Naliona anguko la Kibanda

Naliona anguko la Kibanda

Kesho Jumatano katika Tanzania Daima nimeandika sehemu ya pili ya makala hiyo. Kwanza nimemuomba radhi Sitta na Watanzania kwa lugha kali niliyotumia dhidi yake na dhidi ya Watanzania wenzangu. Naamini katika kukosoana. Nimekiri mapungufu katika maandishi yangu. Hata hivyo nimesisitiza msimamo wangu kuhusu Sitta uko pale pale. Nimejaribu kutumia lugha ya staha kueleza kile ninachoamini kuhusu sakata la Dowans na vitanzi tulivyojifunga

Kibanda to be honest wengi hatujapendezwa na makala yako, si kwamba hatuna uwezo wa kuchambua mambo. Kwanza uliandika kwa hasira na kuonyesha kuwa ni wewe tu ndio mwenye mtazamo sahihi kiasi cha kusema wote wanaomuunga mkono Sitta ni mazuzu(ingawa hukutumia neno zuzu).

Katika makala yako, tofauti kabisa na makala za wapambanaji wengi unaonekana kabisa kutokuchukizwa na malipo ya dowans bali wanaopinga ndio hutaki hata kuwasikia. Hiyo imewapa wasiwasi watu wengi sana wanaofuatilia makala zako na especially ile ya jumatano.

To me naona TZ Daima polepole limeanza kuchukua direction tofauti kidogo na hasa makala zako, ushauri wangu kwako ni kuwa jitathmini upo wapi kwa sasa vinginevyo ukiendelea hivi hilo gazeti la TZ Daima hasa la j5 tutaliweka pembeni tutaendelea na Mwanahalisi na Raia Mwema. Don't say i didn't warn you!

Kwa hiyo umesoma issue ya kwanza na ya pili ya UMOJA halafu unaandika uongo hapa kwamba kwenye jarida hilo kuna utetezi kwa mafisadi. Ama kweli tunajenga taifa la hatari la watu wasomi wazushi. Hebu waandikie wasomaji humu ukitoa ushahidi wa hilo ulilosema.
Pole sana Kibanda! Umesahau kitu kimoja... Kusoma ni jambo moja na kuelewa ni jambo jengine! Baadhi ya wasomi wetu wa kileo, upeo wao ni mdogo sana, kwa sababu wao wanataka kuamini kile walichokwishaamini hivyo basi anaweza kusoma paragraph moja tu, akahitimisha habari nzima na kutoa hukumu zake. Hapo ndipo wanapozusha na hawaambiliki!!

Hivi kama wao ni wakweli na wana-kumbukumbu basi watuambie ni KWANINI MWALIMU ALIKUWA HAMTAKI SS? Na kama SS si mbinafsi na mwenye kupenda kujitenga alikuwamo katika G55!! Na kama kweli yeye SS ni mwenye uchungu na nchi na hana uchu wa madaraka na kupenda sifa KWANINI JENGO LA SPIKA LIJENGWE JIMBONI MWAKE NA SI DODOMA ina maana alitaka USPIKA - UKAMUZU BANDA!?)

Leo sitochangia hadi nihisome makala hiyo ya pili, Cha msingi KIBANDA simamia msimamo wako na wadau mnao amini kuwa KIBANDA kanunuliwa na mafisadi tunaomba ushahidi. KIBANDA ni member humu JF hivyo mkitoa ushahidi tutasubiri utetezi wake na kisha tutachambua mchele ni hupi na chuya ni zipi.

Nakushukuru kwa uvumilivu wako na kwa uzito wa maelezo yako. Nilikaribia kuiweka hapa lakini nimeogopa kuwakera wengi kwa uurefu wake

