Naliona anguko la Kibanda

Naliona anguko la Kibanda

Everyday, now & then, we said here JF, most journalists including this one, are stupid, waganga njaa, illeterate, arrogant & ignorant too,
it doesn't matter how long he has been writting articles, he thinks using his foolish, idiot mind can convince or persuade all of us kwa issue
ya UWIZI MKUBWA wa wazi kama wa DOWANS, as i said ni ujinga wake unamsumbua, he is dirty to discuss him, Prostitution of journalism, hana lolote
hana uzalendo ( Patriotism)
 
Kuna Mzungu mmoja alishawahi sema kuwa ukitaka kumwibia au kumtia mtu mweusi matatani basi uweke mambo kwenye maandishi maana wana uvivu wa kusoma wanapenda vitu vya mkato visivyohitaji kutumia akili na kutafakari. Nikiangalia comments za watu hapa ina-justfy usemi huo. Watu wengi wanapenda ready made kutumia mda kudadasua hawataki,na hii inatokana na uvivu wa watu walio wengi kutokuwa na tabia ya kusoma vitabu. Iwe na vyuoni ni madesa tu mpaka humu kwenye JF wanaendeleza uchovu wao. Ndiyo maana hata wakuu wetu wanasaini mikataba bila hata ya kuisoma na mwishowe tunatiwa matatani. Mtu kusoma page 2 tu mchovu anataka apewe summary, kazi kweli kweli na Poleni sana.
 
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, anafanya kazi part-time kwenye magazine inayomilikiwa na Edward Lowassa inaitwa UMOJA. Pia Kibanda amekuwa anatoa habari za kumbeba Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge kwenye Tanzania Daima mara nyingi. Kwa kupokea maagizo na malipo kutoka kwa Lowassa na Rostam Aziz, Kibanda pia amekuwa akiandika habari na makala nyingi za kuwakashifu Samuel Sitta, Harisson Mwakyembe, Bernard Membe na John Magufuli.

Tanzania Daima ni moja ya magazeti yanayotumiwa na fisadi Rostam Aziz kutetea ufisadi mbalimbali, ikiwemo malipo kwa Dowans kwa nguvu zote. Wanaitumia Tanzania Daima kwa kuwa gazeti linaaminika kuwa ni huru na ni rahisi ku-brain wash watu kuliko kutumia Mtanzania/Rai ambayo Watanzania hawayasomi tena sasa baada ya kugundua kuwa yanamilikiwa na Rostam.

Cha kushangaza ni kuwa mmiliki wa Tanzania Daima, Freeman Mbowe, anaachia tu gazeti lake litumiwe na mafisadi kupitia kwa Kibanda kuangamiza nchi.
 
Mh nina wasiwasi ,mi ni msomaji wa Makala za Kibanda sioni dalili za kuchakuchuliwa!kama ndivyo basi Tnzania DAIMA YOTE!ALICHOJADILI mhariri ni kuhusu msimamo wa Sitta ,kwamba kama anajibainisha kuwa ni mpambanaji kwa nini yupo katika hilo kundi !na alisema kama yeye angekuwa ni Rais/waziri mkuu angemfukuza kazi,Kumbukeni anasema aangekuwa ni Kikwete au Pinda na kwa mazingira ya leo!Nani asiye jua kuwa watu wadilifu wanapoona wameingia sehemu isiyofaa hutoka haraka.inawezekana bwana mhariri anlitumia lugha kali !lakini ujumbe wake ni muafaka.Kumbekeni ni mojawapo wa waandishi aliyesimama thabiti kwa uwazi na hakutetereka kuonesha kuwa Kiwete alaikuwa anapewa sifa asizo stahili na alionesha kutofaa kwake kuwa mkuu wetu!aliyoondika leo kuna mtu atayabishia !
 
cha msingi sitta ni mtu safi lakini yuko katika chama kibaya
 
Sitta kasema hakuna baraza la mawaziri lililokaa na kuamua dowans alipwe, asa collective responsibility ipo wapi hapa? utamfukuzaje waziri alietoa maoni yake? Absolom kachemka, inaelekea kweli yupo ndani ya payroll ya Rostam, yeye ndo anafaa atimuliwe Tanzania Daima.
 
