALAMA UNAANZIA KWANGU". Wewe kama mfanyabiashara, mwenye nyumba, mwenye gari na wengi huwa mnajua au mnachukua hatua gani pale unaposikia janga la moto linaweza kutokea.

Wengi watakwambia janga lamoto uwe na kizima moto (Fire Extinguisher) ndani, au kwenye gari lako au mahala punapokuwepo. Nikweli kizima moto kinasaidia sana lakini kwanini majanga ya moto mengi yakitokea yanaleta maafa na simanzi kubwa kwa walengwa? Jibu ni yawezekana wengi hawana Elimu yakuvitumia hivi vifaa nakupelekea moto kusambaa kwa haraka. Lakini turudi nyuma, mfano wa janga la moto Soko la Kariakoo utahusisha na mtu kutokujua matumizi ya Kizima Moto? Jibu ni hapana, tatizo limetokea muda wa Usiku ambapo wengi wao hawakuwepo eneo la tukio.

Hapa tunagundua janga la moto siyo kujua tu kutumia Kizima moto au Taasisi husika kuwahi kuzima moto bali palihitajika teknolojia mpya yakukabiliana na janga hilo la moto hususani pale moto unapoanza hata kama haupo eneo la tukio. Basi Mwandishi katika kupita pita kwangu nakufanya uchunguzi kwenye teknolojia ya leo niligundua Kizima moto kipya chenye usalama na chaharaka katika kupambana na moto. Kuna kampuni kadhaa sasa zimekuja na kifaa kinaitwa "KIKANDAMIZI MOTO" ambacho husaidia kuzima moto bila ya wewe kuwapo eneo la tukio lakini pia unaweza kurumia ukiwa eneo latukio, moja ya kampuni hizo ni ELIDE FIRE BALLS USA Corp.

KUHUSU TEKNOLOJIA HII YA KIKANDAMIZI MOTO (ELIDE FIRE BALLS).


Ni mfano wa mipira ya plastiki yenye uzito tofauti tofauti ambayo ndani yake inakuwa imebeba kemikali maalumu ya kuzuia moto, poda kavu na michanganyiko mingine. Mipira hii ipo mpaka ya uzito wa kilogramu 1.3 (1.3kg) ambayo ni rahisi kuwekwa mahala popote au kubebwa kirahisi kwenda popote.
download.jpg
Source: ElideFire® - The Product

MATUMIZI

Hii teknologia ni rahisi kutumia kwasababu inajigawanya kwenye aina kuu mbili ambazo ni kwenye moto ulio hai (ACTIVE USE) na ile isiyo hai (PASSIVE USE).

MOTO ULIO HAI:
Hapa tunaangazia endapo moto umeshawaka na hauwezi tena kwenda karibu kuzima na maji au vizuizi vingine wewe utachokifanya nikuutupia KIKANDAMIZI MOTO (ELIDE BALL) kwenye moto unaowaka na ndani ya sekunde tu moto ule utazimwa kabisa.
Elide-Fire-ball-fireball-Fire-Extinguisher-Auto-10.jpg
MOTO USIO HAI: Hapa ndoinatupa picha ya ule moto wa kariakoo na kwingine, kwani hii mipira huwa inajiamsha yenyewe bila wewe kuwapo eneo la tukio (self-activating fire balls). Utachopaswa kufanya nikufunga mpira wako eneo unalohisi lipo na hatari yakutokea moto. Pale moto utapoanza hii mipira ina teknologia yakuakisi moto nakulipuka kuachia mchanganyiko wa kemikali nakuzima moto kabisa kabla yakuwa mkubwa. Hapa utazungumzia magari, nyumbani, madukani na popote. mfano kwenye gari utafunga kwenye injini.
Fire-Protection-ElideFire-3.jpg


AINA YA MOTO INAYOWEZA KUZIMWA KWA TEKNOLOJIA HII

Hii teknologia huzima madaraja yote ya moto kulinganisha na ukubwa wa janga lenye. Hapa chini ni madaraja yanayoweza kuzimwa kwa hii teknolojia

  • Daraja A - moto utokanao na mbao kavu, makaratasi, vitambaa.....nk)
  • Daraja B -moto utokanao na mafuta kama vile vimiminika vya mlipuko (petrol, dizeli),plastiki...nk
  • Daraja C - moto utokanao na gesi
  • Daraja E - moto utokanao na umeme
  • Daraja F - moto utokanao na mafuta yakupikia
FAIDA ZA HII TEKNOLOJIA

Rahisi kutumia

Haina gharama za kwenda kujifunza wala haina matumizi yakuondoa pini kwanza.

Uzito mdogo
Mpira una kipenyo cha milimita 152 na uzito juu ukiwa kilo 1.3 hii hufanya iwe nyepesi na rahisi kuhifadhi popote.

Hujiamsha yenyewe hatari inapotokea (Auto-activation)
Mpira hujiamsha wenyewe ndani ya sekunde 3 inapoakisi moto na kulipuka kuachia kemikali ambazo zitapelekea moto kuzima kabisa.

Inaongeza usalama wa mtumiaji
Huna haja yakwenda karibu na chanzo cha moto au kuwapo kwenye eneo la tukio.

Inaendana na mazingira yeyote
Utengenezwaji wake unaruhusu kuweka popote hata kuning’iniza ukutani au kuweka juu ya meza kwenye sapoti yake.

Hamna gharama za matengenezo.
Hii bidhaa inadumundani ya miaka mitano bila ya kufanyia ukaguzi au matengenezo yeyote.

Pia unaweza kuangalia vidio ya namna ya matumizi na ufanyaji kazi wa teknolojia hii kupitia youtube
 
Back
Top Bottom