Kinana atoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa ya kibiashara kwenye Kituo cha 'EACLC' kinachojengwa Ubungo

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za kibiashara kwa kuchukua mapema maeneo ya kufanyia biashara kwenye mradi wa kituo cha biashara cha Kimataifa kinachojengwa eneo la Ubungo ilipokuwa stendi Kuu ya Mkoa wa Dar es Salaam ambao unatarajiwa kukamilika mwaka huu 2024 katikati.

Wito huo umetolewa leo January 31, 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ambaye ametembelea kampuni inayoratibu mradi huo ya EAST AFRICA COMMERCIAL & LOGISTICS CENTER (EACLC) na kufika sehemu ya mradi huo kuona ujenzi unavyoendelea.

Baada ya kutembelea mradi huo na kufanya kikao kifupi na EACLC pamoja na ubalozi wa China nchini Tanzania Kinana amesema "Nataka nitoe wito kwa watanzania kuchangamkia fursa hii na ningependa kuona asilimia 100 wafanyabiashara kwenye kituo hiki ni watanzania, tusije tukafungua tukawakuta watu wa Nchi jirani ndio wanakuja kufungua biashara hapa wakati watanzania tupo"

Kinana pia ameeleza umuhimu wa mradi huo ambao amedai kuwa ni uwekezaji mkubwa, amesema ni kuchochea cha kukuza uhusiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na China.

"Mradi huu utasaidia kukuza viwanda biashara na mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na China, pili mradi huu pia utasaidia sana kukuza biashara kati ya Tanzania na Nchi zote za jirani, tatu ni dhahiri kwamba watanzania na wafanyabiashara wa Nchi za jirani hawatakuwa na sababu yoyote baada ya kituo hiki kukamilika kwenda Dubai, India wala China kila kitu kitakuwa kinapatikana hapa" amesema Kinana

Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita imekuwa mstari wa mbele kutoa msukumo kwa uwekezaji binafsi akidai kuwa lengo ni kuongeza manufaa yanayotokana uwekezaji huo.

"Napenda ni wahakikishie kuwa Serikali ya awamu ya sita ni Serikali inayotoa msukumo maalumu wa uwekezaji binafsi kwa sekta binafsi kama sehemu ya kukuza biashara, sehemu ya kukuza ajira, sehemu ya kukuza mapato kwa Serikali kwahiyo kituo hiki kitakuwa na manufaa makubwa sana"

Kwa upande ubalozi wa China sambamba na EACLC wamepongeza ushirikiano mbalimbali unaotolewa na viongozi wa Serikali katika kutekeleza mradi huo jambo ambalo limeeleza kuwa ni matokeo ya uhusiano mzuri wa kiuchumi uliopo baina Tanzania na China.

Ikumbukwe Mradi huo ambao unatajwa kukamilika mwezi Juni 2024, unadaiwa kugharimu thamani ya dola za kimarekani Milioni 118 ambapo kwa pesa za kitanzania ni sawa na Bilioni 271 na kuwa utakua na maduka pamoja na ofisi jumla 2,060.

Waratibu wa mradi huo tayari wameweka utaratibu wa wanaohitaji maeneo ya kibiashara kuanza kulipia gharama mapema jambo ambalo Kinana amelisisitiza.
IMG_20240131_115922_545.jpg
IMG_20240131_105413_160.jpg
IMG_20240131_120421_309.jpg
IMG_20240131_105350_493.jpg


Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Unaambiwa utoe 17m hiyo kodi kwa mwaka hii baada kutaka kujua gharama zao zipoje
 
Nilienda pale wakaniambia nitoe mil. 2 kama booking ya chumba /frame ya biashara! Muda wa kuanza kulipa kodi ukifika usipolipa imekula kwako!
 
Back
Top Bottom