Rais Samia aendelea kuifungua Tanzania, kuanza ziara ya kikazi Nchini India

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,311
9,739
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha Watanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi nchini India kuanzia Tarehe 6-11 mwezi huu wa October kwa mualiko maalumu wa Rais wa nchi hiyo. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Rais ameambatana na wafanyabiashara wakubwa mbalimbali wa Kitanzania, ambao watapata fursa ya kukutana na wafanyabiashara wakubwa kutoka nchi ya India. Pamoja, watafanya mazungumzo ya kibiashara na kuangalia fursa za kibiashara na uwekezaji baina ya nchi zetu hizi mbili.

Mheshimiwa Rais wetu atapata fursa ya kufanya mazungumzo pia na Waziri Mkuu wa India, lakini pia kuzungumza na wafanyabiashara wakubwa kutoka India, katika jitihada ya kuwavutia kufanya biashara na uwekezaji nchini mwetu katika nyanja na sekta mbalimbali. Ikumbukwe kuwa Tanzania na India zimekuwa na mahusiano ya kidiplomasia ya kihistoria na ya muda mrefu sana. India ni miongoni mwa nchi za kwanza kabisa kufungua ubalozi wake hapa nchini katika miaka ya mwanzoni kabisa baada ya kupata uhuru wetu.

Watanzania, tutegemee kupata fursa mbalimbali za ajira kutokana na uwekezaji mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka nchini India.

Rais Samia anaendelea kuifungua nchi yetu na kuifungulia fursa mbalimbali za kiuchumi. Tunaendelea kuzoa fursa za kibiashara na uwekezaji kutoka kila kona ya dunia. Tanzania inaendelea kuwa chaguo namba moja la wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa kutoka mataifa mbalimbali. Tuendelee kuchangamkia fursa hizi ambazo zinaletwa na Mheshimiwa Rais wetu, ambaye anakesha akitafuta fursa kwa ajili ya Taifa letu.

Ni kupitia uwekezaji na biashara na wafanyabiashara wakubwa kutoka mataifa mbalimbali ambapo tutapata fursa za ajira, ongezeko la mapato, mapinduzi ya viwanda, kilimo, miundombinu, teknolojia, mapinduzi ya kifikra, na kupaa kiuchumi na kimaendeleo kwa Taifa letu.

Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana Mzalendo na Mpenda Nchi Yangu.

Simu: 0742-676627
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha Watanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi nchini India kwa mualiko maalumu wa Rais wa nchi hiyo. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Rais ameambatana na wafanyabiashara wakubwa mbalimbali wa Kitanzania, ambao watapata fursa ya kukutana na wafanyabiashara wakubwa kutoka nchi ya India. Pamoja, watafanya mazungumzo ya kibiashara na kuangalia fursa za kibiashara na uwekezaji baina ya nchi zetu hizi mbili.

Mheshimiwa Rais wetu atapata fursa ya kufanya mazungumzo pia na Waziri Mkuu wa India, lakini pia kuzungumza na wafanyabiashara wakubwa kutoka India, katika jitihada ya kuwavutia kufanya biashara na uwekezaji nchini mwetu katika nyanja na sekta mbalimbali. Ikumbukwe kuwa Tanzania na India zimekuwa na mahusiano ya kidiplomasia ya kihistoria na ya muda mrefu sana. India ni miongoni mwa nchi za kwanza kabisa kufungua ubalozi wake hapa nchini katika miaka ya mwanzoni kabisa baada ya kupata uhuru wetu.

Watanzania, tutegemee kupata fursa mbalimbali za ajira kutokana na uwekezaji mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka nchini India.

Rais Samia anaendelea kuifungua nchi yetu na kuifungulia fursa mbalimbali za kiuchumi. Tunaendelea kuzoa fursa za kibiashara na uwekezaji kutoka kila kona ya dunia. Tanzania inaendelea kuwa chaguo namba moja la wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa kutoka mataifa mbalimbali. Tuendelee kuchangamkia fursa hizi ambazo zinaletwa na Mheshimiwa Rais wetu, ambaye anakesha akitafuta fursa kwa ajili ya Taifa letu.

