Nakushirikisha Fursa nono ya kibiashara nchini India

Hii iko vzr lkn watanzania walio wengi hawajaona km zao la mbaazi linalipa ila umenifungua macho kaka
 
Ontario Kwa kifupi mimi ninatoa elimu ya kilimo hifadhi kwa wakulima wa kanda ya ziwa, among things we do ni ku connect farmers na crops buyers karibuni wa hizo peagon peas, chick peas na green gram. Naomba nijaribu kuona prices na availability of the ptoduct na nitakuja au waweza kuni PM ili tuongee vizuri
 
mayumbo
Nashukuru sana kiongozi, naomba unicheki PM please.
 
Last edited by a moderator:
kwanza kwa lindi na mtwara hiyo bei ya 4000 haijawahi kutokea,bei ya mbaazi haijawahi kuzidi 1500,ila kama upo serious mkuu mie nipo tayari na naweza kulima hata eka 40 ,tafadhari,najua kuna mbegu nzuri tu kituo cha utafiti NALIENDELE MTWAR
duh kweli inabidi kuwa careful...manake kama Lindi ni Tshs 4,000 then yeye ananunua USD 0.9 /Kg manake ni kama Tshs 1,800 ...inakuwaje hapo wakuu?
 
Kuhusu mashamba ya kukodi nishirikisheni, sumbawanga ni pesa yako yapo hadi maelf ya hekari, mie nilikodi heka 8 lakini tupo kwenye makubaliano ya kuuziana na ni km 4 toka stand kuu
 
Jamaani mtoa taarifa aliye sema bei ilifika sh 4,000/= siyo sahihi na haija wahi , mfano mwaka huu ilicheza sh 1200 mpaka 2350 sasa hivi.
Jamani kama kuna mtu anakua hanataarifa sahihi atawapotosha wengine kwa kuwasadikisha taarifa zisizo sahihi.
 
Jamaani mtoa taarifa aliye sema bei ilifika sh 4,000/= siyo sahihi na haija wahi , mfano mwaka huu ilicheza sh 1200 mpaka 2350 sasa hivi.
Jamani kama kuna mtu anakua hanataarifa sahihi atawapotosha wengine kwa kuwasadikisha taarifa zisizo sahihi.


Mkuu masagati, nashukuru sana kwa hii taarifa
 
Last edited by a moderator:
Nlitaka nishangae ina maana bei ya mbaazi imezid ata ya maharage dukani...jaman ayoo mambo ya pm mngeyaacha mwageni vitu watu tuelemishane zaid..
 
Mkuu ONTARIO Congrats Kwanza. Hujawa Mchoyo Umeamua Kushahare na WanaJf hapa.

Mimi nitakutafuta kama upo UDSM tuonane.. I bet we can talk something.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu @ONTARIA Congrats Kwanza. Hujawa Mchoyo Umeamua Kushahare na WanaJf hapa.

Mimi nitakutafuta kama upo UDSM tuonane.. I bet we can talk something.


Nipo Dar, lakini tarehe 14 Oct naingia porini mkuu, nawahi vuli Ifakara.
 
MBAAZI (PIGEON PEAS)--Cajanus cajan


Utangulizi

- - - - - Mbaazi ni zao la chakula ambalo pia linaweza kulimwa kama zao la biashara kutokana na kuwa na soko zuri la Mbaazi.Mbaazi ina kiasi kikubwa cha protini.Mbaazi inaweza kutoa mavuno ya tani 3.5 hadi 4 kwa hekta

HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO CHA MBAAZI
- - - - - - Mbaazi zinafaa kulimwa katika maeneo ya ukanda wa chini kutoka usawa wa bahari na pia hata sehemu za nyanda za juu nazo zinafaa kulimwa zao hili.-Ni zao linalostahimili ukame na hili linalifanya kulimwa hata katika maeneo yanayopata mvua za wastani na yale yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.


UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA MBAAZI

- - - - - - -Mbaazi zinastawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia linaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya mfinyanzi katika maeneo yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.

AINA KUU ZA MIMEA YA -MBAAZI
- -Kuna aina kuu tatu za mimea ya mbaazi
1)Mbaazi za muda mrefu: Hii ni mbaazi ambazo zinawezwa kuvunwa katika misimu zaidi ya miwili.Huchukua muda mrefu kukua hadi kuvunwa kwa mbaazi zake.Baada ya mbaazi kuvunwa Mbaazi hukatwa nusu yake na kuruhusu Machipukizi yake kukua na kuvunwa tena msimu unaofuata na zoezi hili hufanyika ziadi ya msimu mmoja.Huchukua Siku 180 hadi 270 kupandwa hadi kuvunwa

2>Mbaazi za Muda wa kati; Hizi hulimwa kwa msimu mmoja ila huchukua mda wa kati katika kukomaa kwake.huchukua siku 140 hadi 180

3)Mbaazi za muda Mfupi:Hizi hulimwa kwa msimu mmoja na baada ya kuvunwa mimea yake hukatwa na kung'olewa na kupandwa mbegu mpya msimu unaofuata.mbegu hizi huchukua siku 120 hadi 140.

