Sukari, mchele ni kama dhahabu nchini Burundi. Tuchangamkie fursa

KENGE 01

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
1,592
3,839
Anaandika Kenge,

Nimeshaandika nyuzi kadhaa nikielezea na kuwasogezea michongo mbalimbali inayopatikana nchi jirani. Sasa naendelea kuwaletea hapa ndugu zangu wanajamvi hasa sisi vijana ambao bado tunajitafuta,Tujadili tuone namna gani tunajikwamua kiuchumi.

Kama nilivyosema nchi hii(Burundi)inahali mbaya(Maskini)mara 2 au 3 zaidi yetu. Kwahiyo kila kitu ikiwemo huduma za msingi ni tatizo kubwa sana.Tukianza na Umeme sio wa uhakika kabisaa.Maji yanatoka kwa masaa yakitoka mchana,basi usiku hayatoki Achana na Network ambayo 4G bado haijafika takriban nchi nzima a vitu kama ivyo.

Sasa kwenye suala la chakula kuna vitu havikwepeki kama Sukari.Sukari nchini burundi ni adimu sanaaa..hapa naongelea mji mkuu wa bujumbura achana na uko vijijini sijui wana hali gani ndugu msomaji.

Sukari ni adimu kiasi kwamba ukienda kwenye migahawa ukiagiza maziwa na ukataka wakuwekee sukari basi itakubidi uongeze pesa kwa kila kijiko.Na kama ni chai sahau swala la kuweekewa sukari mezani ujipimie kama bongo.Hapa chai utakuta imeshawekewa sukari na ni kidogo sana kiasi inakosa radha.Nyumba nyingi hutumia Asali kama alternative.

Sasa achana na sukari kidogo, MCHELE nao ni tatizo kubwa lingine.kilo ya mchele ni 6k faranga .Sasa ukitazama vitu kama hivi unaona kabisa ni fursa ambayo hawa kina MO Wanajipigia sana pesa huku.

Kama utakua na uhakika wa kupata tani kadhaa kuanzia 1-5 tu kwakuwa sukari inahitaji mtaji mkubwa.Nikuhakikishie vijana wengi wanauwezo wa kupata nusu tani au hata tani 1 ya mchele kwabmtaji wa 5M tu zinatosha kuanza safari.

Twende sawa sasa..

Nitaieleza kiunaga-ubaga.

Hapa utachukua mzigo wako utafunga kwenye Lori.Kisha safari itaanza.Kuna njia ya Kahama utapita hapo kisha utafika sehemu inaitwa Kibanga hapo itabidi ulipie Sumatra sijui TRA ili wakupe kibali cha kuendelea na safari. Baada ya kufika mpakani PASSPORT ni muhimu sanaa. Utaonesha vibali watakupigia mhuri apo boda.

Kisha utaruhusiwa uendelee na Safari.S asa kutoka boda mpaka Bujumbura ambapo ndio Target ya soko linalozungumziwa hapa. Ukifika Buja utafikishwa BANDARINI wanaiita (Buja port) watakagua mzigo wako kama umeweka madawa je? Wakimaliza sasa hapohapo bandarini kama ni mgeni utatafuta maagent wa bidhaa yako. Kama ni mwenyeji Agent atakuelekeza pakufikisha mzigo

Nikuhakikishie ndani ya Siku 2-3 watu wakijua unaSukari wataigombania kama mpira wa kona ndugu msomaji utarudisha mtaji na faida yako kwa haraka sana.Na kama umekaa kizembe utapigwa pesa ndefu sana na uje umlaumu bwana KENGE kwa kukulisha matango pori.

Huku wanasema Sukari ni dhahabu,Lakinu ukiingia kichwakichwa utapigwa vibaya sana.Nisikufiche kama unakuja individual yani wewe,dereva na mzigo kwa mara ya kwanza itakuwa vigumu sana tofauti na makampuni kama MO naona ndo anakimbiza huku na Lake Oil hawa awasumbuliwi sana tofauti na wewe unaekuja individual kama unamoyo mdogo unaweza kukata tamaa mapema sana.

MAMBO YA KUZINGATIA
-Passport ya kusafiria ni muhimu sana lakinimpakani unaweza kuhonga 15k wakakupa kibali

-Vibali vya kubeba mzigo
Yani cha kwanza utaombwa kibali hasa ukiwa TZ.vibali sijui latra,Sumatra,TRA na takataka zote ni muhimu sana.

