Kibanda
Platinum Member
- Aug 27, 2009
- 87
- 45
Naamini Jamiiforums ni Home of Great Thinkers sasa hawa ndugu zangu akina informer na wengine ni kwa nini wanashusha tuhuma nyingi wasizo na uhakika nazo. Mimi ndiye Absalom Kibanda. Nimekuwa Mhariri wa Tanzania Daima huu ni mwaka wa nne na ninaelekea wa tano. Msimamo wangu kuhusu mambo kadha wa kadha haujabadilika.
Kila mtu ana uhuru wa kufikiri anavyotaka. Niweke kumbukumbu sawasawa. Sina sababu hata moja ya kununuliwa na mtu yeyote. Rostam Aziz amekuwa mkurugenzi wangu Mwananchi na nikaacha kazi kinyume cha matakwa yake. Ninaamini katika mabadiliko. Nimeanza kumpinga Sitta kila anapofanya mambo ambayo sikubaliani nayo tangu akiwa spika na hata kabla Lowassa hajajiuzulu.
Nikiwa mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima ninatoa uhuru kwa viongozi wote pasipo kujali misimamo yao kutoa maoni yao. Nimeruhusu mijadala ya kina kupitia Tanzania Daima kutoka pande zote mbili. Kwangu mimi Rostam, Sitta, Lowassa, Chenge, Mwakyembe na wengine wote ni vyanzo muhimu vya habari na kwa Tanzania Daima wana nafasi sawa kihabari. Msimamo wangu huo uko bayana na kimsingi hili ndilo gazeti linalokimbiliwa na kila mtu, hatufungamani na upande wowote zaidi ya kupigania mabadiliko. Ninapata furaha nisikiapo nikituhumiwa kuwa wakala wa Chadema, mara wakala wa CUF, mara wakala wa mafisadi, mara wakala wa Kikwete kwa sababu ya msimamo huru wa mawazo.
Nilikataa tangu mapema kujiingiza katika vita ya ufisadi inayopiganwa na akina Sitta na akina Mwakyembe kwa sababu nimejiridhidhs kwamba ni vita ya kitapeli na yenye malengo ya kisiasa zaidi kuliko kihalisia. Naamini na hili nimekuwa nikiliandika katika safu yangu ya Tuendako kuwa ufisadi uliopo nchini unakigusa Chama Cha Mapinduzi moja kwa moja. Kwa hiyo hakuna anayeweza kumnyoshea mwenzake kidole. Viongozi wote wa juu wa chama hicho tawala wakianzia na mwenyekiti wao wa taifa hawana ubavu wa kukwepa tuhuma halisi za chama chao kuhusika katika ufisadi.
Hiyo ndiyo dhambi yangu iliyonikosanisha na wengi katika taaluma. Nimekataa kuingia katika mkumbo wa kujifanya mwanaharakati na jemedari wa ufisadi kwa kuwa naamini ni unafiki. Ni jambo la kheri kwamba wamiliki wa Tanzania Daima wanathamini mchango wangu, wanaufahamu na kuuamini msimamo wangu, wanaujua uzushi wa kila siku wa akina informer ambao wao wanalipwa mamilioni ya fedha kuwachafua akina Lowassa kwa sababu ambazo mimi ninazijua na ushahidi upo.
Acha nihukumiwe kwa haki huku nikiwa na uhakika kuwa ipo siku historia itanitetea