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, anafanya kazi part-time kwenye magazine inayomilikiwa na Edward Lowassa inaitwa UMOJA. Pia Kibanda amekuwa anatoa habari za kumbeba Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge kwenye Tanzania Daima mara nyingi. Kwa kupokea maagizo na malipo kutoka kwa Lowassa na Rostam Aziz, Kibanda pia amekuwa akiandika habari na makala nyingi za kuwakashifu Samuel Sitta, Harisson Mwakyembe, Bernard Membe na John Magufuli.

Tanzania Daima ni moja ya magazeti yanayotumiwa na fisadi Rostam Aziz kutetea ufisadi mbalimbali, ikiwemo malipo kwa Dowans kwa nguvu zote. Wanaitumia Tanzania Daima kwa kuwa gazeti linaaminika kuwa ni huru na ni rahisi ku-brain wash watu kuliko kutumia Mtanzania/Rai ambayo Watanzania hawayasomi tena sasa baada ya kugundua kuwa yanamilikiwa na Rostam.

Cha kushangaza ni kuwa mmiliki wa Tanzania Daima, Freeman Mbowe, anaachia tu gazeti lake litumiwe na mafisadi kupitia kwa Kibanda kuangamiza nchi.

Kibanda ameshapotea njia muda mrefu,

siku hizi amekuwa mpiga filimbi wa Lowasa, Rostam, Karamagi & co. wakati huo huo yuko busy kuwakashifu na kuwaandika vibaya Mzee Sita , Mwakyembe & co.

Kama Mmmiliki wa tanzania daima hatochukua hatua za haraka na za makusudi kumuondoa kibanda(sijui ni cha nyasi ama makuti) basi ajue kwamba tanzania daima litaanza kupoteza wasomaji na kubakia kama magazeti ya fisadi "habari corp".

Vinginevyo basi na yeye atakuwa amejiandaa kutoa ruzuku kwa ajili ya uendeshaji wa gazeti lake litakavyokosa soko na kudoda vibandani.
 
Mhariri anakuwaje msemaji wa watanzania? Mtu kuwa muandishi wa habari haikupi mamlaka ya kuwa muamuzi kwa niaba ya wengine. Kibanda amekosea kumshambulia Sitta.

Kuhusu wachangiaji wanaolalamika kuhusu mada kuwa ndefu kuna mada fupi kwenye forum ya 'jokes'. Pia kuna mada zinazovutia kwenye forum ya 'mapenzi'.
 
Sakata la Absolom Kibanda na Samuel Sitta

Dowans yawa ‘tunda la katikati’
la kujua mema na mabaya!