Sitta si safi na kama safi angeruhusu mjadala wa Richmond uendelee mpaka kuparta muafaka bungeni na kwa hesabu tu marupurupu ya Spika yanazidi ya Uwaziri alionao ndo maana anakurupuka.
Sikatai anasema jambo jema lakini wasiwasi wetu wananchi ni kwamba hizi ni hasira za kuukosa uspika.
Kama safi ahame chama maana kinanuka
Thubutu... afanyeje??? Kule ndiko anakojua kwamba angalau angali na chochote na anaheshimika labda hamumjui mzee yule! Ulizeni wanaojaribu kugombea nae ubunge kule jimboni kwake mtapata habari zake. Mnadhani jimboni kwake wanamtaka! Ila wale wapinzani halisi huwa anawawahi kimtindo wa kutumia dola biashara inaisha anabaki na mngombea dhaifu. Akitoka huko na kuja mjengoni anaonekana shujaa! Lakini kwa akili zetu wacha na tumuone shujaa kwa muda, wakati utafika kila ukweli utajulikana... kama mjuavyo media zikikubeba utaonekana na siku zikikuacha ndio mporomoko na mengineyo yanajulikana

Nakushukuru kwa uvumilivu wako na kwa uzito wa maelezo yako. Nilikaribia kuiweka hapa lakini nimeogopa kuwakera wengi kwa uurefu wake
Mkuu, Kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni yake na hatoi maoni kwa sababu ya kumfurahisha mtu bali kutoa ukweli uliomo ndani ya nafsi yake. Mzigo wa moyo hautuliwi kwa kuwafurahisha watu, Koti la mfalme likiwa na mawaa aambiwe... ili asiaibike. Lakini tukitaka kufurahishana (si ni heri tununuliane chai na vitafinwa) sio katika mambo na mustakabali wa Nchi. Hii ni Nchi yetu sote lazime tuwe na muono tofauti ili tupate kilicho bora. Tukiwa na mawazo ya aina moja basi itakuwa Nchi ya wendawazimu na tusio na fikra bali kufatana kama mchwa hata kama tunatumbukia mtoni!!

Usife moyo, UKWELI SIKU ZOTE HAUTAKIWI KWA MAANA NI MCHUNGU, BALI UONGO HUTHAMINIWA KWA MAANA UNAFURAHISHA MIOYO!

Kama nilivyochangia kule kwenye thread ya hoja kwenda kwa Balile wa Mtanzania, mathinkers wengi humu tunaelekea kuwa mediocres-hatusomi.Mwandishi anafanya kitu ambacho watanzania wengi na hata wachambuzi makini wameshindwa kukifanya. Kibanda amekuwa akindika kila wiki kwa takribani mwezi sasa katika Tanzania Daima la Jumatano kumkashifu Sitta na akionekana kuchekelea zigo la mabilioni wanayotakiwa kulipwa Dowans. Kibanda amekuwa akichekelea lakini kwa ujanja ambao si wake, amekuwa akisukuma zigo hilo eti ni lawama kwa Sitta na Bunge lake lililozikataa Richmond na Dowans.

Balile amekuwa akiandika upuuzi huo na hakuna wa kumjibu, mathinker wanapotumia jukwaa hili kujibu kwa hoja sadifu, mathinker wanaotakiwa kusoma wanaishi aya ya kwanza na kuanza kulaumu, kama si ujinga wa kweli, basi nadhani kuna watu wanahujumu hili jukwaa kwa kuanzisha mada za kupuuza michango yenye nguvu matokeo yake jukwaa hili litakosa maana.

Bro/sister kama ndio great thinkers tumekwisha. Wape pole.

Everyday, now & then, we said here JF, most journalists including this one, are stupid, waganga njaa, illeterate, arrogant & ignorant too,
it doesn't matter how long he has been writting articles, he thinks using his foolish, idiot mind can convince or persuade all of us kwa issue
ya UWIZI MKUBWA wa wazi kama wa DOWANS, as i said ni ujinga wake unamsumbua, he is dirty to discuss him, Prostitution of journalism, hana lolote
hana uzalendo ( Patriotism)
Kabanda, Balile, Kibonde deserve a place in CCM's propaganda newspaper Uhuru and not progressive and highly respected papers like Tanzania Daima.
Hawa ni waandishi wajinga, waganga njaa ambao muda si mrefu sana wataaibishwa na matendo yao dhidi ya umma wa watanzania. Ama sasa nimeamini methali ya kiingereza isemayo 'a hungry stomach knows no discipline'' Ndiyo maana tunawashuhudia sasa waandishi hawa na wengine tuliodhani wana weledi kununuliwa kwa bei poa kulingana na saizi ya njaa katika matumbo yao! Ni nani alimtazamia Salva Rweyemamu kuangukia ikulu kwenye lambalamba ya 'Sultani' Kikwete? Historia itawahukumu.