-CRDB mastercard.
Hapa niwapongeze CRDB kwakuwa ukiwa na mastercard unaweza kutoa pes kwenye ATM zao.Pia utaweza kuona rate ya kubadili pesa Tsh to Faranga

USHAURI..
Tumia kampuni za usafirishaji badala ya kutumia gari ambazo hazijasajiliwa kikampuni.

2.NJIA YA KINYEMELA
Hapa napita juujuu kwakuwa wasakatonge wengi wanapeleka ugali nyumbani watoto washibe kwa njia hii.Haitapendeza kuharibu kwani JF imejaa watu tofauti hata wewe Afisa wa TRA najua utapita hapa kusoma.

Hapa kuna baharia wanapitia L.Tanganyika kufikisha mzigo hapa ni mpaka uwe na connection na warundi wajanja wa hizi kazi.

Lakini pia kuna wataalamu wengine wakwepa (Tax) wanapitisha mzigo vizuri sana mpakani lakini ni mpaka uwe na connection na hao watu na pesa nyingi sana utatoa

Kama unamambo mengine unayajua shusha nondo hapa.Vijana wa Buja wamelala sana wanawaza ULAYA Tuuu yani hakuna kitu utawaambia kuhusu ulaya wakakuelewa.Na hivi wanapata kamteremko flani kwenda huko basi wengi huwaza kwenda uko masaa 24/7

NAWASILISHA HOJA.
WAKO MTIIFU,Jini Genious
Mdau,KENGE 01
 
Burundi wana kiwanda chao cha sukari na huuza bei ndogo, na kuna wafanyabiashara huenda kununua huko kutokea Tanzania, zambia na malawi hutumia viazi vitamu kutengeneza sukari na ndio maana wao sukari iko bei ya chini , mchele na sementi ndio biashara kubwa kwa Burundi
 
Unaongelea Burundi ipi?
~Hiihii inayotegemea 70% ya vitu kutoka TZ
~Sukari bei rahisi burundi??
~Viazi kutengeneza Sukari??
Ivi unajua hata raw material za sukari kweli mkuu??
 
Burundi wana kiwanda chao cha sukari na huuza bei ndogo, na kuna wafanyabiashara huenda kununua huko kutokea Tanzania, zambia na malawi hutumia viazi vitamu kutengeneza sukari na ndio maana wao sukari iko bei ya chini , mchele na sementi ndio biashara kubwa kwa Burundi
Bro naomba usikae kimya, ebu tueleze n kivp vip viazi vinatengeneza sukari
 
IMG_1512.jpg

Hivo ni viazi huitwa sugar beet ambavyo hutumika kutengeneza sukari
 
Kajisomeeni kuhusu sugar beet (viazi maalumu kwa kutengeneza sukari) ambapo wazambia wao walishaingia kwenye teknolojia hiyo muda mrefu sana ndio sababu hauwezi kusikia kwao sukari imekua adimu
 
Anaandika Kenge,

Nimeshaandika nyuzi kadhaa nikielezea na kuwasogezea michongo mbalimbali inayopatikana nchi jirani. Sasa naendelea kuwaletea hapa ndugu zangu wanajamvi hasa sisi vijana ambao bado tunajitafuta,Tujadili tuone namna gani tunajikwamua kiuchumi.

Kama nilivyosema nchi hii(Burundi)inahali mbaya(Maskini)mara 2 au 3 zaidi yetu. Kwahiyo kila kitu ikiwemo huduma za msingi ni tatizo kubwa sana.Tukianza na Umeme sio wa uhakika kabisaa.Maji yanatoka kwa masaa yakitoka mchana,basi usiku hayatoki Achana na Network ambayo 4G bado haijafika takriban nchi nzima a vitu kama ivyo.

Sasa kwenye suala la chakula kuna vitu havikwepeki kama Sukari.Sukari nchini burundi ni adimu sanaaa..hapa naongelea mji mkuu wa bujumbura achana na uko vijijini sijui wana hali gani ndugu msomaji.

Sukari ni adimu kiasi kwamba ukienda kwenye migahawa ukiagiza maziwa na ukataka wakuwekee sukari basi itakubidi uongeze pesa kwa kila kijiko.Na kama ni chai sahau swala la kuweekewa sukari mezani ujipimie kama bongo.Hapa chai utakuta imeshawekewa sukari na ni kidogo sana kiasi inakosa radha.Nyumba nyingi hutumia Asali kama alternative.