Na Simon Mhina



Sakata la kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond na baadaye Dowans, ambalo linaelezwa kuwa ni vita baina ya wananchi wengi wanyonge na kundi la wanyonyaji wachache, limetoa funzo kubwa kwa mustakabali wa taifa letu.
Funzo kubwa lililotokana na mjadala huo, ni kujua yupi yuko upande upi na kwa maslahi yepi!
Ni sakata gumu la kufa na kupona, ambalo limefanya mashetani waonekane malaika, na Malaika watakatifu wang’arao waitwe mashetani tena waasi.
Katika sakata hilo, tumeshuhudia wananchi wanyonge wanaolazimika kutembea kwa miguu kutokana na kukosa Sh. 250 ya nauli ya kukweka daladala, wakiitwa wajinga kwa vile wamepaza sauti zao wakipinga kukamuliwa Bilioni 94, ili wanyonyaji hao wachache walipwe.
Jumatano iliyopita siku ya kusherehekea Mapinduzi ‘matukufu’ ya Zanzibar, ni sku ambayo binafsi siwezi kuisahau maishani mwangu, kwani nilisoma makala iliyoandikwa na mwanahabari mwenzangu Absolom Kibanda ambaye ni Mhariri wa gazeti nilipendalo la Tanzania Daima, ambaye alisema aliyekuwa Spika wa Bunge lililopita Samuel Sitta ni muasi, dhaifu asiyefaa kuongoza zaidi ya watu wawili na wala asiye na uwezo wa kujiongoza hata yeye mwenyewe. Haya ni matusi!
Hapa nanukuu maneno ya Kibanda katika makala hiyo, “Kwangu mimi Sitta ni kiongozi na mwanasiasa muasi.Ni mtu asiyestahili kabisa kupewa jukumu la kuongoza watu wanaoanzia wawili, zaidi ya kujiongoza yeye binafsi. Hata hili la kujiongoza mwenyewe nina mashaka nalo”
Awali ya yote huyo anayekashifiwa hivi ni mtu ambaye ameshikilia na bado anaendelea kushikiliwa nafasi kubwa za juu serikalini, bila yeye kuandika barua ya maombi.
Mwaka 2005 Sitta alipigiwa kura na wabunge wote akawa Spika wao. Mwaka 2010, Rais wa Jamhuri ya Muungano akamteua kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Lakini Bwana mhariri anasema huyu hafai kuongoza zaidi ya watu wawili na ana mashaka kuwa hawezi hata kujiongoza mwenyewe! Ndio maana nikatanguliza kusema hayo ni matusi.
Kama Sitta ni duni kwa kiwango hicho, wabunge waliomchagua awe kiongozi wao Bwana mhariri anawaweka kwenye kundi gani?
Kama Sitta ni duni kiasi cha kushindwa kujiongoza mwenyewe, huyo Rais Kikwete aliyempa wadhifa wa uwaziri bila kuombwa, Bwana Kibanda anamuweka kwenye kundi gani? Ama kweli tunda la katikati (Dowans) Tamu!
Awali nilidhani huenda Bwana Mhariri huyo ana ugomvi binafsi na Sitta, lakini baadaye nikagundua kwamba kinachosababisha yote haya ni Dowans, ambayo imegeuka kuwa “Tunda la katikati” la kujua mema na mabaya. Nitafafanua baadaye.
Bwana mhariri wa gazeti hilo ambalo binafsi naliheshimu, hakuishia kumtusi Sitta pekee, bali akawaita wajinga watanzania walio wengi.
Naomba nimnukuu tena “ Ni wazi kwamba Sitta anafanya yote haya kwa sababu anatambua kwamba machoni mwa watanzania wengi waliowajinga, yeye ndiye shujaa wao na kwa hakika ndiye anayeonekana kuwa na jicho moja miongoni mwa vipofu wengi” Astaghafilulaaa!
Katika Makala hayo Bwana mhariri hakusita kutaja kuwa sababu za kumsema vibaya Sitta ni Dowans.
Anasema Sitta hakustahili kutoa kauli za kuashiria kukataa ‘mbinu’ za kuilipa Dowans mabilioni hayo ya Shilingi.
Anasema kitendo hicho kinaenda kinyume na uwajibikaji wa pamoja na kwamba Sitta ametoa siri za baraza za mawaziri! Bwana mhariri Kibanda, akasisitiza kwamba kuna umuhimu Waziri Mkuu amshauri Rais amfukuze Sitta.
Haya ndiyo matokeo ya tunda la katikati, ambapo baada ya Adamu na Hawa kuonjeshwa na kulila, licha ya kwamba walinogewa, lakini matokeo yake walijiukuta wako uchi!
Hawakupata kile walichoahidiwa na nyoka (kufanana na Mungu) badala yake wakatengana naye.
Awali nyoka aliwadanganya binadamu hao wa kwanza kwamba Mungu alikuwa amewakataza kwa makusudi ula tunda hilo, kwa vile alifahamu wakilionja watafanana naye.