MAANDALIZI YA SHAMBA
- - -Andaa shamba lako mapema kadri utakavyoweza kulima kulinga na aina ya kilimo unachotumia, hakikisha umeondoa magugu shambani na uchafu mwingine ambao unaweza kuinyima mimea ya mibaazi kukua vizuri.

UPANDAJI
1> Mbaazi za Muda Mirefu; Panda kwa mistari kwa umbali/ nafasi ya sentimeta 150 kwa 100.
- - - - - - - - - - - - - - - - -(Sentimeta 150 Mstari na mstari na sentimeta 100 Shina hadi shina katika mstari)
2>Mbaazi za Muda wa Kati; Mbaazi.Panda kwa mstari nafasi ya sentimeta 100 -kwa 60

3>Mbaazi za Muda -Mifupi;Panda kwa mstari -kwa umbali/ nafasi ya sentimeta 90 kwa sentimeta 60


ANGALIZO: Maaneo ya Pwani ambayo yanarutuba kwa wingi na joto la kutosha mimea inakuwa kwa kasi na ili upate mavuno bora lazima uhakikishe mimea yako unaipa nafasi ya kutosha,Hivyo uwe makini na nafasi za mimea yako uanapopanda shambani.


MBOLEA ZA VIWANDANI -NA SAMADI
- -Mara nyingi zao la mbaazi halihitaji matumizi ya mbolea na samadi.Ijapokuwa Hustawi zaidi katika shamba lenye rutuba ya kutosha.

PALIZI
- - Mimea ya mibaazi huitaji kupaliliwa mapema ili kufanya ikue katika hali ya afya bora na kusaidia kuongeza mavuno yako.

WADUDU WANAOSHAMBULIA MIBAAZI NA MBAAZI
- - - Mbaazi ni mojawapo ya mazao ambayo hayashambuliwi sana na wadudu japokuwa wapo wadudu ambao kuna maeneo mengine hushambulia kwa kiasi kikubwa mbaazi nao ni funza wa tumba na wadudu wapekechaji wa mbaazi. Zuia wadudu hawa kwa dawa za wadudu kama ATTAKAN-C,Karate au dawa nyingine za wadudu.

MAGONJWA YA MBAAZI-
- - -Ugonjwa mkuu unaoshambulia mbaazi ni mnyauko wa fusaria ( fusarium wilt).Ambao husababisha shina la mbaazi kuwa na rangi nyeusi,ugoro au kahawia.ugonjwa huu huzuia mfumo wa usafirishaji wa mmea.Zuia ugonjwa huu kwa kuzungusha mazao shambani kila baada ya msimu kuisha.usipande kila msimu mbaazi tuu.Kila msimu badilishaz zaa.

UVUNAJI WA MBAAZI
- - Mbaazi zikishakomaa na kuanza kukauka zivunwe mapema kwa kukatwa matawi yenye mbaazi na kukaushwa zaidi kisha Mbaazi zitenganishwe kwa mikono au kwa kupigwa hayo matawi -taratibu -baada ya kukaushwa sana.
 
Mbaazi ni zao lenye uhakika, maisha yake muda mwingi ni wakati wa kiangazi, hudumu zaidi ya msimu mmoja, ila inabidi watu wanaposherehekea bei kubwa ya mbaazi wajue pia mavuno yake kwa ekari. Ninaambiwa kuwa ekari moja hutoa kilo 400 hadi 800 kutegemea aina na matunzo. Hivi sasa kumetokea wimbi kubwa la kutafuta mbaazi kwa nguvu sana, labda zinatumika kutengeneza kitu muhimu sana. Ninachokushauri mkuu Ontario, badala ya mhindi huyo kutaka kulima, angeingia mkataba na wakulima wadogo kwa wakubwa kwa yeye kuwawezesha kidogo gharama ya kutifua udongo na mbegu na utaalamu wa uzalishaji, nakuhakikishia kwa jinsi ninavyofahamu zao la mbaazi, huyo mhindi angeweza kupata mzigo anaotaka na atazikimbia!! Hivi ndiyo wanavvyofanya wanunuzi wa Tumbaku, yale makampuni yanayonunua tumbaku hawana mashamba bali wanawawezesha wakulima kwa mkataba kwa kuwapatia pembejeo muhimu na utaalamu na hununua tumbaku yao.
 
Back
Top Bottom