Ni kupitia uwekezaji na biashara na wafanyabiashara wakubwa kutoka mataifa mbalimbali ambapo tutapata fursa za ajira, ongezeko la mapato, mapinduzi ya viwanda, kilimo, miundombinu, teknolojia, mapinduzi ya kifikra, na kupaa kiuchumi na kimaendeleo kwa Taifa letu.

Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana Mzalendo na Mpenda Nchi Yangu.

Simu: 0742-676627
Anaifungia na si kuifungua, Jana Doha leo India. India anakwenda na ajenda Gani. Zaidi ya kwenda kufungishwa mikataba ya unyonyaji. India juzi wameenda safari na kutua mwezini,yeye ameenda safari ya Qatar. Kipi kipya ambacho Tanzania itaipelekea India. Wajinga na mashetani kama wewe kila siku mapambio ya kusifu hata kama ni ujinga . Mungu chukua shetani huyu haraka
 
Tanzania inashirikiana na India katika mambo mbalimbali sana .India pia limekuwa soko kubwa sana kwa baadhi ya mazao yetu yanayodhalishwa hapa nchini.
 
Anaifungia na si kuifungua, Jana Doha leo India. India anakwenda na ajenda Gani. Zaidi ya kwenda kufungishwa mikataba ya unyonyaji. India juzi wameenda safari na kutua mwezini,yeye ameenda safari ya Qatar. Kipi kipya ambacho Tanzania itaipelekea India. Wajinga na mashetani kama wewe kila siku mapambio ya kusifu hata kama ni ujinga . Mungu chukua shetani huyu haraka
Wanataka majani ya tambuu.

Tanga na Zanzibar ndiyo wazalishaji. Soko hilo linafunguliwa, changamkia fursa.

Unapanda miti ya tambuu hata uwani kwako, kila jani ni mali.
 
Mheshimiwa Raisi tunaomba utumie nafasi hiyo kuomba technology transfer manake wahindi wana viwanda vidogo vidogo huko kwao india kama tunavyoona kwenye tik tok watu wa viwanda vidogo india waletwe huku waajiriwe SIDO na VETA kwani huko kwao wapo wengi wakija huku itakuwa faida kwetu

Mfano wa viwanda vyao vidogo ni vya kutengeneza mazulia,kufua vyuma na kutengeneza majembe mapanga nk, kutengeneza rangi, kutengeneza karatasi, kutengeneza mapambo nk, tuombe watu hawa kupitia ubalozini india na waziri wa mambo ya nje watangaze nafasi za kazi hao watu wa viwanda vidogo waje huku Tanzania kutufundisa uwezo wao tusitegemee tuu malecturer kutoka india
 
Wanataka majani ya tambuu.

Tanga na Zanzibar ndiyo wazalishaji. Soko hilo linafunguliwa, changamkia fursa.

Unapanda miti ya tambuu hata uwani kwako, kila jani ni mali.
Waoneshe mifano basi dada yangu

Ova
 
Wawekezaji gani watakuja sehemu ambayo haina umeme?
Tanzania muda siyo mrefu inakwenda kuwa na umeme wa kutosha mpaka mwingine itauza nje ya nchi.Tunakwenda kuzalisha mega watti 2115 kupitia Bwawa la mwalimu Nyerere pekee,hapo bado vyanzo vingine.
 
Mimi sio mtoto wa kulishwa Propaganda, waambie huko Kijijini kwenu
 
Huo ndio ukweli wenyewe japo unaweza ukaukataa lakini utabaki kuwa ukweli tu.
Wewe utakuwa ni Mtoto mdogo wa Juzi juzi sisi tuliambia na Serikali ya Mwinyi kuwa 'Maji kwa wote ifikapo mwaka 2000" umenielewa my point?

Usituone humu tumekwepa mishale mingi.
 
Back
Top Bottom