Hata hivyo walivyoleweshwa na ushawishi wa nyoka yule na kula tunda, walijiona wako uchi tofauti na mategemeo yao kuwa wangefanana na Mungu.
Hata hivyo yule nyoka aliyemdanganya Adamu na Hawa alishakufa, lakini kwa hili la tunda la Dowans bila shaka nyoka ‘R.A’ au kwa kirefu ‘red action’ ametumika kumdanganya Bwana mhariri! Ila Bustani ya Eden iliyotumika kumdanganya inabaki kuwa siri yao (Siku hizi bustani ziko nyingi).
Nyoka amemdanganya akampa tunda, kweli amenogewa lakini matokeo yake badala ya kufanana na hicho alichoahidiwa, amebaki uchi machoni mwa watanzania, kwani bila woga amewaita wajinga na vipofu!
Kiburi cha kufanya hivyo kinatokana na yeye kujiaminisha kwamba atafanana na ‘Mungu’ kwani ndivyo alivyoambiwa na nyoka ‘RA’ kabla hajapewa tunda. Hivyo tunda likamlewesha akajikuta anawaita ‘wajinga na vipofu’ watanzania ( wakiwemo kaka na dada zake).
Nasisitiza tena Bwana mhariri huyu tunayemjua, mtu mwema, mwenye waledi, asingefikia hatua ya kutoa maneno haya ya dharau bila kudanganywa.
Aidha kutokana na kuleweshwa na tunda hilo Bwana mhariri Kibanda mtu mwenye waledi, akapotosha kwa makusudi maana halisi ya “Uwajibikaji wa Pamoja”.
Na hapa tena naomba ni mnukuu “ Kosa la tatu ambalo Sitta anapaswa kukabiliana nalo ni lle la kuwadharau wakuu wake wa kazi. Anatoa kauli kuhusu serikali kukataa kulipa Dowans wakati akijua fika kwamba Waziri Mkuu Pinda alipata kulizungumzia jambo hili na akasema iwapo mwanasheria mkuu wa serikali ataridhia suala la kulipa Dowans litakuwa halina mjadala”
Kwa kifupi Bwana Mhariri ametoa makosa mengi ambayo ameyatafsisi kwamba Sitta amekiuka uwajibikaji wa pamoja. Akaenda mbali zaidi akamfananisha na Agustine Mrema enzi zile za sakata la Chavda.
Lakini Bwana Mhariri Kibanda anapaswa kuelewa kuwa tunaposema ‘uwajibikaji wa pamoja’ awali tunapaswa kujiuliza ‘kuwajibika’ katika nini?
Uwajibikaji wa pamoja, hususan kweye baraza la mawaziri ni kusimamia na kutetea maamuzi mema ambayo washiriki wameyakubali na kuyapitisha hata kama mmoja wao hakukubaliana.
Nimesema ‘maamuzi mema’kwa sababu maamuzi hayo lazima yazingatie katiba, haki za binadamu na kanuni za uongozi.
Kwa hiyo Bwana Mhariri asifikiri kwamba ‘uwajibikaji wa pamoja’ wa baraza la mawaziri utakuwa halali, kama utahusu kuyavunja majeshi ya ulinzi na usalama na kubakisha wanamgambo!
Hata hivyo hakuna ukiukwaji wa uwajibikaji wa pamoja uliofanywa na Sitta katika sakata la Dowans, kwa vile hilo suala halikupata kujadiliwa na baraza la mawaziri wala chombo chochote cha serikali!
Badala yake, Sitta ndiye amekuwa mtetezi mzuri wa baraza la mawaziri, pale alipomshangaa waziri mwenzake kufanya maamuzi makubwa kama hayo ya kuilipa Dowans bila kujadiliwa na baraza hilo.
Vilevile Bwana mhariri amepotosha kwa makusudi kauli ya waziri Mkuu ambayo yeye mwenyewe ameiandika na mimi nikamnukuu hapo juu. Narudia tena kunukuu kwa uchache, “…Waziri Mkuu Pinda alipata kulizungumzia jambo hili na akasema iwapo mwanasheria mkuu wa serikali ataridhia suala la kulipa Dowans litakuwa halina mjadala”
Hapa neno ‘iwapo mwansheria Mkuu ataridhika” maana yeke ni kwamba jambo hilo bado lina utata, halifahamiki hata na waziri mkuu wenyewe hivyo ni jipya. Ndio maana akatumia neno ‘iwapo’.
Kama lingekuwa neno la kiofisi linalotokana na baraza la mawaziri au angalau ana kumbukumbu nalo, Pinda asingetumia neno ‘iwapo’. Angesema moja kwa moja ‘Tutalipa”.
Hivyo kitendo cha kulinganisha sakata la Mrema na Sitta ni upotoshaji wa makusudi kwa vile Chavda alijadiliwa kwenye baraza la Mawaziri, lakini sio tu Dowans haijapata kujadiliwa, lakini hata majina ya wamiliki wake rasmi hayafahamiki.
Hata hivyo mimi na watanzania wenzangu (wajinga na vipofu) ni heri yetu kupata mtu ambaye yupo tayari kwenda kinyume na maamuzi yenye kuliangamiza taifa letu na sisi wenyewe.