Kama kweli kibanda umesema ivo,ebu piga moyo konde. Mi namheshimu sana mzee6.

Safi sana Mkembe 2010! Umechambua vizuri makala ya Kibanda na ni ukweli mtupu! Nadhani wako wengi wameahidiwa na hao mafisadi tunda la mtu wa kati ukiachia Kibanda na Fungamtama ili Dowans ilipwe! Ninachotaka kuwakumbusha hao waahidiwa na ambao tayari wameshafungasha mtama wao kibindoni waangalie kitu kimoja, upande huo waliopo (wa mafisadi) ni waovu na wako tayari kupoteza reputations zao ili mradi hela ipatikane, kwahiyo kama na wao wako tayari historia iwakumbukwe kwa hayo basi waendelee ila sisi wananchi (wajinga na vipofu) hatutakubali na tutambana mpaka dakika ya mwisho!!

Wakuu siwezi kuwasemea wengine, lakini yeyote aliyesoma mada yote na michango yote anabakia na kiu ya makala ya kesho. Tunawaomba walioko nchini na wenye uwezo watuletee hapa kesho tena yote nzima. Kuna kitu nahisi kinafichwa kwa ustadi mkubwa. Msisahau humu tuko wengi na wenye fani mbali mbali licha ya tofauti za umri na "level of exposure". Msomi hafichwi maana kama lugha anaijua.

Naamini Jamiiforums ni Home of Great Thinkers sasa hawa ndugu zangu akina informer na wengine ni kwa nini wanashusha tuhuma nyingi wasizo na uhakika nazo. Mimi ndiye Absalom Kibanda. Nimekuwa Mhariri wa Tanzania Daima huu ni mwaka wa nne na ninaelekea wa tano. Msimamo wangu kuhusu mambo kadha wa kadha haujabadilika.

Kila mtu ana uhuru wa kufikiri anavyotaka. Niweke kumbukumbu sawasawa. Sina sababu hata moja ya kununuliwa na mtu yeyote. Rostam Aziz amekuwa mkurugenzi wangu Mwananchi na nikaacha kazi kinyume cha matakwa yake. Ninaamini katika mabadiliko. Nimeanza kumpinga Sitta kila anapofanya mambo ambayo sikubaliani nayo tangu akiwa spika na hata kabla Lowassa hajajiuzulu.

Nikiwa mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima ninatoa uhuru kwa viongozi wote pasipo kujali misimamo yao kutoa maoni yao. Nimeruhusu mijadala ya kina kupitia Tanzania Daima kutoka pande zote mbili. Kwangu mimi Rostam, Sitta, Lowassa, Chenge, Mwakyembe na wengine wote ni vyanzo muhimu vya habari na kwa Tanzania Daima wana nafasi sawa kihabari. Msimamo wangu huo uko bayana na kimsingi hili ndilo gazeti linalokimbiliwa na kila mtu, hatufungamani na upande wowote zaidi ya kupigania mabadiliko. Ninapata furaha nisikiapo nikituhumiwa kuwa wakala wa Chadema, mara wakala wa CUF, mara wakala wa mafisadi, mara wakala wa Kikwete kwa sababu ya msimamo huru wa mawazo.

Nilikataa tangu mapema kujiingiza katika vita ya ufisadi inayopiganwa na akina Sitta na akina Mwakyembe kwa sababu nimejiridhidhs kwamba ni vita ya kitapeli na yenye malengo ya kisiasa zaidi kuliko kihalisia. Naamini na hili nimekuwa nikiliandika katika safu yangu ya Tuendako kuwa ufisadi uliopo nchini unakigusa Chama Cha Mapinduzi moja kwa moja. Kwa hiyo hakuna anayeweza kumnyoshea mwenzake kidole. Viongozi wote wa juu wa chama hicho tawala wakianzia na mwenyekiti wao wa taifa hawana ubavu wa kukwepa tuhuma halisi za chama chao kuhusika katika ufisadi.

