Nakushirikisha Fursa nono ya kibiashara nchini India

Nakushirikisha Fursa nono ya kibiashara nchini India

Ni kweli kaka mbaazi kwa ekari unapata kilo chache sana nakumbuka miaka ya tisini na mama yangu maeneo ya kusini uku tulilima kama tu ka eka moja tukipata tu Kilo 50 tunaridhika wenyewe mboga... Ila siku hizi mbaazi imekua hatari ndugu zangu walikua wanavuniwa shamba lao na wezi usiku kwa usiku.
 
Mbaazi ni zao lenye uhakika, maisha yake muda mwingi ni wakati wa kiangazi, hudumu zaidi ya msimu mmoja, ila inabidi watu wanaposherehekea bei kubwa ya mbaazi wajue pia mavuno yake kwa ekari. Ninaambiwa kuwa ekari moja hutoa kilo 400 hadi 800 kutegemea aina na matunzo. Hivi sasa kumetokea wimbi kubwa la kutafuta mbaazi kwa nguvu sana, labda zinatumika kutengeneza kitu muhimu sana. Ninachokushauri mkuu Ontario, badala ya mhindi huyo kutaka kulima, angeingia mkataba na wakulima wadogo kwa wakubwa kwa yeye kuwawezesha kidogo gharama ya kutifua udongo na mbegu na utaalamu wa uzalishaji, nakuhakikishia kwa jinsi ninavyofahamu zao la mbaazi, huyo mhindi angeweza kupata mzigo anaotaka na atazikimbia!! Hivi ndiyo wanavvyofanya wanunuzi wa Tumbaku, yale makampuni yanayonunua tumbaku hawana mashamba bali wanawawezesha wakulima kwa mkataba kwa kuwapatia pembejeo muhimu na utaalamu na hununua tumbaku yao.

Nashukuru sana kiongozi wangu Kubota, hiki ndicho nakifanya sasa.

Yayari nipo ktk makubaliano na huyu Muhindi aje Nov/Dec tufanye utaratibu wa kuInvest kupitia wakulima wadogo wadogo.

Nikikwama nitawashirikisha wanazi wa kilimo....

Vijana tumeeanza, wazee mtupe dira.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ontario kama ni hivyo niko Kilosa, usitusahau wakulima ni wengi sana na maeneo ni makubwa tu
 
Sory kwa kuchelewa kujibu, mkuu kwa kaasi hicho kwa sasa sidhani kama kinaweza patiakana, make msimu wa kilimo usha isha, na ili kupata hizo tani 50 inahitajika shamba si la kitoto make mbazi hazizai sana, vile vile ni kweli kwamba Wahindi wanahitaji sana mbazi na zina demand sana huko India na hata kama isingekuwa huko India bado soko la mbazi ni kubwa sana na supply ni ndogo kuliko demand na hii inasababishwa na nature yake kwa sababu mikoa mingi mfano Mkoa wa Manyara wanalima sana Mbazi ila huwa sio first priorities make mbazi huchanganywa na mahindi na pale mahindi yanapo vunwa na baadae mbazi huvunwa.

Ishu ni kwamba unaweza zipata tu wakati wa msimu but ni kujinadaa kwa competition kutoka kwa wanunuzi wengine hasa wahindi, kuna wahindi wengi sana huku bongo wanafanya hiyo biashara ya kununua mbazi mimi nimekuata nao mara kibao.
 
JF ya sasa hivi inashangaza kidogo, watu wanapenda sana kukimbilia PM hata kwa vitu ambavyo vinahitaji majadiliano ya kuelimishana tu na kunufaisha wengine!
 
duh kweli inabidi kuwa careful...manake kama Lindi ni Tshs 4,000 then yeye ananunua USD 0.9 /Kg manake ni kama Tshs 1,800 ...inakuwaje hapo wakuu?
Hao ndio Wahindi bwana, siku zote wao ni walaliaji wakidhani sisi hatujui. Kwa bei yake, ni heri hata bei ya wakulima wa Lindi, lima na uuze hapa hap! Hata hivyo nakushauri, the best approach, mwambie muingie naye ubia wa kulimahuzo pegion peas hapa na mkauze India kama wabia. Wewe toa ardhi yeye atoe working capital. Zungumza na watu wako wa TPSF wakupe maujanja ya biashara. All the best.
 
Mkuu ontario kheri ya mwaka mpya na wachangiaji. Wote hapa.
 