Lakini kinachofurahisha ni jinsi Bwana Mhariri Kibanda alivyoumbuliwa na Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya, ambaye katika makala yake ndiye alikuwa ‘somo wake’
Alisema wazi kuwa anaamini Msuya angekuwa waziri Mkuu leo, Sitta asingekuwa na kazi kama ilivyotokea kwa Mrema.
Siku chache baadaye Msuya akatoa taarifa ndefu kwenye gazeti moja akisisitiza kumuunga mkono Sitta na kulilaani tunda la Kati kati (Dowans)! Akasema hajui ni kwasababu gani Dowans walipwe! Kibanda tafuta taulo ujisitiri!
Ni jambo la kusikitisha kuona hasara ya Bilioni 94 inayowakabili watanzania Bwana Mhariri haioni, kwake anachoona ni tatizo ni Sitta!
Aidha Bwana mhariri haoni umuhimu wa kujadili kesi iliyoipa ushindi Dowans, kufunguliwa kinyemela huko ICC na kusikilizwa kwa siri kubwa kama maazishi ya Daudi Balali, ila kwake yeye tatizo ni Sitta. Kumbe tunda la katikati linalewesha, badala ya kujuza mema na mabaya! Au labda Bwana Kibanda ameahidiwa kuwa Ghorofa!
Ni katika ulevi huo, Bwana mhariri Kibanda ametoa kauli zinazoelekea kutoboa siri iliyojificha, pale aliposema “Sitta ni mwanasiasa aliyekosa ustahimilivu na uvumilivu ni mtu aliyekosa upendo kwa maadui zake,”.
Jamani kumbe Sitta ana maadui? Lakini ametakiwa eti awe na uvumilivu kwao.
Katika makala hayo Bwana Mhariri akawataka wanasiasa aliodai wananyooshwa kidole na Sitta kwamba ni Rostam Aziz, Nimrod Mkono na Edward Lowassa.
Kwa hiyo anataka kutueleza nini kuhusu uhusiano wa Dowans na hayo majina aliyoyataja? Anataka kusema hao anaowaita maadui wa Sitta, chanzo cha uadui wao ni Dowans? Ndio maana nikatangulia kusema hapa ametoboa siri aliyojitahidi kuificha, tangu mwanzo hadi mwisho wa makala yake hiyo. Kama aliowataja hawahusiki, iweje uadui wa jamaa hao na Sitta, uibuliwe kwenye sakata la Dowans? Ama sivyo, kwanini azungumzie ‘uadui’ binafsi wa watu katika mjadala wa Dowans?
Nafikiri wakati mwingine atatueleza kwamba hao maadui wa Sitta chanzo cha uadui wao ni nini, kama sio Dowans!
Tunavyojua Sitta ameshatoa msimamo wake wa kukataa Dowans walipwe, hivyo bila shaka maadui wake walio kinyume chake, wanataka Dowans ilipwe. Na kama wanataka ilipwe katika mazingira yaliyojaa dhambi nyeusi kiasi hiki, maana yake ni kwamba watafaidika na malipo hayo.
Kesho yake tena kwenye gazeti hilo hilo, ikaandika taarifa inayomnukuu mwanasheria Kennedy Fungamtama akiitaka serikali kupuuza kauli za Sitta kwamba Dowans isilipwe.
Fungamtama alichukua muda mwingi kuitetea Dowans na kuwatisha watanzania kwamba wasipolipa fedha hizo, eti watajiingiza kwenye matatizo ya kunyimwa misaada na wafadhili pamoja na kukosa wawekezaji.
Huyu Fungamtama anafanya kazi hii ya kuitetea Dowans kwa maelekezo ya nani? Kwanini Dowans wenyewe wasiwe mstari wa mbele kutetea hukumu ya ICC? Bila shaka Fungamtama ‘alishafungashiwa mtama’ wake, akawake kibindoni, vinginevyo asingeweza kufanya kibarua kisichomhusu.
Mimi sina mgogoro na Fungamtama kutoa maoni yake, lakini kinachoshangaza ni jinsi anavyotetea uhalali wa Dowans kulipwa, kuliko wenye Dowans wenyewe! Hili linatia shaka kwamba huenda amefanya kazi hiyo kwa malipo kwa vile kabla mtanzaia yoyote hajapata hukumu hiyo ya ICC, Fungamtama anasema yeye ameipata na ameisoma mara kibao! Kazi tunayo. Ninachosema hapan ni kwamba kama Fungamtama amefungashiwa mtama wake akaweka kibindoni, aseme kwani sio dhambi, kwavile wakili kama yeye anaruhusiwa kumtetea mtu kwa malipo, lakini asiwe mnafiki wa kutoa utetezi unaoelea hewani.
Ulevi wa tunda la katikati utafanya mengi yafahamike, nasi wananchi tunaoitwa wajinga na vipofu, tunamuomba mwenyezi Mungu iwe hivyo (Amen) kwani yafahamika ni faida yetu na siku ya siku Goliati atadondoka mwenyewe!
Tatizo nililoliona siyo urefu bali font ndogo kiasi cha kuumiza macho.