Hiyo ndiyo dhambi yangu iliyonikosanisha na wengi katika taaluma. Nimekataa kuingia katika mkumbo wa kujifanya mwanaharakati na jemedari wa ufisadi kwa kuwa naamini ni unafiki. Ni jambo la kheri kwamba wamiliki wa Tanzania Daima wanathamini mchango wangu, wanaufahamu na kuuamini msimamo wangu, wanaujua uzushi wa kila siku wa akina informer ambao wao wanalipwa mamilioni ya fedha kuwachafua akina Lowassa kwa sababu ambazo mimi ninazijua na ushahidi upo.

Acha nihukumiwe kwa haki huku nikiwa na uhakika kuwa ipo siku historia itanitetea
Kibanda kuna kitu kinaitwa jf public opinion kwenye issues mbali mbali. Ukitofautiana na public opinion hizi tegemea matukano.

Kuhusu Sitta ile siku anahitimisha mjadala wa Richmond pale Dodoma kwa mtindo wa fumika kombe, nilitoa maoni yangu humu na nilishambuliwa.

Juzi baada ya hukumu ya ICC nilitoa maoni kuhusu mkataba ile ulivyo mbovu tumeshikwa pabaya. Nikasema kauli za Sitta na Mwakiembe ni furahisha genge. Wakunishukia walinishukia.

Kwa upande wangu nakukubali japo kuna pengi natofautiana na wewe na wengi kuhusu baadhi ya issues zikiwemo zihusuzo Chadema.

Kwanza kabisa nampongeza mkuu mkembe kwa analysis yake nzuri, hata kama ilishajadiliwa but yeye ameipresent kivingine and bcaz we are great thinkers hatuchoki kujadili hot topics kama hizi..!

Mwisho kabisa niseme tu huyu bwana ametuchosha..! hamna ubishi ameshachakachuliwa tena to the maximum, sioni sababu ya kamanda mbowe kuendelea kumkip this chap, hata kama alisema nini bila kutetereka against Jk he is nat da same chap nowdays!

I THINKS ITS A HIGH TIME NOW HE DECIDES IF HE IS WITH US OR AGAINST US ILI TUJUE ASIJIDAI YE NI MTU WA KATI WKT UPANDE WAKE UNJIDHIHIRISHA...! SO KAMA ATAENDELEA KUBAKI TANZANIA DAIMA AACHE KUANDIKA UOZO WAKE ATHER WISE AHAMIE UHURU AMA RAI..!:frusty:

KIBANDA KWA HILI TUKO PAMOJA ! sema tu, nimekuelewa na ninatayarisha nakala ya kutetea na kuuelewesha umma unamaanisha nini! just simple logic is needed!

Kibanda ni yule nilimfahamu chuo kikuu cha dsm aliyemaliza 1994 au mwingine. Maaana sitegemei kama anaweza kuwatetea mafisadi

Everyday, now & then, we said here JF, most journalists including this one, are stupid, waganga njaa, illeterate, arrogant & ignorant too,
it doesn't matter how long he has been writting articles, he thinks using his foolish, idiot mind can convince or persuade all of us kwa issue
ya UWIZI MKUBWA wa wazi kama wa DOWANS, as i said ni ujinga wake unamsumbua, he is dirty to discuss him, Prostitution of journalism, hana lolote
hana uzalendo ( Patriotism)

Acha uvivu kipindupindu. Hoja zimepangwa na zinaeleweka vyema. Namuunga mkonn kuwa Kibanda ameanza kutumiwa na mafisadi. And they pay him good ndo maana anakubali kuharibu reputation yake but aonekane mzuri kwa kina EL+RA.

Hicho kibanda kimeshaungua kimenunuliwa zamani sana na hao Mafisi kumbe hamjui!! tatizo hawafanyi tathimini kama wakifanya tathimini hilo gazeti limepungua wasomaji kwa asilimia zaidi ya kumi tokea hicho kibanda kiungua na moto wa pesa za Rushwa.

KIBANDA KWA HILI TUKO PAMOJA ! sema tu, nimekuelewa na ninatayarisha nakala ya kutetea na kuuelewesha umma unamaanisha nini! just simple logic is needed!

Tunasubiri makala yako bwana wakili a.k.a mtetezi wa wanyonge.

Hapa tunahitaji facts sio utetezi.

Back
Top Bottom