Aisee kama hii opportunity iko serious, please naomba tukutane, niko na heka zangu 30 mkoa wa Kilimanjaro, full irrigation. Sitegemei mvua, kama vp atoe working capital, watu tuingie shamba
 
Nashukuru sana kiongozi wangu Kubota, hiki ndicho nakifanya sasa.

Yayari nipo ktk makubaliano na huyu Muhindi aje Nov/Dec tufanye utaratibu wa kuInvest kupitia wakulima wadogo wadogo.

Nikikwama nitawashirikisha wanazi wa kilimo....

Vijana tumeeanza, wazee mtupe dira.


Hii project iliishia wapi mkuu!?
 
Mkuu mimi heka 100 ninazo ila zipo mkoani Tabora na ni shamba jipya la kufyeka msitu eneo ni kubwa mno yaani ni zaid ya ekar 200
 
m
Nawasalimu ndugu zangu wa JF, Habarini!

Niende moja-kwa-moja kwenye mada husika.
Mimi ni kijana (21), mjasiriamali wa kilimo na mwanafunzi (UDSM).

Kutokana na harakati zangu za kilimo cha biashara, huu mwaka umekuwa wa mafanikio sana kwangu na kwa kampuni yangu pia, hii imeniwezesha kupata media coverage kubwa hasa nilipomulikwa na CCN startup Africa, How we made it in Africa, venture africa, ALU, mkulima young, pamoja na blogs nyingi ikiwemo millard_ayo.com. Pia nimeweza kupata membership TPSF.

Media coverage hii imeniwezesha kupata connections nyingi sana, ndani na nje ya nchi. Sasa ningependa niwashirikishe hii fursa kubwa zaidi kutoka India.

Kuna mfanyabiashara mkubwa kutoka India alinitafuta kupitia twitter, tukapeana emails, then tukaanza mawasiliano. Huyu bwana anahitaji tufanye partnership katika kilimo_biashara...

Anahitaji tufanye biashara ya pigeon peas, kwanza hapo awali sikumwelewa. Nikazama google nikagundua kuwa hizo pigeon peas ni mbaazi, na kwa hapa Tz zinalimwa sana mikoa ya kusini. Hitaji la jamaa ni kwamba niwe nasupply kwake 50 metric tons kila mwezi, ambapo alidai 1 ton ni $900 kwasasa. Ijumaa last week akaniuliza kama naweza kupata 500 metric tons kabla ya xmas.

Nilipopiga hesabu zangu za haraka-haraka nikaona uwezo wangu kusupply hiyo tender ni mdogo sana, kiasi kwamba sitaweza kukidhi hitaji lake, while at the same time sitaki nimpoteze kizembe zembe. So nikamuomba huyu bwana awe mvumilivu kwanza wakati mimi natafuta plan B. Nikamwambia nitamtafuta soon nitakapoweka vitu sawa.

Pia jamaa alikuwa attracted sana kufanya kilimo hicho cha mbaazi hapa Tz, nikamweleza inawezekana sana, akaniwekea tenda mezani nimtafutie shamba la kukodi heka 100 kwa kuanzia. Kwa haraka-haraka nikamweleza mashamba ya kukodi yapo, na ni 100,000/ha, jamaa akasema nifanye hima by Nov nimpe feedback.

Naleta kwenu hii fursa ndugu zangu wa JF, tukamate hii fursa tuendeleze mapambano ya kuinua kilimo cha mkulima wa hali duni...


Malila Chasha Poultry Farm Kubota Mama Joe Watu8 mwekundu boss Sikonge Mkoroshokigoli Mzuzu Msanii n.k n.k karibuni sana.
mbaazi, choroko, ngwara,kunde haya mazao yote ya jamii ya mikunde(pulse) yana soko kubwa sana India kuna msimu huwa gunia la ngwara linafika mpaka shs 350,000 ila kwa mwaka huu kutokana na sababu ambazo hazijulikani kwetu wakulima wa mazao haya bei ipo chini sana na hakuna wanunuzi wanaokuja kununua toka INDIA kama zamani.kwa stori za mitaani tunaambiwa kuwa INDIA wamevuna nyingi mwaka huu na wengine wanasema tatizo mwaka huu ni ushuru umekuwa mkubwa.Kila mwaka huwa nalima na kununua mazao haya kwaajiri ya kuyauza baadaye bei ikipanda kwa mwaka huu store zimejaa,bei chini na wanunuzi hakuna.kwa mawasiliano zaidi inbox.KUHUSU ENEO LA EKA 100 NA HATA MAZAO YENYEWE NITAKUPA USHIRIKIANO.Hii ndio kilimo na biashara yangu!
 
Back
Top Bottom