 
Mh nina wasiwasi ,mi ni msomaji wa Makala za Kibanda sioni dalili za kuchakuchuliwa!kama ndivyo basi Tnzania DAIMA YOTE!ALICHOJADILI mhariri ni kuhusu msimamo wa Sitta ,kwamba kama anajibainisha kuwa ni mpambanaji kwa nini yupo katika hilo kundi !na alisema kama yeye angekuwa ni Rais/waziri mkuu angemfukuza kazi,Kumbukeni anasema aangekuwa ni Kikwete au Pinda na kwa mazingira ya leo!Nani asiye jua kuwa watu wadilifu wanapoona wameingia sehemu isiyofaa hutoka haraka.inawezekana bwana mhariri anlitumia lugha kali !lakini ujumbe wake ni muafaka.Kumbekeni ni mojawapo wa waandishi aliyesimama thabiti kwa uwazi na hakutetereka kuonesha kuwa Kiwete alaikuwa anapewa sifa asizo stahili na alionesha kutofaa kwake kuwa mkuu wetu!aliyoondika leo kuna mtu atayabishia !


Kama hajachakachuliwa, mbona siku hizi yuko busy kutuandikia habari za Lowasa?? hata gazeti la uhuru halimpi coverage yoyote Lowasa lakini Kibanda siku hizi imekuwa bandika bandua Lowasa hakosi kwenye front page.

Ni dhahiri kwamba kibanda ameshachakachuliwa, na siku zake zinahesabika, yuko njiani kuelekea kwa bosi wake muya fisadi papa

si umeona kuna mhariri mmoja tayari ameshachoropoka na kuingia zizini?
 
Nimeisoma Makala yako hii ndefu na kugundua kwamba ina weledi wa hali ya juu na ni nzuri sana. Sasa nimemuelewa vema kibanda-na kikoba chake alichokabidhiwa! DOWANS HAKUNA KUKUBALI mpaka kieleweke. BIG up 6, usikate tamaa, najua mafisadi watalipa watu wengi sana kujitakasa wakiwemo wanasheria wawapigie debe kama BOMANI! Lakini mwisho wa habari-DAMU YA WATANZANIA ITAWASUTA HATA MKIWA KABURINI!!!
 
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, anafanya kazi part-time kwenye magazine inayomilikiwa na Edward Lowassa inaitwa UMOJA. Pia Kibanda amekuwa anatoa habari za kumbeba Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge kwenye Tanzania Daima mara nyingi. Kwa kupokea maagizo na malipo kutoka kwa Lowassa na Rostam Aziz, Kibanda pia amekuwa akiandika habari na makala nyingi za kuwakashifu Samuel Sitta, Harisson Mwakyembe, Bernard Membe na John Magufuli.

