Naliona anguko la Kibanda

Kaka yangu ABSALOM KIBANDA ni mwandishi na mhariri mahiri ambaye kwa muda mrefu nimekuwa nikiifurahia kazi yake kwa uwezo wake wa kuandika makala moto moto na uchambuzi wake mahiri. Haikunishangaza pale alipopewa kazi ya kuvaa viatu alivyokuwa anapewa kazi ya kuvaa viatu vilivyokuwa vimeachwa na Deadatus Balile pale alipokuwa amefadhiliwa kwenda kusoma huko Hull.

Lakini dalili za Kibanda kubadili mwelekeo zilianza takribani miaka miwili iliyopita pale alipoanza mkondo wa kutumika kupigana vita vya kihasimu vilivyokuwepo ndani ya CCM huku akijikita zaidi kuwabeza na kuwakebehi wale walioonekana kukosoa vitendo vya kifisadi. Majukumu mapya ya Kibanda yamedhihirika zaidi baada ya uchaguzi uliopita ambapo yeye na gazeti lake la Tanzania Daima limegeuka kama mdomo mahususi wa mafisadi katika kutoa matamko mbalimbali ambayo nia yake ni kujaribu kumsafisha yule waliyemteua kurithi mikoba ya rais JK. Amekuwa akiendesha harakati hizo kwa kuendesha mahojiano na Lowassa na washirika wake, na hata kumwaga sifa kwake na hata ushabiki wa wazi waliouonyesha katika kuunga mkono malipo ya Dowans. Nakumbuka mahojiano kati ya Hapiness Katabazi na wakili wa Dowans Kennedy Fungamtama, akimpamba kwamba ni mmoja wa watu walioisoma hukumu hiyo kwa zaidi ya mara saba. Makala ile ilikuwa ikisisitiza kwa nini serikali ni lazima iridhie malipo ya Dowans. Taarifa zisizo rasmi zinasema kwamba gharama za uchapaji wa gazeti la Tanzania Daima zinalipwa na Lowassa na mafisadi wenzake na malipo hayo hufanywa kwa Kibanda ijapokuwa Freeman Mbowe amekuwa bado akitoa fedha za kuendeshea gazeti hilo, ikimaanisha kwamba fedha za mafisadi zinaingia kwa Kibanda moja kwa moja.

Lakini Kibanda hakuishia hapo, sasa ame-graduate na kujitambulisha kama JIK ya kujaribu kuondoa madoa sugu katika mwili wa mafisadi na hasa kinara wao EL. Kwa ufadhili wa mafisadi hao na hasa EL na RA limeanzishwa jarida la UMOJA ambalo tayari limeashaingia mitaani, likijifanya kuinadi Chadema lakini mpango mpana ukiwa ni kulifanya jarida hilo kuwa ni maliwato maalum ya kumsafisha mkubwa huyu ili mwakani aukwae uenyekiti wa CCM na baadae kuingia ikulu 2015. Gazeti hili ambalo wamiliki wanaotajwa humo ni Absalom Kibanda na wakili Masatu Makaki, linaendesha shughuli zake kutokea mikocheni ambako wamelipiwa kodi ya ofisi ya kifahari kwa miaka kadhaa ijayo na kwa kusaidiana na Charles Mullinda, wako katika harakati za kuligeuza kuwa gazeti la kila siku ambalo kwa kushirikiana na magazeti ya Rai na Mtanzania, yatakuwa yanaendesha mradi huu wa kumtakasa EL na genge lake na kujenga mazingira ya kuchagulika. Mpango huu kabambe umekamilishwa sambamba na kununuliwa kwa kituo cha redio cha Radia 5 cha Arusha na kuanzishwa kwa kituo cha TV ambacho kiko mbioni kuanza matangazo hivi karibuni.

Wakati Mbowe amesikika kutaka kuchukua hatua za kumuondoa Kibanda pamoja na Mullinda, ukweli unabaki kwamba KIBANDA ameamua kujirahisisha na kwa tamaa ya fedha kukubali kugeuka sabuni ya aina ya JIK na kuichimbia kaburi taaluma yake na weledi alioujenga kwa miaka kadhaa wa kadhaa. Ameingia kwenye mtego ulionasa wenzake akina Muhingo Rweyemamu, Salva Rweyemamu, Deodatus Balile, Dr. Gidion Shoo, Manyerere Jackton, Theophil Makunga na wengine wengi.

Swali ni kwamba je, ni nani sasa amebaki katika tasnia hii ya habari? Labda Kubenea! Ama kweli ufisadi unatujeruhi watanzania!
 
Banyimwa kweli umechimba. Mimi ilikuwa mpenzi mkubwa sana wa gazeti hili lakini ghafla limehama kutoka kuwa gazeti makini lililosheheni hoja na sasa limegeuka gazeti la kupima upepo wa watanzania kuhusu hisia zao kwa mafisadi. Hili Jarida jipya lilinishtua kidogo nilipoliona na jinsi lilivyojaza makala ya kumpamba EL. Lakini haya mahusiano ya Kibanda na Makaki ni ya kushangaza na sasa naelewa kwamba ndani ya jarida hili kuna mafisadi kwani Makaki mara zote huwa anawakilisha fisadi mmoja ambaye utajiri wake umetokana na madili ya EPA pale Benki Kuu. Kweli mtandao huu ni mpana.
 
Kibanda siyo kama alimaliza UDSM 1994, bali ni Juni 1995 na akagraduate November 1995. Nilisoma naye kwa miaka yote minne aliyokuwa akisomea shahada yake ya kwanza. Ni mwalimu kwa taaluma. Sasa huku kwenye uandishi wa habari sijui aliingiaingiaje kwa sababu alisoma ili awe mwalimu wa shule za sekondari.

Ni mchambuzi mzuri wa issues hata akiwa UDSM, na ni mtu asiyeburuzwa hovyo. Ana msimamo, labda kwa wale wasiomwelewa ndio watakaomwona kama amenunuliwa na mafisadi. Msimamo wake waulizeni wakuu wa Kitivo cha Elimu wa miaka ya 1992 - 1995, UDSM; wanamfahamu.
 
Hizi thread za kujadili watu zinaonyesha uwezo wa kufikiri unapungua na ni hatari tukianzisha thread za kijinga jinga kama hizi maana hazina faida kwa jamii.
Masatu sasa na wewe waanza kufulia.

Sijaelewa kabisa what are we trying to think here. Nimeachwa trafic light, Lakini napita tu.:israel:
 
Hivi huyu Kibanda ni mtu wa Mbeya? Hilo Absalom linaonyesha kama huyu ni wa huku kwetu.

Lakini mbona anaongea mbofu mbofu sana kulinda boss wake. Watu wa Mbeya huwa hawajikombi kwa maboss.

Itabidi tumwitie wazee wamkanye.

This is really interesting now.......
 
CDLv3-kUgAAx_0j.jpg
 
Back
Top Bottom