Sasa achana na sukari kidogo, MCHELE nao ni tatizo kubwa lingine.kilo ya mchele ni 6k faranga .Sasa ukitazama vitu kama hivi unaona kabisa ni fursa ambayo hawa kina MO Wanajipigia sana pesa huku.

Kama utakua na uhakika wa kupata tani kadhaa kuanzia 1-5 tu kwakuwa sukari inahitaji mtaji mkubwa.Nikuhakikishie vijana wengi wanauwezo wa kupata nusu tani au hata tani 1 ya mchele kwabmtaji wa 5M tu zinatosha kuanza safari.

Twende sawa sasa..

Nitaieleza kiunaga-ubaga.

Hapa utachukua mzigo wako utafunga kwenye Lori.Kisha safari itaanza.Kuna njia ya Kahama utapita hapo kisha utafika sehemu inaitwa Kibanga hapo itabidi ulipie Sumatra sijui TRA ili wakupe kibali cha kuendelea na safari. Baada ya kufika mpakani PASSPORT ni muhimu sanaa. Utaonesha vibali watakupigia mhuri apo boda.

Kisha utaruhusiwa uendelee na Safari.S asa kutoka boda mpaka Bujumbura ambapo ndio Target ya soko linalozungumziwa hapa. Ukifika Buja utafikishwa BANDARINI wanaiita (Buja port) watakagua mzigo wako kama umeweka madawa je? Wakimaliza sasa hapohapo bandarini kama ni mgeni utatafuta maagent wa bidhaa yako. Kama ni mwenyeji Agent atakuelekeza pakufikisha mzigo

Nikuhakikishie ndani ya Siku 2-3 watu wakijua unaSukari wataigombania kama mpira wa kona ndugu msomaji utarudisha mtaji na faida yako kwa haraka sana.Na kama umekaa kizembe utapigwa pesa ndefu sana na uje umlaumu bwana KENGE kwa kukulisha matango pori.

Huku wanasema Sukari ni dhahabu,Lakinu ukiingia kichwakichwa utapigwa vibaya sana.Nisikufiche kama unakuja individual yani wewe,dereva na mzigo kwa mara ya kwanza itakuwa vigumu sana tofauti na makampuni kama MO naona ndo anakimbiza huku na Lake Oil hawa awasumbuliwi sana tofauti na wewe unaekuja individual kama unamoyo mdogo unaweza kukata tamaa mapema sana.

MAMBO YA KUZINGATIA
-Passport ya kusafiria ni muhimu sana lakinimpakani unaweza kuhonga 15k wakakupa kibali

-Vibali vya kubeba mzigo
Yani cha kwanza utaombwa kibali hasa ukiwa TZ.vibali sijui latra,Sumatra,TRA na takataka zote ni muhimu sana.

-CRDB mastercard.
Hapa niwapongeze CRDB kwakuwa ukiwa na mastercard unaweza kutoa pes kwenye ATM zao.Pia utaweza kuona rate ya kubadili pesa Tsh to Faranga

USHAURI..
Tumia kampuni za usafirishaji badala ya kutumia gari ambazo hazijasajiliwa kikampuni.

2.NJIA YA KINYEMELA
Hapa napita juujuu kwakuwa wasakatonge wengi wanapeleka ugali nyumbani watoto washibe kwa njia hii.Haitapendeza kuharibu kwani JF imejaa watu tofauti hata wewe Afisa wa TRA najua utapita hapa kusoma.

Hapa kuna baharia wanapitia L.Tanganyika kufikisha mzigo hapa ni mpaka uwe na connection na warundi wajanja wa hizi kazi.

Lakini pia kuna wataalamu wengine wakwepa (Tax) wanapitisha mzigo vizuri sana mpakani lakini ni mpaka uwe na connection na hao watu na pesa nyingi sana utatoa

Kama unamambo mengine unayajua shusha nondo hapa.Vijana wa Buja wamelala sana wanawaza ULAYA Tuuu yani hakuna kitu utawaambia kuhusu ulaya wakakuelewa.Na hivi wanapata kamteremko flani kwenda huko basi wengi huwaza kwenda uko masaa 24/7

NAWASILISHA HOJA.
WAKO MTIIFU,Jini Genious
Mdau,KENGE 01
Mkuu unaweza nipatia namba yako pm
 
Back
Top Bottom