Tanzania Daima ni moja ya magazeti yanayotumiwa na fisadi Rostam Aziz kutetea ufisadi mbalimbali, ikiwemo malipo kwa Dowans kwa nguvu zote. Wanaitumia Tanzania Daima kwa kuwa gazeti linaaminika kuwa ni huru na ni rahisi ku-brain wash watu kuliko kutumia Mtanzania/Rai ambayo Watanzania hawayasomi tena sasa baada ya kugundua kuwa yanamilikiwa na Rostam.

Cha kushangaza ni kuwa mmiliki wa Tanzania Daima, Freeman Mbowe, anaachia tu gazeti lake litumiwe na mafisadi kupitia kwa Kibanda kuangamiza nchi.

Umesema yote kamanda.
Ang'olewe tu Tz Daima, aende rasmi kwa Rostam na Lowassa au kwa Ridhiwani (Jambo Leo) ili awe wazi. Kama vp aende Uhuru au Habari Leo.
Vinginevyo anakuwa anaharibu from within.
Credibility ya magazeti ya mafisadi ni ndogo ndiyo sababu wanatafuta wahariri wa magazeti mengine. Lets be vigilant!

Mambo ya kuwasifia Rostam, Lowassa, Chenge na kuwakashifu Sitta, Dk Magufuli, Dk Mwakyembe na Membe sanasana yanamuonyesha muandika makala hizo jinsi alivyonunuliwa.

Kuhusu hiyo makala, si ndefu kiasi cha kumfanya msomaji makini achoke. Tuwe na utamaduni wa kusoma na kujisomea!
 
bandikeni alichoandika Kibanda la sivyo acheni ngojera humu

Tatizo kubwa letu hatupendi kufanya tafiti hilo gazeti nami nililisoma na kustaajabika sana kuhusu huyo kibanda na sasa nanyi mwashindwa elewa au hamkununua gazeti hilo okay me ninalo kesho ntali post hapa maana mwenzenu kachukua kwa ufupi tu na kutupa dondoo zake na alicho kisema ni kweli huyo mhariri Kibanda alichemka kubwa pamoja na ni mawazo yake ila yameendea kushoto sana

 
Sitta si safi na kama safi angeruhusu mjadala wa Richmond uendelee mpaka kuparta muafaka bungeni na kwa hesabu tu marupurupu ya Spika yanazidi ya Uwaziri alionao ndo maana anakurupuka.
Sikatai anasema jambo jema lakini wasiwasi wetu wananchi ni kwamba hizi ni hasira za kuukosa uspika.
Kama safi ahame chama maana kinanuka
 
laiti kama sitta angeruhusu kifikiwa kwa maazimio ya bunge leo hii tusingekuwa na dowans,kwa kuogopa kwake hawezi kamwe kukwepa dhambi hii....tafakari
 
SITTA SHUJAA WA WATANZANIA.

Nampongeza sana kwa kuwa ndiye mtu pekee anayesimamia ukweli mpaka sasa. Najua fika kuwa sita analijua suala la DOWANS vizuri

kuliko mtu yeyote. DOWANS ni mafisadi wapo hapa hapa na pengine wapo ikulu. Ipo siku watachomwa moto kule mbinguni mana

mungu kasikia kilio chetu cha kulala gizani ana watoto wetu wanakufa kwa ajili ya joto la dar.
 
Kibanda, Kibanda wait and see lakini ameshanunuliwa
 
watu wanachoka kusoma summarize

Mkuu kwani wewe unamsemea nani hapa? Sema umechoka kusoma usiseme tumechoka, wewe na nani? Au ndo hivyo unajaribu kufanya kazi uliyotumwa kuifanya? "Motion neutralizer"?.

Huyu mwandishi naona ameamua kumpiga nyoka Kibanda kichwa ili kummaliza kabisa wala hakupiga mkia hata kidogo. Kina Kibanda ndio waandishi uchwara wanaotetea upumbavu katika nchi hii eti kwa kuwa wamekatiwa kitu kidogo. Hata wakifanya nini malipo hayo hayatafanyika. Ngoja tusubiri kauli ya JK juu ya hili.

Tiba
 
Back
Top Bottom